Tukipika kuku nyumbani, mimi nalishwa vipapatio, vitoto vyangu vya umri wa miaka 5 na 8 ndio vinalishwa mapaja. Je, hii ni sahihi wakuu?

Mfumo wa zamani wa kikoloni ni kutengewa chakula peke yako ndio maana hayo yanakukuta. Ipo siku utawekewa sumu. Kula pamoja na familia yako mezani au na mkeo.

Zamani chakula tulikula kwenye sahani moja na wazazi. Lengo lilikuwa kuona watoto tunavyokula na kutufundisha ulaji mzuri tusijewaabisha ugenini kwa kutafuna kama ng'ombe. Kama kuna vipande vya nyama walianza wazazi kisha mtoto wa mwisho na wengine wanafuata.

Mfumo huu ukaboreshwa ikawa chakula kinawekwa mezani kisha wote tunakutana hapo kila mmoja akijipakulia kinachomtosha. Ukitumia mfumo huu utakula kile unachotaka lakini si vibaya kama wanao wanapenda kula paja wewe ukala kidali au ule mgongo wenye nyama tamu.

Jambo la msingi mchape kwelikweli mkeo atakupa mapaja yote mawili au vipande vyote vya kuku. Wala huhitaji kusema chochote. Amefanya vitendo fanya vitendo. Nafikiri umeelewa.
 
Huyo mama ana akili na anakupenda sana bwashee, the best part kwa kuku ni chicken wings, nenda popote uliza! Vidari vnatengenezewa salad hapewi mtu anayependwa na kuheshimiwa. Vipaja ni vya watoto siku zote kwa tuliofuga kuku tunajua.
 
Mkuu,
Huwa unaongea vizuri sana sana, maturity yako ni zaidi ya umri wako. Hongera.

Nina kanuni hiyo pia, watoto wale vizuri, hizo desturi za zamani kwangu hazina nafasi, japo siwekewi vipapatio ila napenda kuona madogo wanakula vizuri.
 
Paja lake anakupa lote lakini?

Af Kishua, chicken wings(vipapatio) ndo the best.
 
Ulitakiwa upewe makanyagio.

NB: Una uhakika wewe ni baba ya hao inaowaita vitoto vyako?
 
Wanawake wa siku hizi hawajalelewa vizuri.
Wanalea watoto wao kuwa wapinzani wa baba zao, bila kujua kuwa wanapandikiza sumu ambayo huyo mtoto naye atakutana nayo akiwa baba
 
huwezi ukawa mwanaume kamili ukaja kutulalamikia huu ujinga wa maswala ya chakula..... ukiwa mtaani unakula vingapi ambavyo home hawajala...... inaonekana ww ukiwa sehem umekula kitu kitamu huwez peleka home...

punguza kutuaibisha wanaume kama baba gusa kidogo acha umaskini wa kipumbavu
 
Hii lugha ya watu ilikuja na meli
Sio kila kitu unakitafsiri unavyotaka
Km hujui chicken breast we kwenye kuku unakulaga shingo tu au?
Nilitaka kujua tu kama kuku ana manyonyo kama hana basi sawa.
 
Mimi mara nyingi Huwa nagombana na Mke Kwa kunirundikia vyakula ambavyo Huwa naona naleta Kwa Ajili ya Watoto.

By the way hawezi thubutu kunipa vitu vya ajabu ajabu,na pia sijawahi muona mama akimpa baba vitu vya ajabu ajabu na pia baba alikuwa akila hamalizi anatupatia.
 
Hii biashara ya mwanaume kuwahi kurudi nyumbani Ili ule na familia ni ujinga mwingine.

Nitakula nao pale tuu nitakapokuwa around
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ