Tukiwa tunasema Kanisa Katoliki ndiyo Alama rasmi ya Ukristo Tanzania na Duniani muwe mnatuelewa tafadhali

Barikiwa Sana kiongozi wangu [emoji1666]
 
Imani ya Mtu Kama Inakukera Ina Maana Hujakomaa Kwenye Hiyo Uliyopo.... Kuna Kumtafuta Mungu Halafu Kuna Kuwafurahisha Binadamu Wenzio Usikose Wa Kukuzika...
Ni kutokujua Maandiko tu kwani ukizikwa na watu wote walioko duniani ndy utaenda mbinguni??
 
Kumbe hujui hata Ibada ya sanamu![emoji13][emoji13]
Kwa faida yako ibada ya sanamu hii hapa!
[emoji116][emoji116]
KOL. 3:5-6 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.
 
Katoliki hakuna ibada ya sanamu wala hakuna ushoga mkuu si vyema kukashfu imani za watu kwa maneno ya uongo. Kwa hapa wewe una chuki sasa.
Kuipigia magoti sanamu ya huyo mnaemuita bikira Maria sio kuabudu sanamu huko??
 
Ibada ya sanamu maana yake ni ipi kulingana na biblia? hapa nadhani umeandika kitu usichokijua maana yake.
 
Umeniwahi, naamini ameshajifunza.

Hapo kifupi utaona kwamba ibada ya sanamu ni kutii matamanio ya mwili, na akili, kwa kufanya uasherati na mengine mtu anakuwa ameabudu sanamu; lakini pia, Yesu Kristo aliposema hata amtazamae mwanamke kwa kumtamani nae anakuwa amezini rohoni mwake, hapo utaona mtu anaweza kuabudu sanamu kwa matendo ya mwili, na kwa mawazo (kiroho).

Kuabudu sanamu kulingana na biblia sio kuabudu vinyago vya mbao vilivyochongwa kama wengi wanavyodhani.
 
Ukiona shetani anakusifia ni Kwa vile huna madhara nae ( mwenye akili anafahamu)

Ni kweli naunga mkono hoja. Ni kanisa halisi linalo onyesha ukristo wa kweli ulimwenguni.

Na kubaliana na wewe Sana Kuna nidhamu nyingi Sana ndan ya kanisa katoliki kwa viongoz na mambo mengine. Ila umesahau nidham nyingine ambayo nayo tunaishuhudia kanisa katoliki nayo si nyingine bali ni nidhamu ya kuliomba lisanamu lisilo ongea linalofananishwa na bikra Maria eti atuombee sisi wakosefu.

Nimekaa India Sana nimeona wahindu wanavyokuwa na nidham kwa miungu yao hakuna tofauti kanisa ulilosema.

Nakushauri mada yako ungeibadirisha kidogo inaelekea kuponda dini za wengine.

Unaposema kanisa katoliki ndo kanisa la ukiristo wa ukweli unatufanya wengine walutheli tujione tuko makanisa ya ukiristo wa uongo.

Tukianza kuliongelea kanisa lako na ukristo wa ukweli usemao nahis Kama waweza kukwazika.

Rekebisa ujumbe wako la sivyo wanathiolojia tufunguke hapa hapa..........kuanzia karine ya 6BC -hadi 4 AD.
 
Kwa hiyo madhehebu mengine ni magumashi?
 
Papa huyu huyu ambae anaishi kwenye temple lenye alama ya nyoka ndy aongee kibiblia??[emoji15][emoji15]
Hayo ndiyo uliyo karirishwa[emoji13][emoji13]
Hebu Mskilize YESU AKIWAONYA WAFUASI WAKE WW UMESHA KUWA MOSHI PUANI KWA MUNGU
[emoji116][emoji116]
ISA. 65:5-6 watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa. Tazama, neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao;

: MT. 7:1-5 msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

: 1 KOR. 4:1-5 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu. Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu. Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana. Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

TUMSIFU YESU KRISTO MILELE AMIMA[emoji123][emoji123][emoji106]

UNGEKUWA MFUASI WA YESU UNGEYAISHI MAFUNDISHO HAYO!
 
Wewe
Wewe hata biblia huijui, msingi wa kanisa la kikiristo ni huruma ya Mungu isiyo na mipaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…