Son of Alaska
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 2,812
- 1,061
[media]http://rspringwater.com/images/EastAfrica_UhuruParadeGround_jpg.jpg[/media]
kwata la uhuru Tanganyika 1961....click to enlarge the picture!
Yes, Mzee Mchongoma umenikumbusha mbali sana. Nilipanda EAA ningali mdogo kutoka Musoma kwenda Tabora; nadhani mwaka 1968 hivi. Kila mtu ndani ya ndege ile alikuwa kavalia vizuri sana utadhani nini. Wale akina dada waliokuwa wakihudumia walionekana wazuri kweli kweli. Nadhani enzi hizo tulikuwa na ulimbukeni sana na usafiri wa anga.
nasema tena shukrani wakuu wa thread hii...mnakumbuka wakati wa kumaliza mgambo ile nyimbo?Nadhani kuna watu hatambui kuwa Mzee kawawa alikuwa ni mmoja wa kuruta wa kwanza kwanza wa JKT pale Ruvu. Kwenye picha hii Mzee Kawawa ni huyu wa pili kwenye msitali wa mbele, mfupi na mwenye kitumbo kikubwa kuliko wote. Pich hii ilipigwa wakati wa pass-out parade, sikumbuki mwaka gani lakini ni kati ya mwaka 1968 na 1970 hivi.
...enzi hizo, East African Airways wanatesa na Dakota ilokuwa inatua mpaka Kilwa Airport!, halafu kulikuwa na DC-8, DC-9 na DC-10 ilokuwa na regular trips to London!
Mkuu Mwanzage,
Maneno mzito sana, binafsi nitakutafuta week end unajua mashughuli sasa hivi, lakini tutazungumza zaidi.
Labda ni vizuri pia kujikumbusha muungano kwa vile uko kwenye msukosuko sasa hivi:
Wino unaangushwa rasmi kuhalalisha muungano
Maelezo ya picha hii yanaeleweka
Nyerere anachanganya mchanga wa Zanzibar na Tanganyika kukamilisha zoezi la Muungano.
Ndani ya bunge, Nyerere na Karume wanabadilishana hati za kisheria kukamilisha zoezi la muungano.
Mwanzilishi FMES na wachangiaji wengine wote. Thread hii imneivutia sana kwa kutukumbusha tulikotoka. Ngoja sasa niwageuzie upande wa mpira wa Miguu. Kwa bahati mbaya wachezaji wengi siwafahamu kwa vile tulizowea kukariri majina zaidi wakati huo. Anayejua majina asaidie kutukumbusha.
Hii ni Timu ya African Sports ya Tanga mwaka 1974: Waliopo ni pamoja na kipa Omar Mahadhi, Mwabuda, Sharif, Abdallah Luo(mrefu) Hemedi Seif, Omar Zimbwe, Zacharia Kinanda
Na hii ni Coastal Union ya Tanga mwaka huo huo wa 1974. Waliopo ni pamoja na Salim Amri, Jalala, Omar Bafadhili, Mohamed Salim.
Hii ni timu ya yanga wakiwa ziarani Brazil mwaka huo huo wa 1974; waliopo ni pamoja na Bona Max, Maulid Dilunga, Michael Clement, Moshi Dayan na Gibson Sembuli, Leodgar Tenga, Athumani Kilambo, Elias Michael, Said Sanga, Abdulrahman Juma na Omar Kapera. Nadhani kuwa sunday Manara alikuwa keshaenda Austria kucheza kandanda ya kulipwa wakati huo.
Sikuweza kupata picha za Simba na Cosmo wakati huo. Nadhani timu za Red Devils na Pan African zilikuwa hazijaanzishwa mwaka huo wa 1974.
Yes, Mzee Mchongoma umenikumbusha mbali sana. Nilipanda EAA ningali mdogo kutoka Musoma kwenda Tabora; nadhani mwaka 1968 hivi. Kila mtu ndani ya ndege ile alikuwa kavalia vizuri sana utadhani nini. Wale akina dada waliokuwa wakihudumia walionekana wazuri kweli kweli. Nadhani enzi hizo tulikuwa na ulimbukeni sana na usafiri wa anga.
Hii picha imenipa huzuni sana...hayo maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa na nguvu sana.
Maneno haya kwa kiasi kikubwa yanatoka katika sala maarufu sana ya Mt. Francis wa Asizi (1182 - 1226). Hii sala inabeba ndani yake ambacho haswa Biblia inasema kuhusu kuwa Mkristu.
Wanasiasa wanaoenziwa hakuna chochote cha maana walichokifanya zaidi ya kuongoza juhudi za kugombea uhuru. Hatuna wataalamu wa maana ktk hizo fani zote ulizozitaja. Tungekuwa nao tungekuwa tumeendelea. Ngoja nikuulize, hivi kuna mtaalam gani wa maana ktk uchumi ambaye angeendelea kukumbatia sera ya ujamaa na kujitegemea huku akiona kuwa haifanyi kazi? Hao ma injinia unaotaka tuwaenzi wameshindwa hata kutatua matatizo ya kilimo, umeme, maji masafi, n.k. Sasa tuwaenzi kwa kitu gani? Watu bado wanaugua magonjwa kama ya kichocho, utapiamlo, kisonono, na mengine mengi tu. Hao wataalamu wa afya na tiba wamefanya nini kuangamiza magonjwa kama hayo yanayoweza kuangamizwa? Jibu ni hakuna!! Sasa tuwaenzi wataalamu wa fani ulizotaja kwa minajili ipi?