Mkuu Kichuguu,
1. Heshima mbele tena, hapa naona Shem Karenga alikuwa very young na pia inakumbusha sana enzi zile za Tabora Jazz, yaani wana-Segua Segua, kwa kweli na wao walitamba sana na kuweka signature kubwa sana kimuziki nchini, na wao pia walikuwa wakisikika sana kwenye Radio Bukavu, na hata gwiji mmoja wa muziki kule Zaire, Kitonzengu Lokassa ya Mbongo ambaye originally, alianzia kwa Tabu Ley, alikuwa na heshima kubwa sana na Karenga mpaka akaamua kurudia kwa ku-modify wimbo wake wa Asha akiu-mix na ule mwingine Rosa, uliopigwa na Wema Abdallah, akiwa na Western Jazz,
2. Bendi hizi mbili yaani Western na Tabora, zilikuwa na uhusiano wa karibu sana enzi hizo, kwa sababu Wema Abdallah alitokea Tabora Jazz, kabla hajahamia Western Jazz, yaani Siku Kuu Street, hapa Kariakoo. Siku zote walikuwa na mahusiano ya karibu na hata kumpelekea Wema kupiga kibao kimoja akiwa na Western, cha "Huenda Tutarudiana" ambacho kilitamba sana in the 70s, chenye tafsiri ya kuwa huenda siku moja atarudiana na Tabora Jazz, ambayo siku zote alikiri kuikumbuka sana.
3. Tabora Jazz ni moja ya bendi ambayo baadye in the 80s, ilikuja athirika na mabadiliko ya kiuchumi nchini, ambapo matatizo ya uchumi yalitupelekea enzi hizo wa-Tanzania wengi kuamini kuwa vitu vizuri vilikuwa ni vya kutoka nje tu ya nchi yetu lakini sio vyetu wenyewe, kasumba hii ndio iliyotuplekea wananchi wengi kuwathamini sana mabaharia waliorudi kutoka nje, au mwananchi yoyote aliyefanikiwa kuishii nje, tulifkia mahali muziki wetu wa local Discos ulikuwa ni wa nje tu, hivyo bendi hii ikaishia kufa kifo cha mende,
4. Lakini baadaye Shem Karenga, alijiunga na bendi mpya iliyoanzishwa na Msilwa (Twanga) na Martin (FM-Academia), yaani bendi ya MK.Group, pale New Africa Hotel, iliyowajumisha kina Kassongo Mpinda (Marquis), Mzee Mwema Mudjanga (Mzee Chekeeeencha-Marquis), Nkurlu Wabangoi (Marquis), Mbombo Wa Mbombo-Ka (Safari Sound) na wengineo wazawa, bendi hii ilivuma sana mwanzoni mwa 90s, mpaka waanzilishi wa bendi hii walipoamua kuachana na kuanzisha bendi zao za sasa, Shem alijaribu kupiga muziki wa solo kwenye mahotel makubwa, lakini hakufika mbali sana.
Since then sijamsikia tena mwanamuziki huyu, Karenga ambaye kwa kweli alikuwa ni mmoja wa mabingwa wa muziki nchini.