Tukisema Royal Tour Tulipigwa tunamaanisha ukweli

Kimsingi hii initiative ni ya kupongezwa tena saana
Kwa jinsi hali ilivyokuwa ni lazima tulitakiwa tuanzie mahali
Kama mdau nimpongeze Mh. Raisi kwa kuona namna utalii unavyoweza kutumia kulingizia taifa pesa nyingi ila wanufaika ni wachache saana,, unapojaribu kuangalia multplier impacct na muingiliano mzima wa sector ya utalii na sector nyingine kama kilimo,,viwanda nk


Hii filamu kwa kiasi kikubwa ILITEKWA,, watu waliokuwa wamemzunguka RAIS walijitwika majukumu ambayo kimsingi hayo majukumu yalikuwa ya wataalamu wa UTALII... na UKARIMU....Ilitakiwa iundwe team ya wataalamu wa UTALII na UKARIMU,,,,, iandae na itambue maeneo, documentary ingechukuliwa na ilitakiwa iwe na series,,,,,mfano Utalii wa wanyama pori,,,, utalii wa utamaduni,,,,,,,Utalii wa uwindaji,,,,,utalii wa fukwe na bahari na maziwa,,,,,,

Hii ingesaidia kuonyesha Uhalisia wa UTALII wa Tanzania na documentary ingekuwa inajitosheleza
TATIzO kubwa la sector ya UTALII Tanzania imevamiwa na watu ambao sio wataalaamu wanatake advantage ya situation na kujipendekeza kwa watoa maamuzi wao wanafikiri kutumia internet ndio kigezo cha kuwafanya kuawa wataalamu ilihali wapo watu wamesomea na wengi hawapewi na wala hawajawahi pewa nafasi kutokana tu na hawafahamiani au hawapo karibu na watoa maamuzi

Anyway tutafika tu japo tutakuwa tumechoka saana
 
Suppose ingetumia 100 billions na kuonyesha tuu the potrait photo ya Samia, kama ilivyo picha ya Mona Lisa iliyochorwa na Leonardo Da Vinci, na hizo billions sio zetu ni za mfadhili wa kujitolea, kuna tatizo gani?.
Hao wafadhili ni kina nani? Kwa nini iwe siri? Ikulu sio sehemu ya kufanyia biashara ya Rasilimali zetu
 
Hoja yangu ni kwamba maadam sio pesa ya umma then tuna hasara Gani?

Hoja ya pili ni kwamba kwa nchi kama yetu watu hujikomba sana kwa Raish hivyo usishangae wafanyabiashara kama Rostam ama Mo walimchangia hiyo movie Ili tu wajiweke karibu na mfumo na sio sababu ya hongo.

Usiri wa serikali hakuna anayependa ila kama Hela sio ya umma mdhamini kujulikana or not Ina faida Gani? Hata sisi huku Chadema tunachangiwa Hela za kampeni sana na wafanyabiashara kwenye kata yetu ila hatujawahi kuwataja. Ila ikiwa pesa ni ya wanachama lazima muitolee hesabu!!
 
Tumepigwa bwana wee
 
Hiyo ya kujikomba kwa mkubwa ili upate upendeleo kwa tafsiri nyingine ni rushwa
 
Wewe ni CDM wa mchongo, endelea kujichomoa fuse.
Hivi Chadema si tunajiita chama Cha demokrasia then ni vizuri tukiheshimu watu kuwa na maoni tofauti. Ndio maana Lissu alipinga Royal tour ila Msigwa aliunga mkono, that's democracy.
 
Duh.... Mbona kwenye Royal Tour hawajaonesha Dodoma
Sijapenda, capital city inatakiwa ipewe heshima yake
 
Punguzeni ujuaji yaani nchi iuzwe kisa billion 5? Mko serious kweli? Hiyo si pesa ya madafu!!

Cha ajabu angechukua pesa serikalini mngesema anatapanya Kodi alichukua Hela private sector mnasema kahongwa Sasa kwa maoni Yako ulitaka pesa itoke wapi?

Nachofahamu Ile ni movie na yenyewe Ina malipo and all that coz inauzwa huko Amazon sijui Sky so Kuna faida inarudi na hapo fungu la mchangiaji linarudishwa.

Tupunguze kelele waTanzania, pesa sio yetu kelele za Nini. Mlitaka atoe pesa yake binafsi?
 
Target group siyo wewe uliyeko hapa!

Wako watu wanahangaika na NATURE...uumbaji wa Mungu!

Hawa ni watu waliovuka hatua tulioko sisi tuliowengi!

Huko ndiko Royal Tour inakobamba!

Tanzania iko kwenye hizo page kwa Sababu ya Dhamira ya Dhati ya Mheshimiwa Rais Wetu!

Doesn't matter how much was spent!

Ni jambo la kusifu na kutia Moyo.
 
Tuna uhakika gani kwamba sio pesa za walipa kodi endapo mpaka sasa hakuna uthibitisho ni kina nani walichangia.
Sasa pesa za umma hamtaki, alafu Bado pesa za kuchangiwa hamtaki, Sasa mnataka Nini zaidi? Au issue ni documentary ndio tatizo sio chanzo Cha pesa?
 
We Jamaa unajifanya mjuzi wa siasa uchwara, uende ukawaibie wananchi kwa hizo siasa zako njaa.

Kuna mfadhili anayeweza akatoa Hundred Billions for free of charge bila ya kupata return yoyote.
Hukana Mpumbavu wa namna hiyo lazima uelewe ''In this world there is no free lunch".

I have already measured your level of stupidity.
 
Hivi Chadema si tunajiita chama Cha demokrasia then ni vizuri tukiheshimu watu kuwa na maoni tofauti. Ndio maana Lissu alipinga Royal tour ila Msigwa aliunga mkono, that's democracy.
Pitia comment uliyoandika, unaamini UBONGO na akili vilishirikiana kuandika uliandika?

Yaani mtu mwenye AKILI timamu uongee kama conman halafu tukuheshimu?
 
Unaamini kuwa unastahili Heshima Kwa comment za aina hii?
 
Huwezi kuwa mwajiriwa wa umma halafu ufanye mambo ya siri then uje kutetea uamuzi huo kisa sio pesa ya umma haina shida, wakati hata makubaliano yao huyajui, usitetee hili jambo.
 
Jamaa kuna kitu huelewi, hapa tuna wasiwasi huenda hayo makubaliano yao ya siri yakasababisha mali za umma kuwekwa rehani mbele ya safari, ndio maana tunataka kujua huyo mfadhili ni nani?

Wewe unaonekana umewekeza akili yako yote kwenye pesa aliyopewa, lakini hujiulizi vipi kama kuna return itahitajika na itatoka wapi?

Au unaamini pia kama ikitokea ikahitajika hiyo return, Rais atatoa pesa mfukoni mwake amrudishie huyo mfadhili?

Come on!.
 
Ile Documentary haikuandaliwa kitaalamu na sijajua ni kwanini iliandaliwa ni a fast track manner kiasi kile.Tulipaswa kufanya utafiti wa kina kwanza kwa kuainisha attractive Tourism Destinations zetu zote kwanza na kutafuta Makampuni bobevu kwenye Tourism Destination Marketing kama ambavyo Egypt wanafanya.Soko la Utalii Duniani ni very competitive,hivyo Market Penetration unahitaji akili kubwa.
Nimeshawashauri serikali way forward mara nyingi sana ila sisi Watanzania tunapenda ujanjaujanja!
Kwa muda wako tafuta hizi clips za nchi ambazo zimefanya vizuri sana kutangaza Utalii wake;
I.Incredible India
II.I love New York
III.Amazing Thailand
Kwa uchache utaona hizi kazi zina wenyewe na siyo yule Journalist Bwana Peter!
 
Makada wa CCM wanaelewa mambo wao kazi yao kisifia tu.National Geographic ni kampuni kubwa sana kwenye anga ya Utalii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ