Tukipika kuku nyumbani, mimi nalishwa vipapatio, vitoto vyangu vya umri wa miaka 5 na 8 ndio vinalishwa mapaja. Je, hii ni sahihi wakuu?

Tukipika kuku nyumbani, mimi nalishwa vipapatio, vitoto vyangu vya umri wa miaka 5 na 8 ndio vinalishwa mapaja. Je, hii ni sahihi wakuu?

Wakuu Bwana Yesu asifiwe!

Ebana kuna issue inanitatiza halafu nimeshindwa kuizungumza kwa mhusika ambae ni wife nikaona nitafute kwanza mawazo humu.

Issue nzima iko hivi, ninavyojua kwa mila na ustaarabu wa kiafrika endapo itatokea familia ikachinja kuku basi baba ndiye mwenye kustahili kula mapaja ya kuku.

Sasa hapa kwangu sielewi wife ananichukuliaje, yaani kila kuku akichinjwa basi mimi father house ntalishwa vipapatio na vitoto vyangu viwili vya kiume vyenyewe ndio vinawekewa mapaja. Hii kitu wakuu inanishangaza kidogo as iko kinyume na mila na desturi za kiafrica.

Wife yeye kwao walikua ni mambo safi hivyo nadhani hawakua watu wa kujali vitu hivyo vidogo vidogo ndio maana anaona ni sawa tu mimi Baba kula vipapatio.

Wakuu, nitumie mbinu gani kumfikishia ujumbe kuwa siridhishwi na kulishwa vipapatio?

Bwana kyagata kwanza nikupongeze kwa kuwa mkweli. Sasa mbinu nzuri hapa ni kuhakikisha wewe unachinja si chini ya kuku wawili. Halafu unamwambia mkeo kabisa kwamba leo wote tule mapaja. Mkiwa mnakula mapaja msifie mkeo kwa upishi wake wa kuku na ukimwambia kuwa umependa sana mapaja.

Siku nyingine nakuhakikishia, mapaja yakiwa yanatosha na wewe utapewa paja tu. Vipapatio baadae.
 
Kwanini mtu mzima upakuliwe chakula? Watoto nyama nzuri kwao ni paja coz ni laini kidari kitafyonzwa kitupwe huko.

Sie kwetu kidari ndio heshima.
 
Hii biashara ya mwanaume kuwahi kurudi nyumbani Ili ule na familia ni ujinga mwingine.

Nitakula nao pale tuu nitakapokuwa around
Kiuhalisia ni muhimu kuwa na mlo mmoja pamoja na familia, ni hizi changamoto za maisha tu ndio zinatuumiza ila pale mezani kuna vingi watoto wanajifunza kupitia kwa wazazi. Usipokula nao nani atawafunza table manners, au tabia nzuri kwa ujumla?
 
Mkuu sio kila mila ni yakuifuata.

Asa nyama nayo ni kero ya kukaza shingo namna hiyo tena wanaokula ni wanao?
Wewe unaongelea kutoka upande wa mapenzi kwa watoto, nakuelewa vizuri kabisa lakini baba kupewa kilichonona si ukandamizaji. Kimsingi, huu utaratibu wa baba kupewa vinono unajenga adabu kwa mtoto, vitu kama kinaa, nafasi ya baba katika familia na kwake yeye kama mtoto n.k

Kutokana na mapenzi kama haya kwa watoto yasiyokuwa na vipimo vya adabu za mila, utaratibu na desturi ndo maana leo hii watoto wengi hawaridhiki na chochote wanachopewa, hawathamini na kuheshimu wazazi wao kwa kuwa wamelelewa wakiwa wao ni kama mabosi wa wazazi wao.
 
Wakuu Bwana Yesu asifiwe!

Ebana kuna issue inanitatiza halafu nimeshindwa kuizungumza kwa mhusika ambae ni wife nikaona nitafute kwanza mawazo humu.

Issue nzima iko hivi, ninavyojua kwa mila na ustaarabu wa kiafrika endapo itatokea familia ikachinja kuku basi baba ndiye mwenye kustahili kula mapaja ya kuku.

Sasa hapa kwangu sielewi wife ananichukuliaje, yaani kila kuku akichinjwa basi mimi father house ntalishwa vipapatio na vitoto vyangu viwili vya kiume vyenyewe ndio vinawekewa mapaja. Hii kitu wakuu inanishangaza kidogo as iko kinyume na mila na desturi za kiafrica.

Wife yeye kwao walikua ni mambo safi hivyo nadhani hawakua watu wa kujali vitu hivyo vidogo vidogo ndio maana anaona ni sawa tu mimi Baba kula vipapatio.

Wakuu, nitumie mbinu gani kumfikishia ujumbe kuwa siridhishwi na kulishwa vipapatio?
Huna haja ya kumfikishia ujumbe. Ukiwa na haja ya mapaja ya kuku pitia bar agiza kuku wako mzima kula.
 
Mimi kama baba mpambanaji nahitaji virutubisho pia nipate nguvu ya kulea familia,nikitoka job napitia zangu mahali nakula hayo mapaja mtoa mada anayosema nikirudi nyumbani Sasa! Nikikuta msosi nadokoa dokoa naita madogo waje wamalizie msosi na watoe sahani na kufuta meza
 
Hii biashara ya mwanaume kuwahi kurudi nyumbani Ili ule na familia ni ujinga mwingine.

Nitakula nao pale tuu nitakapokuwa around
Usilalamike kula vipapatio wakati wanaokula ni wanao. Kama njemba. Kwanza kuku ana vipande vingi vya kula sio lazima ule paja. Sasa kama wanafuta kuku mzima wanakuachia vipapatio jitafakari mwenyewe wapi unakosea
 
Kiuhalisia ni muhimu kuwa na mlo mmoja pamoja na familia, ni hizi changamoto za maisha tu ndio zinatuumiza ila pale mezani kuna vingi watoto wanajifunza kupitia kwa wazazi. Usipokula nao nani atawafunza table manners, au tabia nzuri kwa ujumla?
Watafunzwa na ulimwengu.
 
Kwanini mtu mzima upakuliwe chakula? Watoto nyama nzuri kwao ni paja coz ni laini kidari kitafyonzwa kitupwe huko.

Sie kwetu kidari ndio heshima.

Mimi kwetu shingo na hiki kisehemu cha nyuma cha mkia ndio sehemu za baba.
 
Mwambie kwanzia leo mtakua mnakula pamoja ugali uwekwe kwenye sinia na mboga kwenye bakuli moja alafu mnauzunguka hapo sasa anza undava mtoto akishika paja mdake mkono
 
Back
Top Bottom