Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil

Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil

Mshambuliaji akiguswa kidogo tu penalty
Zamani haya mambo hayakwepo
 
Mpaka mastaa siku hizi wana sheria za kuwalinda na mabeki
Ndio maana mabeki hawafanyi kazi yao
 
Hat-trick 92 maisha yake yote
Mabao 4 mara 36 maisha yake yote
Mabao 5 mara 6 maisha yake yote
Mabao 8 mara 1 maisha yake yote

Miguu yake yote ilifunga magoli yasiyo na idadi
Kichwa chake kilifunga magoli yasiyo na idadi
Alikuwa na chenga ambazo aliemzidi ni garincha tu
Alikuwa na kasi ya sunami uwanjani
Ndiye mchezaji aliefunga bao bora kuwahi kitokea duniani santos vs juventus

Amecheza match 1385 katika maisha yake yote ya mpira kuliko mchezaji yeyote

Amefunga mabao 1280 katika maisha yake yote ya soka kuliko mchezaji yeyote

Bao lake la 1000 alifunga kwa penalty na mashabiki waliingia uwanjani kusherekea bao hilo kitu kilichopelekea mpira kusimama kwa nusu saa kuwaondoa watu uwanjani

Alianza soka la kulipwa akiwa na miaka 15 tu
Na hat-trick yake ya kwanza alifunga akiwa na miaka 15 mwaka 1956

Brazili haijawahi kupoteza match pele akiwa uwanjani

Takwimu ndio kila kitu zaidi ya hapo ni kudanganyana tu

Jamaa amechezea team 2 tu maisha yake yote huku akitumia muda wake mwingi santos

Fifa wanamtaja kama mchezaji bora kuwahi kuonekana duniani mpaka leo

Ni mchezaji pekee katika hii dunia alietwaa kombe la dunia mara tatu huku akiwa tegemeo kubwa kwa taifa lake la brazili
Mchezaji pekee aliekuwa akiumia mchezoni mashabiki wake wanamlilia mpaka arudi uwanjani

Na huyo ndiye mfalme wa kandanda duniani PELE
Binafsi duniani sijaona mtu kama Messi,,na haitokuja kutokea
 
Unaonyesha jinsi usivyoujua mpira ndugu
Mpira ni takwimu kama unazo toa za messi
Toa za maradona
Ili tuone kama wamemzidi Pele au laa
Sasa unaongea bila takwimu hapa nani mwenye akili atakuelewa?
Kwa sisi tunaoujua mpira duniani kwa upande wa soka Pele ni namba 1 mpaka sasa labda tumsubiri mwingine lakini sio messi wala maradona wala yeyote kwa sasa

Hayo ni mawazo yako tu mkuu, na kujifanya unaujua mpira zaidi ya wengine. Kwaheri!
 
Ukitaka kujua watu wenye chuki na mfalme Messi fuatilia commets zao utajionea. Yote kwa sababu kawagalagaza wazee na vijana 😀😀
Ukiambiwa toa takwimu unabaki unabisha tu
Yaani ukitoa match za kirafiki za santos na taifa lake la brazil
Match za kimashindano za pelle amefunga mabao karibu 800
Sasa ukitoa kwa messi namna hiyo si ajabu akabaki na magoli 250
Hapo kwa mbio hamfikii pele
Sio kwa chenga
Sio kwa lolote
Ingia you tube uwalinganishe utaacha ubishi
 
Siku hizi mpira umekuja kuwa na judgemental za kipuuzi sana ukimuambia mtu flani ni mchezaji mzuri anakuuliza ana magoli mangapi?
Sio magoli tu ndugu vitu vingi alivyokuwa navyo pele kwa sasa hakuna mchezaji football anayemkaribia
 
Watu mnaweza kudhani nina miaka 70 kwa kumpamba pele hapana
Mi mwenyewe ni kijana ambaye hata 27 sina ila nilikuwa mbishi pia kuamini hakuna zaidi ya messi
Mpaka niliposhawishika kuingia YouTube kuwaangalia watu watatu wanaotajwa sana
Pele
Messi
Maradona
Kwa nilichokiona nilimweka pele namba 1
Messi 2
Maradona 3
Nikiri tu maradona hakunishawishi kabisa kati ya huyu pele na messi
 
Takwimu, takwimu, takwimu! Ili takwimu ziwe na maana Mpira wa 1956 pamoja na sheria zake, uimara wa timu pinzani na mbinu za mchezo za wakati huo basi ziwe sawasawa na za wakati huu unapotaka kumlinganisha Pele na wengine wa wakati huu. Kinyume chake unaweza kukuta Pele alishapitwa na wengi kimpira. Takwimu, takwimu, takwimu!
 
Back
Top Bottom