Tukio limejirudia tena katika mazingira yaleyale, nikiwa na watu walewale huku tukizungumza maneno yaleyale

Ishantokea sana
 
Nafsi zetu huwa zinaacha mwili tunapata nafasi ya kupumzika (sinzia). Hivyo zinapokuwa kuwa hoko mtaani zinazurura hukutana na nafsi za watu wengine na kufanya mawasiliano kama tufanyavyo tukiwa hatujapumzika.

Hivyo mawasiliano unayofanya na watu pamoja na sehemu unazotembelea ukiwa usingizini hutunzwa kwenye ubongo.
Kuna baadhi ya watu hutunza kwa picha halisi na tukio kamilifu na wengine hutunza kwa kimvuri na tukio likiwa limekatika (pungufu).

Ndio maana ukifika eneo husika au ukikutana na mtu, unakuwa na kumbukumbu kiasi la mtu, kitu au sehemu husika.

Wahenga walisema usimuhadithie mtu ndoto yako ya jana usiku.

Utaratibu wa kunakili ndoto katika maandishi ni muhimu, utakusaidia kupangua baadhi ya matukio hatarishi katika maisha yako.

Hata unabii hushushwa katika mazingira ya namna hiyo.

Usidharau ndoto. Hususan isiyokuwa na uhusiano na matukio ya mchana uliyopita.
 
Wenye uelewa na hilo kuweni specific tupate madini,, maana wengi mnatuacha njiani.
 
75% ya watu waliokuzunguka au watu unaoambatana nao ni WANGA. Huo ndio ukweli ndugu yangu.
 
Maisha ni ndoto tu,, ukweli ni kuwa hata wewe si halisi,, ni ndoto tuπŸ˜‚
 
Kuna kipindi nilikuwa kama naionaga siku nzima ile asubui mikiamka mfano naweza ona siku hio nitapata Ela na kuitumia na kubaki na hata iweje hayo lazima yatimie ila now dayz nahisi sijui Ni nn kimetokea sipati hayo maono ya siku Wala ishara
 
Acha uongo
 
Mie inanitokea sana tu
 
Fafanua mzee kidogo umeniacha ....how mtu ataingia katikati ya mlima , pili kuna uhusiano gani kati ya nafsi na mlima ...kama hutojali tupe madini zaidi
 
Hii ata mimi huwa inanitokea sana, yani sometimes kuna mazingira fulani naweza kuwepo, au kufanya alafu nahisi kwamba hiki kitu au hii sehem mbona nshakuwepo au nshakifanya, lkn nakuwa kama naona labda niliota tu
 

Umemaliza so roho ni uhalisia wa maisha yetu na tunaona future yetu
 
Ndugu tuoe elimu basi tunaoipe da na sisi tunufaike

Ndugu yangu ninavyojua ni hivi

Sisi tunaishi katika sehemu mbili tofauti
ulimwengu tunaojitambua ambao sio halisi ( mwili)
Na ulimwengu tusiojitambua ambao ni halisi (roho)
Sasa ili tuweze kuconnect matukio lazima nafsi itumike kuweka mawasiliano
Binadamu (mwili +nafsi+ roho)

Ukisoma hapo juu kwa waliochangia utapata uelewa zaidi ni mada ndefu kidogo

Na njia pekee tunayoweza kuwasiliana na roho ni ndoto
 
Mhhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…