Nimekuuliza Yesu Alikuwa Anaongea na nani?!
Unaleta mafungu na blabla...
Kwani Aliye kudanganya Ukatoliki ni Jengo nani??[emoji13][emoji13]
Huu Ndio Ukatoli jee ni Majengo??
NGUVU YA KANISA KATOLIKI DUNIANI.
Ukitaka kuona Nguvu ya kanisa katoliki duniani angalia tu mambo machache ambayo yameasisiwa ndani ya kanisa hili takatifu la mitume wa Yesu Kristo na mambo hayo yanafanywa na kufuatwa na madhehebu yote na dini zote, serikali zote na falme zote.
1. CALENDER YA GREGORIAN
Hii ndio kalenda inayotumika duniani kote, kwenye dini zote na madhehebu yote.Hii ndio calendar inayopanga mipango yote kwa kipindi chote cha mwaka katika makampuni,serikali,taasisi na na watu binafsi.Kalenda hii iliasisiwa PAPA Gregory wa Kanisa katoliki,hii ndio calendar rasmi kwa mataifa yote na taasisi zote hata sasa hivi ww usomaye hapa uwe msabato au mwislamu simu yako inatumia system ya Gregorian Calendar.
2.
JUMAPILI [emoji1787]
Najua hapa utabisha,achilia mbali swala la kuabudu katika siku hii,ila ukweli ni kwamba hii ndio siku pekee ambayo dunia mzima inakuwa mapumzikoni katika weekend.Hii ndio siku pekee ambayo karibia asilimia 80 ya ofisi zote duniani,mashule, makampuni n.k yanafungwa kwa ajili ya mapumziko ya weekend.
Waislamu husali siku ya Ijumaa lakini mashule* yanafungwa,maofisi, watu wanakuwa home wamerelax? Hali kadhalika na jumamosi vile vile.Ila ifikapo jumapili dunia mzima inapumzika nyumbani, Jumapili ni zao la kanisa katoliki na inaheshimiwa duniani kote kwa serikali zote na watu wote
3. SIKUKUU YA MTAKATIFU YOSEFU,SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI
Kila Mei Mosi,kanisa katoliki duniani kote huadhimisha sikukuu ya mtakatifu YOSEFU MFANYAKAZI,huyu ndio yule mume wa Maria na Baba mlishi wa Yesu Kristo,makala kuhusu sikukuu hii ipo kwenye page ya Mkatoliki Imara . Sikukuu hii imechukuliwa kama ilivyo na serikali zote ulimwenguni na imekuwa ikitambulika kama Public Holiday.Yaani hata leo hii Rais Mama Samia anahutubia wafanyakazi wote Tanzania kupitia siku hii iliyoasisiwa na kanisa katoliki.Hata wewe leo hii kama ingekuwa sio weekend usingeenda kazini wala hutapata huduma maofisini kwa sababu ya sikukuu hii ya YOSEFU MFANYAKAZI
4. PAPA NA BALOZI WAKE.
Huyu ndio kiongozi pekee wa kidini ambaye ana ofisi ya balozi wake karibia kila nchi duniani,na balozi huyu anatambulika rasmj na serikali za nchi mahalia.Pia hili ni kanisa ambalo makao yake makuu kuna ofisi za mabalozi wa nchi mbalimbali.Kiongozi wa Kanisa hili akienda nchi yoyote ile duniani huwa anapewa heshima ya kipekee zaidi ya kiongozi yoyote yule awe wa kidini au kiserikali.Hii ni nguvu na ushawishi wa kanisa katoliki duniani.
5. BIBLIA
Hili ndio kanisa la kwanza kabisa kuratibu na kuanzisha uandishi wa Biblia.Mtakatifu Jerome ndiye mtu wa kwanza kuandika biblia.Ikumbukwe *kwamba Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vitakatifu vya maandiko ya Mungu.Kwahiyo kazi hii ya kukusanya vitabu hivi na kuvipangilia kwa mpangilio huu unaotumika hadi sasa ulifanywa na kanisa katoliki.Madhehebu yote duniani wanafurahia kazi hii takatifu iliyofanywa na Kanisa katoliki kupitia kwa mtakatifu wake Jerome.
HESHIMA HII YA KIPEKEE HUPATIKANA TU IKIWA KANISA LINAONGOZWA NA ROHO WA MUNGU.
[emoji120][emoji120][emoji1672][emoji1672]