John Steven Akhwari akimaliza mbio za marathon katika olimpiki ya mwaka 1968 Mexico City, saa moja baada ya washiriki wote kumaliza mbio hizo.
John anakumbukwa dunia nzima kwa kauli yake hii
"My country did not send me 7000 miles away to start the race. They sent me 7000 miles to finish it."
1. ABDULRAHAMAN BABU na NYERERE wote walikuwa wasocialist waliobobea,
2. tofauti zao ilikuwa ni njia za kuufikia huo usocialist,whereas nyerere alitaka african socialism,ujamaa ambao centered around utu na ubinadam,
3. whereas babu,alihisi ujamaa huu ungechelewesha maendeleo.yeye aliadvocate scientific socialism based on the advancement of factors of production,
4. hapa palikuwa patamu moto uliwaka chinichini.masikini tanzania yetu,sijui vichwa kama hivi tutavipata wapi tena
Kwa sasa nawakumbushia Shem Kalenga aliyekuwa gwiji wa muziki pale mtaa wa Lumumba akiwa na Tabora Jazz enzi hizo akitoa vitu kama Dada Asha No 1, 2, 3, 4; Alhamdulilah; Serafina; Mariamu na vinginevyo vingi vilvyohusu Wazee wa Kazi:
Filbert bayi alivunja rekodi ya dunia ya mita 1500 kwenye michezo ya jumuia ya madola huko Christchurch New Zealand mwaka 1974, baada ya kuwa amempiku Kipchoge Keino wa Kenya kwenye mashindano ya Afrika mwaka 1973,
Ila, Bayi alinivunja mbavu sana alipokuwa akiongea na BBC mwaka 1980 au 81 hivi alipoulizwa kuhusu mipango yake ya baadaye kwa vile umri ulikuwa unaanza kumpinga kuendela na riadha. Akakurupuka na kudai kuwa watu walikuwa wanamwonea wivu tu, hata hivyo yeye alishakuwa ni afisa wa jeshi la wananchi wakati huo kwa hiyo hakuwa na wasiwasi wowte
Inasikitisha sana kuwa watu kama Babu ambao nje ya Tanzania walionekana kama lulu, nchini kwao walitazamwa kama wahaini. Sina hakika kama hii ni matokeo ya ujinga wa watanzania au la,
lakini jana tu nimeshuhudia waandamanaji wa CCM waliokuwa wakiandamana kupongeza hotuba ya Kikwete wakizomewa na baadhi ya wananchi
Kama nilivyoahidi kuhusiana na comment yangu hapo juu; well nimecheki na nimeona inawezekana lakini sharti kwa kupata ushirikiano wa dhati kutoka kwenu, isije ikatokea yaleeee ya t-shirts. Mwenye maoni.....nasikiliza.Wakuu mi nimeonelea ni vema kuwa na suala la kama kitabu/kijarida kikiwa na picha pamoja na maelezo mengine yoote kuhusiana na picha hizi kama hatujawa nacho bado. Ngoja niangalie kama itawezekana tutengeneze kitabu/kijarida kikiwa na mambo yoote haya. Nitarudi na jibu kama wanajamvi mtakubaliana na hili. Nawakilisha.....
Mkuu Kichuguu,
1. Heshima mbele tena, hapa naona Shem Karenga alikuwa very young na pia inakumbusha sana enzi zile za Tabora Jazz, yaani wana-Segua Segua, kwa kweli na wao walitamba sana na kuweka signature kubwa sana kimuziki nchini, na wao pia walikuwa wakisikika sana kwenye Radio Bukavu, na hata gwiji mmoja wa muziki kule Zaire, Kitonzengu Lokassa ya Mbongo ambaye originally, alianzia kwa Tabu Ley, alikuwa na heshima kubwa sana na Karenga mpaka akaamua kurudia kwa ku-modify wimbo wake wa Asha akiu-mix na ule mwingine Rosa, uliopigwa na Wema Abdallah, akiwa na Western Jazz,
2. Bendi hizi mbili yaani Western na Tabora, zilikuwa na uhusiano wa karibu sana enzi hizo, kwa sababu Wema Abdallah alitokea Tabora Jazz, kabla hajahamia Western Jazz, yaani Siku Kuu Street, hapa Kariakoo. Siku zote walikuwa na mahusiano ya karibu na hata kumpelekea Wema kupiga kibao kimoja akiwa na Western, cha "Huenda Tutarudiana" ambacho kilitamba sana in the 70s, chenye tafsiri ya kuwa huenda siku moja atarudiana na Tabora Jazz, ambayo siku zote alikiri kuikumbuka sana.
3. Tabora Jazz ni moja ya bendi ambayo baadye in the 80s, ilikuja athirika na mabadiliko ya kiuchumi nchini, ambapo matatizo ya uchumi yalitupelekea enzi hizo wa-Tanzania wengi kuamini kuwa vitu vizuri vilikuwa ni vya kutoka nje tu ya nchi yetu lakini sio vyetu wenyewe, kasumba hii ndio iliyotuplekea wananchi wengi kuwathamini sana mabaharia waliorudi kutoka nje, au mwananchi yoyote aliyefanikiwa kuishii nje, tulifkia mahali muziki wetu wa local Discos ulikuwa ni wa nje tu, hivyo bendi hii ikaishia kufa kifo cha mende,
4. Lakini baadaye Shem Karenga, alijiunga na bendi mpya iliyoanzishwa na Msilwa (Twanga) na Martin (FM-Academia), yaani bendi ya MK.Group, pale New Africa Hotel, iliyowajumisha kina Kassongo Mpinda (Marquis), Mzee Mwema Mudjanga (Mzee Chekeeeencha-Marquis), Nkurlu Wabangoi (Marquis), Mbombo Wa Mbombo-Ka (Safari Sound) na wengineo wazawa, bendi hii ilivuma sana mwanzoni mwa 90s, mpaka waanzilishi wa bendi hii walipoamua kuachana na kuanzisha bendi zao za sasa, Shem alijaribu kupiga muziki wa solo kwenye mahotel makubwa, lakini hakufika mbali sana.
Since then sijamsikia tena mwanamuziki huyu, Karenga ambaye kwa kweli alikuwa ni mmoja wa mabingwa wa muziki nchini.
Mada hii baaabu kubwa sanaaaa yaani Jamii Forums inabidi kujiweka sawa na kuanzisha kumbukumbu hizi kisha kuzikabidhi Makumbusho!...FMES mkuu wangu hongera sana kwa kutoa hoja hiii...
Ni muhimu sana kwa sababu vijana wengi hawafahamu kabisa tulitoka wapi!...