Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

due to world shortage,in vegetable oils,the then british labour government,emanicipated The Tanganyika Groundnut scheme,hii ilikuwa late 1940's.it was decided to grow peanuts in kongwa(dodoma) on a large extensive scale,feasibility studies ziliconclude mradi ukikamilika,tanganyika itakhidi mahitaji ya vegetable oil duniani.the project cost a COLLOSSAL £ 49 million,this was a massive project.it FAILED,and almost led to the downfall of the labour government.huu mradi it is still talked about today,sababu it was massive.had the project succeded DODOMA and tanzania in general would have greatly benefited
 
Hii Thread nikiisoma najiskia raha na kupumizisha kichwa na maskendo ya EPA etal.......Big up wachangiaji na muanzisha Thread.....
 
jamani mbona our fathers,and grandfathers waliopigana the great war,for queen and country,tumewasahau,i am sure lazima katika second world war,tulikuwa na mashujaa wazalendo,nakumbuka one or two,the late mzee barakati,the late makutika.nakumbuka nikiganda na bumbuwazi wakati marehemu mteketa akinieleza exploit zake as a signaller in varios theaters of war notably mauritius,ethiopia,south africa,burma.akiwa sudan alimuona captain mweusi for the first time,alikuwa mnubi,jitu la foot saba na ushee
 
Wazo zuri sana Field Marshall ninaomba ulikuze liwe ni kuanzisha na kutunza VIRTUAL NATIONAL PICTURES MUSEUM GALLERY ONLINE!
 
[media]http://rspringwater.com/images/EastAfrica_UhuruParadeGround_jpg.jpg[/media]


kwata la uhuru Tanganyika 1961....click to enlarge the picture!

Aaah mkulu umenikumbusha kofia za tarbushi hapo.......Kumbe zilikuwepo kwa armed forces pia....Dah si unaona historia ilikuwa imeingia vumbi kichwani mwangu sasa. Ahsante mkuu...
 
Yes, Mzee Mchongoma umenikumbusha mbali sana. Nilipanda EAA ningali mdogo kutoka Musoma kwenda Tabora; nadhani mwaka 1968 hivi. Kila mtu ndani ya ndege ile alikuwa kavalia vizuri sana utadhani nini. Wale akina dada waliokuwa wakihudumia walionekana wazuri kweli kweli. Nadhani enzi hizo tulikuwa na ulimbukeni sana na usafiri wa anga.


attachment.php


Wacha weee picha za ndege zimenikumbusha looongi....mzee akiondoka au akirudi ilikuwa tunagombania kwenda kumsindikiza au kumpokea mi na masiblings wangu....ilikuwa lazima ugomvi, hadi faza na maza wakaweka zamu...dah zamani wakulu.
 
Nadhani kuna watu hatambui kuwa Mzee kawawa alikuwa ni mmoja wa kuruta wa kwanza kwanza wa JKT pale Ruvu. Kwenye picha hii Mzee Kawawa ni huyu wa pili kwenye msitali wa mbele, mfupi na mwenye kitumbo kikubwa kuliko wote. Pich hii ilipigwa wakati wa pass-out parade, sikumbuki mwaka gani lakini ni kati ya mwaka 1968 na 1970 hivi.

attachment.php
nasema tena shukrani wakuu wa thread hii...mnakumbuka wakati wa kumaliza mgambo ile nyimbo?
kumaliza mgambo wetu ni kazi ngumu saaana!(*2)
Hata ndege wa ngani wanaruka ruka(*2)

siku hizi hata jeshi wametoa sia ajabu vijana wanakosa uzalendo....
 
...enzi hizo, East African Airways wanatesa na Dakota ilokuwa inatua mpaka Kilwa Airport!, halafu kulikuwa na DC-8, DC-9 na DC-10 ilokuwa na regular trips to London!

Unajua the sad news ni kwamba ni Nkurumah, ndiye aliyepigana sana kuiuwa EAA, na aliweza kum-recruite Njonjo akishirikiana na Makaburu wa Africa Kusini, na Muingereza Tiny Rowland,

Nkurumah, alitaka kuwe na muungano wa Afrika nzima, huku yeye akiwa rais wake wa kwanza, Mwalimu akawa a big competititor wake kwa sababu, tayari Mwalimu alikuwa na Muungano wa Tanzania, na EAA hivyo viongozI wengi wa Africa, walikuwa wako radhi kumsikiliza Mwalimu zaidi on this ishu ya muungano kuliko Nkurumah, ambaye hakuwa na any experience. Kuona hivyo Nkurumah akaanza hizo njama, ambazo baadaye zilizaa matunda ya kuvunjika kwa Jumuiya, ambako Kenya ndio waliofaidika sana na matokeo kwa sababu waliweza ku-retain mali nyingi sana za Jumuiya kuliko nchi zingine yaani sisi Tanzania na Uganda.

Mkuu Kichuguu, Ahsante kwa hizo picha kati ya hao ma-Air Hostess wa EAA, kuna mama mmoja ninaishi naye karibu sana, yaani hata leo akisema kuwa aliwahi kuwa one of hao kina mama huwa tunakufa sana na kucheka na hata yeye mwenyewe hucheka sana, lakini off course ujana na uzee ndio maisha na owte siku moja tutakuwa hivyo, kama tutafanikiwa kuishi kwa muda mrefu maana kila siku life expectency huku kwetu Africa inazidi kushuka tu, nafikiri kama sikosei mara ya mwisho ilikuwa ni miaka 37 tu! Damn it!
 
Wakuu mi nimeonelea ni vema kuwa na suala la kama kitabu/kijarida kikiwa na picha pamoja na maelezo mengine yoote kuhusiana na picha hizi kama hatujawa nacho bado. Ngoja niangalie kama itawezekana tutengeneze kitabu/kijarida kikiwa na mambo yoote haya. Nitarudi na jibu kama wanajamvi mtakubaliana na hili. Nawakilisha.....
 
Mkuu Mwanzage,

Maneno mzito sana, binafsi nitakutafuta week end unajua mashughuli sasa hivi, lakini tutazungumza zaidi.
 
huyu mwingereza,TINY ROWLAND,amezivuruga sana serikali za africa,ametumia sana mali za LONRHO kuziyumbisha nchi za kiafrika,in fact this man was almost a behind the scenes president of many african countries,coup de tat nyingi africa,his name cropped up.HATA nyerere,tough as he was,amewahi kuwa cornered na TINY.in one of his speeches,nyerere amewahi kusema 'aka kaTINY kana mambo makubwa kuliko jina lake'
 
Labda ni vizuri pia kujikumbusha muungano kwa vile uko kwenye msukosuko sasa hivi:


attachment.php

Wino unaangushwa rasmi kuhalalisha muungano

attachment.php

Maelezo ya picha hii yanaeleweka
attachment.php


Nyerere anachanganya mchanga wa Zanzibar na Tanganyika kukamilisha zoezi la Muungano.

attachment.php

Ndani ya bunge, Nyerere na Karume wanabadilishana hati za kisheria kukamilisha zoezi la muungano.

Sasa hizi hati ndio tunataka tuzione. Ili tuegemeze Muungano wetu kutokana na hati hizi. Vinginevyo inakuwa ni usanii tu.
 
Mwanzilishi FMES na wachangiaji wengine wote. Thread hii imneivutia sana kwa kutukumbusha tulikotoka. Ngoja sasa niwageuzie upande wa mpira wa Miguu. Kwa bahati mbaya wachezaji wengi siwafahamu kwa vile tulizowea kukariri majina zaidi wakati huo. Anayejua majina asaidie kutukumbusha.


Hii ni Timu ya African Sports ya Tanga mwaka 1974: Waliopo ni pamoja na kipa Omar Mahadhi, Mwabuda, Sharif, Abdallah Luo(mrefu) Hemedi Seif, Omar Zimbwe, Zacharia Kinanda

attachment.php

Na hii ni Coastal Union ya Tanga mwaka huo huo wa 1974. Waliopo ni pamoja na Salim Amri, Jalala, Omar Bafadhili, Mohamed Salim.

attachment.php

Hii ni timu ya yanga wakiwa ziarani Brazil mwaka huo huo wa 1974; waliopo ni pamoja na Bona Max, Maulid Dilunga, Michael Clement, Moshi Dayan na Gibson Sembuli, Leodgar Tenga, Athumani Kilambo, Elias Michael, Said Sanga, Abdulrahman Juma na Omar Kapera. Nadhani kuwa sunday Manara alikuwa keshaenda Austria kucheza kandanda ya kulipwa wakati huo.

attachment.php


Sikuweza kupata picha za Simba na Cosmo wakati huo. Nadhani timu za Red Devils na Pan African zilikuwa hazijaanzishwa mwaka huo wa 1974.


Mkuu, pongezi kwa nukuu yako lakini naomba kuchangia kidooogo kwenye baadhi ya data zako. Hiyo picha ya Coastal Union ni ya mwishoni mwa mwaka 1975 ama mwanzoni mwa mwaka 1976 na ndio maana wamo pia Saidi Jacky, Mwihaji Ally, Mohamed Kampira na Salim Omar ambaye alianza kuichezea Coastal Union mwaka 1975 akiwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza pale Usagara Sec School.

Hiyo picha ya Yanga ilipigwa mwanzoni mwa mwaka 1974 Yanga ilipokwenda Brazili na Simba kwenda Poland na ziliporudi zikaenda moja kwa moja Mwanza kushiriki michuano ya klabu bingwa ya Tanzania ambapo zilifanikiwa kufika fainal kwenye uwanja wa Nyamagana na Yanga kuilaza Simba 2-1 wafungaji wakiwa Sunday Manara na marehemu Gibson Sembuli.
Katika kikosi hicho cha Yanga kilichokwenda Brazil Tenga alikuwa hajajiunga na Yanga kwa sababu yeye alijiunga mwaka 1974 mwishoni akiwa pamoja na Muhaji Mukhi, Juma Matokeo, Patrick Nyaga, Juma Shabaan na Jellah Mtagwa wote wakitokea Morogoro baada ya michuano ya Taifa Cup ya mwaka huo.
Pia Sunday Manara alikwenda Austria mwanzoni mwa mwaka 1976.

Timu ya Yanga ilicheza na timu ya Enugu Rangers International mwezi May mwaka 1975 ukiwa ni mchezo wa pili wa raundi ya pili wa kombe la klabu bingwa Afrika baada ya kutoka sare ya 1-1 wiki mbili kabla huko Nigeria. Yanga ilitakiwa kutoa draw tu ya kutofungana isonge mbele lakini dakika za mwanzo tu za kipindi cha kwanza wakapigwa kimoja kilichokaa hadi mwisho wa mchezo na kuacha umati mkubwa wa watanzania ukibubujikwa na machozi. naunga mkono mchangiaji mmoja kuwa huu ulikuwa miongoni mwa michezo ya kusisimua sana iliyopatwa kuchezwa Uwanja wa taifa.

naomba kuwakilisha.
 
Yes, Mzee Mchongoma umenikumbusha mbali sana. Nilipanda EAA ningali mdogo kutoka Musoma kwenda Tabora; nadhani mwaka 1968 hivi. Kila mtu ndani ya ndege ile alikuwa kavalia vizuri sana utadhani nini. Wale akina dada waliokuwa wakihudumia walionekana wazuri kweli kweli. Nadhani enzi hizo tulikuwa na ulimbukeni sana na usafiri wa anga.


attachment.php



...Hiyo ya Pili yenye bawa la nyuma la juu ilikuwa ni Vickers 10 ama VC 10 miongoni mwa ndege zilizotamba sana miaka ya 60 na 70 mwanzoni!
 

Hii picha imenipa huzuni sana...hayo maneno ya Mwalimu Nyerere yalikuwa na nguvu sana.
Maneno haya kwa kiasi kikubwa yanatoka katika sala maarufu sana ya Mt. Francis wa Asizi (1182 - 1226). Hii sala inabeba ndani yake ambacho haswa Biblia inasema kuhusu kuwa Mkristu.


PRAYER OF SAINT FRANCIS
Lord, make me an instrument of your peace,
Where there is hatred, let me sow love;
where there is injury, pardon;
where there is doubt, faith;
where there is despair, hope;
where there is darkness, light;
where there is sadness, joy;
O Divine Master, grant that I may not so much seek to be consoled as to console;
to be understood as to understand;
to be loved as to love.

For it is in giving that we receive;
it is in pardoning that we are pardoned;
and it is in dying that we are born to eternal life.
 
Wanasiasa wanaoenziwa hakuna chochote cha maana walichokifanya zaidi ya kuongoza juhudi za kugombea uhuru. Hatuna wataalamu wa maana ktk hizo fani zote ulizozitaja. Tungekuwa nao tungekuwa tumeendelea. Ngoja nikuulize, hivi kuna mtaalam gani wa maana ktk uchumi ambaye angeendelea kukumbatia sera ya ujamaa na kujitegemea huku akiona kuwa haifanyi kazi? Hao ma injinia unaotaka tuwaenzi wameshindwa hata kutatua matatizo ya kilimo, umeme, maji masafi, n.k. Sasa tuwaenzi kwa kitu gani? Watu bado wanaugua magonjwa kama ya kichocho, utapiamlo, kisonono, na mengine mengi tu. Hao wataalamu wa afya na tiba wamefanya nini kuangamiza magonjwa kama hayo yanayoweza kuangamizwa? Jibu ni hakuna!! Sasa tuwaenzi wataalamu wa fani ulizotaja kwa minajili ipi?

Samahani Labda nakurudisha nyuma sana. Je si kunatofauti kubwa sana kati ya kuwa na wataalamu na kuwatumia wataalamu hao? Tatizo kubwa kwa TZ ni kutojali na kutumia wataalamu wetu. Mbona wakienda kwenye mashirika ya njee they do wonders?
 
Heshima mbele kwa FMES kwa kuanzisha hii thread. Kwa kweli inaburudisha na inatukumbusha mbali na pia inatufundisha mengi.
 
Back
Top Bottom