hizi note nazo ni sehemu ya historia yetu
jamani wako wapi magavana kama ndugu yetu GILMAN RUTIHINDA leo mpaka shule iliyopewa jina lake inasadifu wasifu wake!!
je,hakuna vuiongozi tena kama hawa!!??
Nikiwa mmoja wapo; nimemlaumu sana Kambarage kutokana na mambo yaliyotusibu sisi watanzania kama mahindi ya njano na mengineyo, lakini kitu kimoja nampa big Up mzee Kifimbo, ushauri! Tanzania tulikuwa washauri na 'Big brother' kwa nchi nyingi kusini mwa jangwa la sahara. Kitu kidogo kikienda mrama tu, haoooo wanakimbilia Tanzania wanajua watakuja kuwekwa sawa. siku hizi hayo yamepotelea wapi? Ina maana Kambarage kaenda nayo kaburini au ni viongozi wa sasa wanajishughulisha sana na mabiznes diliz wamesahau kuwa kuna kitu kinaitwa kuongoza? mtu na anisaidie....
viongozi wa zamani kwa nini walikuwa hawana matumbo makubwa?
Kishoka,
Baada ya mapinduzi ya Zanzibar na mwungano wa 1964 Abdulrahman Babu alihamia Dar-es-Salaam full time. Kulikuwepo rumours wakati huo kuwa aliogopa kurudi Z'bar kwa sababu alidhania Karume angemkolimba. Hata Salim Ahmed Salim alikuwa hatubutu kuweka mguu wake Zanzibar mpaka mwaka 1975. There's more about Zanzibar and Karume that we simply do not know.
Kuna viumbe wengine wanafurahia sana kufanya uchokozi; dawa yao ni kuwapuuza tu; teh!!!!!! teh!!!!!! teh!!!!!! teh!!!!!!
Mkuu Kichuguu,
Na wenine wote mlibandika picha zaidi heshima mbele sana, mkuu umenimaliza sana na picha ya timu za mpira, ninaikumbuka sana na kwa makini picha ya timu ya Yanga,
1. Waliosimama kutoka kushoto ni Athumani Kilambo, Adam Juma, Elias Michael, Selemani Said, Abdurahaman Juma (Captain), na Mwamba Omar Kapera.
2. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Moshi Dayani, Maulidi "Mexico" Dilunga, Clement Joseph, Bona Max, na Sembuli.
Waliokosekana hapo ni Sunday "Computer" Manara, Kitwana Manara, Vivian, Muhidin Fadhili, Leodgar Tenga na Leornad Chitete. Ni baada ya hii safari ndipo walirudi bongo na kuja kupambana na timu maarufu sana ya Nigeria kwa jina la Enugu Rangers, ninakumbuka sana jinsi wananchi wengi tulivyolia machozi pale Uwanja Wa Taifa baada ya hii, yaani a heart breaking game ilikuwa ni pamabano la Raundi ya pili ya kombe la Afrika, yaani Osagefyo Kwame Nkurumah Cup, si unajua siku zile kipindi cha michezo saa mbili kassoro na mtangazaji Abdul Masudi Jalewa "The Jaws" yaani mkitoka mpirani ni lazima tena muikalie chini Radio Tanzania kusubiri michezo,
Mkuu siku ile wa-Nigeria walituweka bao moja tu, na ninakumbuka ile timu walikuwa na wachezaji wawili sijawasahau mpaka leo, yaani kpa wao Emmanuel Okalla, na Sentahaafu wao Chwuku, the high level ya perfomance ya ule mpira, sidhani kama imeshawahi kutokea Tanzania tena hivi karibuni, maana ule ulikuwa ni mpira hasa, na hasa Yanga, ambao walirudi kutoka Brazil na staili moja bongo tulikuwa tunaiiita Diognal style na kuwategea wachezaji wa timu ya adui waonekane wameotea kila wakati.
Ahsante mkuu Kichuguu, picha safi sana, Mkulu Kibunango, naomba mkuu ziweke sawa picha za wakulu hapo ambazo ziko wkenye link, yaani ziweke wazi! Duh elimu kubwa sana hapa!
nilisikia ete temeke wailes,jina limetokana zamani kulikuwa kituo cha WIRELESS communication
alaafu kariakoo jina ni sababu watumwa wakifikishwa hapa hukata tamaa hence the word kariakoo lakini wengine usema it was because kulikuwa base ya askari wa CARRIER CORPS na pronoucement ya kiswahili ikawa kariakoo
sanamu la askari,katikati ya jiji,originally ilikuwa ni sanamu ya a german general jina nimemsahau
hivyo daraja la salender lilijengwa na nani,na mwaka gani,the name suggests,it was not german made,au it was by another name.and again oysterbay ilijengwa na mjerumani au mwingereza
nilisikia ete temeke wailes,jina limetokana zamani kulikuwa kituo cha WIRELESS communication
alaafu kariakoo jina ni sababu watumwa wakifikishwa hapa hukata tamaa hence the word kariakoo lakini wengine usema it was because kulikuwa base ya askari wa CARRIER CORPS na pronoucement ya kiswahili ikawa kariakoo
sanamu la askari,katikati ya jiji,originally ilikuwa ni sanamu ya a german general jina nimemsahau
hivyo daraja la salender lilijengwa na nani,na mwaka gani,the name suggests,it was not german made,au it was by another name.and again oysterbay ilijengwa na mjerumani au mwingereza
Ninavyofahamu ni kuwa:-
Watumwa waliambiwa wakate tamaa ni Bagamoyo. Na hasa waliambiwa BWAGAMOYO, umeshakuwa mtumwa tayari.
KARIAKOO ni kuwa kulikuwa na GOGO hapo, na hivyo hiyo sehemu walikuwa wakiita KALIA-GOGO. Msasani ni KWA MUSA HASSAN (Wamakonde hao wakasema KWA MUCHA-ACHANI)...... Chekeleni ni CHECK LINE, ShokaMzoba ni Shock Absorb, Fulumasinonda ni FULL MACHINE in ORDER, fingapointi ni Finger-Print...........