Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

akhwari1.gif
John Steven Akhwari akimaliza mbio za marathon katika olimpiki ya mwaka 1968 Mexico City, saa moja baada ya washiriki wote kumaliza mbio hizo.

John anakumbukwa dunia nzima kwa kauli yake hii
"My country did not send me 7000 miles away to start the race. They sent me 7000 miles to finish it."

Yes jamaa ni shujaa kwelikweli.
[media]http://www.youtube.com/watch?v=Hq3rOMnLGBk[/media]
 

...Humud ndiye anayetajwa sana sababu 'inasemekana' mafuzoni urusi aliapa ipo siku atalipiza kisasi cha kuuliwa baba yake.

...watu wanne waliingia pale kisiwandui. kuruhusiwa kwao kupita getini kuna maanisha walikuwa ni askari walokuwa wanatambulika, na wenye vyeo vikubwa tu jeshini wakati huo.

...Baada ya mauaji, mmoja wao aliuwawa, mmoja alikamatwa, na wawili walikimbia...

unajua 1.nani aliuwawa? 2.nani alikamatwa, 3. wawili waliokimbia kina nani? ...kwa sababu za kiusalama itabakia ni "siri-kali"

tuendelee na picha; ...Malcolm X na Abdulrahman Babu!


View attachment 2177
 
ABDULRAHAMAN BABU na NYERERE wote walikuwa wasocialist waliobobea,tofauti zao ilikuwa ni njia za kuufikia huo usocialist,whereas nyerere alitaka african socialism,ujamaa ambao centered around utu na ubinadam,whereas babu,alihisi ujamaa huu ungechelewesha maendeleo.yeye aliadvocate scientific socialism based on the advancement of factors of production,hapa palikuwa patamu moto uliwaka chinichini.masikini tanzania yetu,sijui vichwa kama hivi tutavipata wapi tena
 
Tumezungumza wanasiasa, wanasoka na baadhi ya wanamuziki na wanariadha, lakini hatujajikumbusha wanandondi wetu. Nawaomba wale vijana wa zamani watuletee picha za akina Titus Simba, Habib Kinyogoli, Emmanuel Mlundwa na Isaac Mabushi walotamba katika uwanja huo enzi hizo.

Kwa sasa nawakumbushia Shem Kalenga aliyekuwa gwiji wa muziki pale mtaa wa Lumumba akiwa na Tabora Jazz enzi hizo akitoa vitu kama Dada Asha No 1, 2, 3, 4; Alhamdulilah; Serafina; Mariamu na vinginevyo vingi vilvyohusu Wazee wa Kazi:

front%20photo.jpg
 
Filbert bayi alivunja rekodi ya dunia ya mita 1500 kwenye michezo ya jumuia ya madola huko Christchurch New Zealand mwaka 1974, baada ya kuwa amempiku Kipchoge Keino wa Kenya kwenye mashindano ya Afrika mwaka 1973,

1623297.jpg

Picha hii hapa ya bayi nimeinasa kwenye mtandao wala sijui ni ya lini na alikuwa akifanya nini.


3094414.jpg

Ila, Bayi alinivunja mbavu sana alipokuwa akiongea na BBC mwaka 1980 au 81 hivi alipoulizwa kuhusu mipango yake ya baadaye kwa vile umri ulikuwa unaanza kumpinga kuendela na riadha. Akakurupuka na kudai kuwa watu walikuwa wanamwonea wivu tu, hata hivyo yeye alishakuwa ni afisa wa jeshi la wananchi wakati huo kwa hiyo hakuwa na wasiwasi wowte
 
1. ABDULRAHAMAN BABU na NYERERE wote walikuwa wasocialist waliobobea,

2. tofauti zao ilikuwa ni njia za kuufikia huo usocialist,whereas nyerere alitaka african socialism,ujamaa ambao centered around utu na ubinadam,

3. whereas babu,alihisi ujamaa huu ungechelewesha maendeleo.yeye aliadvocate scientific socialism based on the advancement of factors of production,

4. hapa palikuwa patamu moto uliwaka chinichini.masikini tanzania yetu,sijui vichwa kama hivi tutavipata wapi tena

Mkuu Son Of Alaska,

Ahsante kwa hiii picha ya Baba na Malcom -X, na pia hii analysis yako ndogo lakini very powerful ya mawazo ya Mwalimu na Babu,

1. hivi ni kweli kwamba tofauti zao kuhusu ujamaa upi unaofaaa na usiofaa, zinaweza built arround tofauti za jadi kati ya Lenin na Mao, kwa sababu baada ya kuwasoma sana na kwa makini Mao na Lenin, ninaona kama hata tatizo la Babu na Mwalimu, linaanzia kutoka kwenye itikadi za then Urusi na China,

Where mawazo ya Mwalimu, in simple terms politically yalikuwa ni ya Mao kwamba model ya ujamaa kwanza sio lazima iwe moja kwa dunia nzima, na ni lazima iwe adjustable kulingana na mazingira na watu walengwa na pia ijali walengwa zaidi yaani wananchi kuliko vitu au mali,

Ambapo Warusi walikuwa total opposite na hiyo model, wao waliamini kwamba one socialism na one model kwa dunia nzima, na hakuna negotiations na walengwa on the implementation ya model, kwa sababu sauti ya umma haiko right siku zote na kwamba sometimes ni kiongozi tu anaweza ku-determine the good of the people kwa niaba ya the people at large,

2. Halafu ni kwa nini Babu, who was very convincing na ideas zake akiwa nje in enxile, aliporudi bongo infact yeye na Kambona, naona kama walishindwa not only ku-communicate their good old ideas kwetu wananchi, lakina walishindwa vibaya sana hata kutushawishi wananchi wengi kuwa walikuwa na a good case against Mwalimu's ideas as opposed na walipokuwa nje ya nchi ambapo walionekana ku-make more sense kila walipouwa wakiongea kuhusu siasa zetu za bongo?
 
Kwa sasa nawakumbushia Shem Kalenga aliyekuwa gwiji wa muziki pale mtaa wa Lumumba akiwa na Tabora Jazz enzi hizo akitoa vitu kama Dada Asha No 1, 2, 3, 4; Alhamdulilah; Serafina; Mariamu na vinginevyo vingi vilvyohusu Wazee wa Kazi:

Mkuu Kichuguu,

1. Heshima mbele tena, hapa naona Shem Karenga alikuwa very young na pia inakumbusha sana enzi zile za Tabora Jazz, yaani wana-Segua Segua, kwa kweli na wao walitamba sana na kuweka signature kubwa sana kimuziki nchini, na wao pia walikuwa wakisikika sana kwenye Radio Bukavu, na hata gwiji mmoja wa muziki kule Zaire, Kitonzengu Lokassa ya Mbongo ambaye originally, alianzia kwa Tabu Ley, alikuwa na heshima kubwa sana na Karenga mpaka akaamua kurudia kwa ku-modify wimbo wake wa Asha akiu-mix na ule mwingine Rosa, uliopigwa na Wema Abdallah, akiwa na Western Jazz,

2. Bendi hizi mbili yaani Western na Tabora, zilikuwa na uhusiano wa karibu sana enzi hizo, kwa sababu Wema Abdallah alitokea Tabora Jazz, kabla hajahamia Western Jazz, yaani Siku Kuu Street, hapa Kariakoo. Siku zote walikuwa na mahusiano ya karibu na hata kumpelekea Wema kupiga kibao kimoja akiwa na Western, cha "Huenda Tutarudiana" ambacho kilitamba sana in the 70s, chenye tafsiri ya kuwa huenda siku moja atarudiana na Tabora Jazz, ambayo siku zote alikiri kuikumbuka sana.

3. Tabora Jazz ni moja ya bendi ambayo baadye in the 80s, ilikuja athirika na mabadiliko ya kiuchumi nchini, ambapo matatizo ya uchumi yalitupelekea enzi hizo wa-Tanzania wengi kuamini kuwa vitu vizuri vilikuwa ni vya kutoka nje tu ya nchi yetu lakini sio vyetu wenyewe, kasumba hii ndio iliyotuplekea wananchi wengi kuwathamini sana mabaharia waliorudi kutoka nje, au mwananchi yoyote aliyefanikiwa kuishii nje, tulifkia mahali muziki wetu wa local Discos ulikuwa ni wa nje tu, hivyo bendi hii ikaishia kufa kifo cha mende,

4. Lakini baadaye Shem Karenga, alijiunga na bendi mpya iliyoanzishwa na Msilwa (Twanga) na Martin (FM-Academia), yaani bendi ya MK.Group, pale New Africa Hotel, iliyowajumisha kina Kassongo Mpinda (Marquis), Mzee Mwema Mudjanga (Mzee Chekeeeencha-Marquis), Nkurlu Wabangoi (Marquis), Mbombo Wa Mbombo-Ka (Safari Sound), Mafumu Bilali (Vijana Jazz) na wengineo wazawa, bendi hii ilivuma sana mwanzoni mwa 90s, mpaka waanzilishi wa bendi hii walipoamua kuachana na kuanzisha bendi zao za sasa, Shem alijaribu kupiga muziki wa solo kwenye mahotel makubwa, lakini hakufika mbali sana.

Since then sijamsikia tena mwanamuziki huyu, Karenga ambaye kwa kweli alikuwa ni mmoja wa mabingwa wa muziki nchini.
 
FMES,
Inasikitisha sana kuwa watu kama Babu ambao nje ya Tanzania walionekana kama lulu, nchini kwao walitazamwa kama wahaini. Sina hakika kama hii ni matokeo ya ujinga wa watanzania au la, lakini jana tu nimeshuhudia waandamanaji wa CCM waliokuwa wakiandamana kupongeza hotuba ya Kikwete wakizomewa na baadhi ya wananchi kuomba atokee dereva kichaa awaswage kwa gari lake. Nafikiri taratibu tunaanza kubadilika na matumaini yangu ni kuwa ipo siku historia itampa Babu nafasi anayostahili.
 
Filbert bayi alivunja rekodi ya dunia ya mita 1500 kwenye michezo ya jumuia ya madola huko Christchurch New Zealand mwaka 1974, baada ya kuwa amempiku Kipchoge Keino wa Kenya kwenye mashindano ya Afrika mwaka 1973,

Ila, Bayi alinivunja mbavu sana alipokuwa akiongea na BBC mwaka 1980 au 81 hivi alipoulizwa kuhusu mipango yake ya baadaye kwa vile umri ulikuwa unaanza kumpinga kuendela na riadha. Akakurupuka na kudai kuwa watu walikuwa wanamwonea wivu tu, hata hivyo yeye alishakuwa ni afisa wa jeshi la wananchi wakati huo kwa hiyo hakuwa na wasiwasi wowte

1. Filbert Bay, alikuwa ni mwanajeshi wa kikosi cha Anga kilichopo ndani ya Airpot yetu ya zamani hapa Dar, akiwa na cheo cha Liutenant alivunja record ya dunia kule New Zealand, na behind kuvunja record huko aliweza kujikusanyia hela nyingi sana, enzi hizo.

2. Bay alikuwa amemuoa mcheza netball hatari sana enzi hizo, Anna Bay, ambaye pia alikuwa ni mfanya biashara maarufu sana mjini Dar, kwa hiyo hela nyingi za Bay kutoka kwenye riadha, huyu mama aliweza kuzi-invest kwenye biashara mbali mbali, kwa hiyo Bay aliweza kuwa mmoja wa wanamichezo wachache sana kama sio peke yake tu nchini, aliyeweza kuishi maisha ya juu sana na kwa muda mrefu sana, sina uhakika leo yukoje na kama bado yupo na yule mama, lakini nimemuonam mara nyingi hivi karibuni akionekana bado kuwa na maisha mazuri, pia anamiliki shule moja ya sekondari ya kulipia kule Sinza, ambayo ni moja ya shule maarufu sana jijini.

Na siku zote ninamuheshimu sana kwa sababu huyu Bay, alikua a very big heart kila aliporudi toka nje, alikuwa na tabia ya kugawia wanamichezo zawadi za vifaa vya michezo, na hasa marafiki zake, aliweza kuwasaidia sana some of our local athletes na hasa kina Juma Ikangaa na Nyambui

Na niaamini kuwa bado mpaka leo yeye ni kiongozi wa juu sana nchini katika mchezo wa riadha. Again, ahsante mkuu Kichuguu kwa hii picha ya another hero wa taifa.
 
1.
Inasikitisha sana kuwa watu kama Babu ambao nje ya Tanzania walionekana kama lulu, nchini kwao walitazamwa kama wahaini. Sina hakika kama hii ni matokeo ya ujinga wa watanzania au la,

Mkuu ni kweli kabisa, Babu ninaamini kuwa alikuwa ni kichwa sana binafsi ninakumbuka siku moja nilikuwa nimekwenda Ukonga Magereza, kumuona mshikaji wangu mmoja, aliyekuwa deported kutoka nje alikuwa ameshikiliwa kule, kama kawa nilikuwa na washikaji pale askari wa magereza wapiga muziki, kwa hiyo unajua bongo mshikaji askari akanipeleka mpaka ndani kabisa ambako hakuruhusiwi raia kufika, na nikapiga tour ya gereza zima kwa ndani, na sehemu wanazolala wakulu, damn it!

Curiously, nikamuomba jamaa anionyeshe mahali alipokuwa akiishi Babu na wenzake, wakati huo ilikuwa ni kama wiki moja tu toka aachiwe duh mkuu niliona vitabu vya mkulu Babu vinasubiri kuja kuchukuliwa yaani ni vingi haijwahi kutokea, toka siku ile nikaamua kumfuatilia sana kujua who was he haswa?

Kwa kweli I was impressed na record yake academically, lakini sikuwa na uhakika kama ni kweli he was involved na so many local political conflicts, it seems kuwa mikono yake ilikuwa all over, kuanzia kwenye ile mutiny ya the 60s, mpaka kifo cha Karume, lakini swali moja mpaka leo bado linanisumbua sana kwamba kama kweli alihusika na hizi conflicts ambazo kama ni kweli alivunja sheria, Why he was never punished legally?

ninaweza kuwatetea wa-Tanzania kwamba tulikuwa innocent people na hizi politics, mabazo zilikuwa too much sio kwetu tu hata kwa viongozi wetu wa juu kama sikosei, lakini something was not right na sijui what it is!



2.
lakini jana tu nimeshuhudia waandamanaji wa CCM waliokuwa wakiandamana kupongeza hotuba ya Kikwete wakizomewa na baadhi ya wananchi

Wa-Tanzania tumekuwa watumwa wa akili ya siasa kwa muda mrefu sana, miaka 45 ni mingi sana katika maisha kwa bin-adam kuwa katika mfumo wa siasa na mawazo ambayo hana the will ya kuamua anachotaka, bali kuamuliwa na wengine,

Na ukweli ni kwamba hata viongozi wetu wa sasa wa juu wanalijua sana hili, wanachofanya sasa ni wana-count tu the time, kwamba lini wananchi tutaamuka kabisaa, so far wanajua kuwa bado tumelala na itachukua muda kidogo, lakini pole pole tunaanza kuamka, ingawa bado sana,

Hotuba ya juzi ya Kikwete, iliyonikatisha tamaa sana, ukiiangalia kwa makini the side ya political saikolojia yake na impact yake kwetu wananchi, utagundua kuwa hawa viongozi wetu wana-benki kwenye ujinga wetu wananchi.
 
Wakuu mi nimeonelea ni vema kuwa na suala la kama kitabu/kijarida kikiwa na picha pamoja na maelezo mengine yoote kuhusiana na picha hizi kama hatujawa nacho bado. Ngoja niangalie kama itawezekana tutengeneze kitabu/kijarida kikiwa na mambo yoote haya. Nitarudi na jibu kama wanajamvi mtakubaliana na hili. Nawakilisha.....
Kama nilivyoahidi kuhusiana na comment yangu hapo juu; well nimecheki na nimeona inawezekana lakini sharti kwa kupata ushirikiano wa dhati kutoka kwenu, isije ikatokea yaleeee ya t-shirts. Mwenye maoni.....nasikiliza.
 
Mkuu Kichuguu,

1. Heshima mbele tena, hapa naona Shem Karenga alikuwa very young na pia inakumbusha sana enzi zile za Tabora Jazz, yaani wana-Segua Segua, kwa kweli na wao walitamba sana na kuweka signature kubwa sana kimuziki nchini, na wao pia walikuwa wakisikika sana kwenye Radio Bukavu, na hata gwiji mmoja wa muziki kule Zaire, Kitonzengu Lokassa ya Mbongo ambaye originally, alianzia kwa Tabu Ley, alikuwa na heshima kubwa sana na Karenga mpaka akaamua kurudia kwa ku-modify wimbo wake wa Asha akiu-mix na ule mwingine Rosa, uliopigwa na Wema Abdallah, akiwa na Western Jazz,

2. Bendi hizi mbili yaani Western na Tabora, zilikuwa na uhusiano wa karibu sana enzi hizo, kwa sababu Wema Abdallah alitokea Tabora Jazz, kabla hajahamia Western Jazz, yaani Siku Kuu Street, hapa Kariakoo. Siku zote walikuwa na mahusiano ya karibu na hata kumpelekea Wema kupiga kibao kimoja akiwa na Western, cha "Huenda Tutarudiana" ambacho kilitamba sana in the 70s, chenye tafsiri ya kuwa huenda siku moja atarudiana na Tabora Jazz, ambayo siku zote alikiri kuikumbuka sana.
3. Tabora Jazz ni moja ya bendi ambayo baadye in the 80s, ilikuja athirika na mabadiliko ya kiuchumi nchini, ambapo matatizo ya uchumi yalitupelekea enzi hizo wa-Tanzania wengi kuamini kuwa vitu vizuri vilikuwa ni vya kutoka nje tu ya nchi yetu lakini sio vyetu wenyewe, kasumba hii ndio iliyotuplekea wananchi wengi kuwathamini sana mabaharia waliorudi kutoka nje, au mwananchi yoyote aliyefanikiwa kuishii nje, tulifkia mahali muziki wetu wa local Discos ulikuwa ni wa nje tu, hivyo bendi hii ikaishia kufa kifo cha mende,

4. Lakini baadaye Shem Karenga, alijiunga na bendi mpya iliyoanzishwa na Msilwa (Twanga) na Martin (FM-Academia), yaani bendi ya MK.Group, pale New Africa Hotel, iliyowajumisha kina Kassongo Mpinda (Marquis), Mzee Mwema Mudjanga (Mzee Chekeeeencha-Marquis), Nkurlu Wabangoi (Marquis), Mbombo Wa Mbombo-Ka (Safari Sound) na wengineo wazawa, bendi hii ilivuma sana mwanzoni mwa 90s, mpaka waanzilishi wa bendi hii walipoamua kuachana na kuanzisha bendi zao za sasa, Shem alijaribu kupiga muziki wa solo kwenye mahotel makubwa, lakini hakufika mbali sana.

Since then sijamsikia tena mwanamuziki huyu, Karenga ambaye kwa kweli alikuwa ni mmoja wa mabingwa wa muziki nchini.




'Ewe mpenzi wangu pokea hizi salamu ee,
Huenda tukarudiana hapo baadaye usife moyo,

Kwa kuwa tabia zetu sasa hazilingani ee,
Huenda tukarudiana hapo baadaye usife moyo,

Mimi najua hata mwisho wa mapenzi eee,
Huenda tukarudiana hapo baadaye usife moyo,

Mwisho wa penzi kutenganishwa na kifo mama ee,
Huenda tukarudiana hapo baadaye usife moyoo,




Chorus:

Ikiwa tupo hai ee,
Huenda yakarudi tena aa,
Mapenzi yetu eee, uusife moyo,

EEwe sikia ikiwa tupo hai ee,
Huenda yakarudi tena aa,
Mapenzi yetu eee, uusife moyo x2


Mheshimiwa, umenikumbusha mbali sana muziki ulipokuwa muziki kweli!!!
 
Karume%20Funeral%20.jpg

Ulinzi wakati wa maziko ya Karume ulikuwa tight... kama inavyoonekana hapo juu..
 
Duh,

Mada hii baaabu kubwa sanaaaa yaani Jamii Forums inabidi kujiweka sawa na kuanzisha kumbukumbu hizi kisha kuzikabidhi Makumbusho!...FMES mkuu wangu hongera sana kwa kutoa hoja hiii...
Ni muhimu sana kwa sababu vijana wengi hawafahamu kabisa tulitoka wapi!...
Hakika miaka ya 70 na 80 Tanzania pamoja na mapungufu yetu kiuchumi lakini jamani tulikuwa - The Giant of Africa....
Kinachinishangaza zaidi ni pale kila shirika la serikali mbali na Ujamaa wetu tulikuwa na bendi, timu za mpira wa miguu na netball, jeshi letu lilikuwa imara ktk kila fani, Ulinzi (National security) yaani hapo ndio hata usigusie, riadha chini ya Sarakikya ilikuwa ktk kiwango cha juu sana..
Ni wapi tulikwenda mrama...
 
Mada hii baaabu kubwa sanaaaa yaani Jamii Forums inabidi kujiweka sawa na kuanzisha kumbukumbu hizi kisha kuzikabidhi Makumbusho!...FMES mkuu wangu hongera sana kwa kutoa hoja hiii...
Ni muhimu sana kwa sababu vijana wengi hawafahamu kabisa tulitoka wapi!...

Mkuu Bob,

Heshima ikurudie, unajua ile hotuba ya Rais bungeni, mpaka leo bado sija-recover bro, kwa sababu kwa maoni yangu that was the biggest political joke of our time, kama sio of the century,

After all the hard work ya kujaribu kuisaidia serikali na uchunguzi mbali mbali kuhusiana na ufisadi wa viongozi wake, kamati zote zilizochaguliwa kuchunguza ufisadi, maneno yote tena mpaka yake mwenyewe kuwa anawajua wauza unga na wala na watoa rushwa nchini, with all the build up ya ile hotuba na the hype, yaani rais anakuja bungeni na kutufanya wananchi kuwa ni wajinga wa juzi, ila yeye na mafisadi ndio wenye akili sana,

Mpaka leo mkuu bado sijajielewa, ndio maana nikaamua kutafuta something powerful, cha kuwahakikishia viongozi wetu kuwa kwanza tunaijua historia ya taifa letu, na kwamba hili taifa kuna wakati lilikuwa on the right track kimaendeleo, lilikuwa na viongozi safi wasio wabinafsi na mafisadi kama walivyo sasa, picha zinajisema zenyewe viongozi walivyotulia, sio siku hizi kwenye picha tu unawajua kuwa hawa viongozi ni wasanii, taifa lilipokuwa limetulia wananchi pia tulikuwa tunachacharika, kuanzia michezo mpaka kwenye siasa,

Tatizo la kisiasa mara moja rais hakukawia kuwaita wazee wa Dar, na kulihutubia taifa, nafikiri unakumbuka zile enzi za wahujumu, siku ile Diamond Jubilee, Mwalimu aliposhambuliwa na kina Eda Sanga kuwa anaifanya kazi ya Sokoine kuwa ngumu kwa sababu anatetea mafisadi flani viongozi, na Mwalimu ilibidi asimame wazi na kusema anachofanya na asichofanya kuhusu ile operation ya wahujumu uchumi, na akasema wazi kuwa sio kila kiongozi anayesemwa kuwa ni mwizi basi ni mwizi tu!

Sikuwahi kuwa mpenzi mkubwa wa siasa za Mwalimu, lakini ni recently tu ndio nimegundua kuwa no matter the ishu, kubwa au ndogo siku zote under Mwalimu, kulikuwa na response kutoka either kwake direct, au kutoka kwa serikali with a political act, ingawa those acts bado ni open for debates on its effectiveness kwa taifa, lakini we have to give it to Mwalimu kwamba he cared ndio maana siku zote kulikuwa quick response,

Kwa mfano, kwenye:-

1. mutiny the next thing ni kwamba kuna wanajeshi walifungwa, kuna wanajeshi walifukuzwa kazi, kuna waliohamishwa uraiani.

2. Kwenye kuhamisha wananchi vijijini, Kawawa paid for with a public rebuke kutoka kwa Mwalimu, na hata kushuhwa cheo na kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalum, kutoka kuwa the second powerful man in our nation.

3. Kwenye majaribio ya mapinduzi, kina Mwakalindile, Sarakikya, na Mayunga wakahamishiwa nje ya nchi kuwa mabalozi, kina Mahiga na Kitine wakastaafishwa.

4. Waziri wa sheria na katiba alipotuhumiwa kuwa mla rushwa, Mwalimu alimfikuza kazi na kutangaza rasmi kwa taifa, tena mara moja, I mean we can go on and on na hii mifano,

Sasa what happened today? Hawa viongozi huu ujeuri wanautoa wapi? Kina Chenge na Lowassa, wao ni nani hasa? Rais hawezi kusema kuwa hana ukweli, kwa sababu hata wazungu wa UK wamewaita kuhusiana na kuhusika kwao na ufisadi, inasadikiwa kuwa wazungu walikuwa tayari kuwafungulia mashitaka, ndio maana Kibello akatolewa pale mapema, kwa sababu under him pale hawa wangetinga kweli kwenye sheria huko majuuu, akapelekwa balozi wa sasa a compromise wa rais, what a shame? Halafu rais anatoka pale anapanda ndege kwenda US kama vile nothing happened!

Halafu eti kuna wananchi wanaenda kuandamana kuunga mkono hotuba zake za maji ya sharubati! Ndio maana nimeona for now kula picha tu hapa na histroria, heshima kwa wachangiaji wote hapa na bado tunaendelea kula historia nzito hapa, kwa mara ya kwanza nimekuja kumjua vizuri Karume, kutokana na hii thread.

Ahsante Wakuu.
 
Field Marshal Es,
Basi baba basi huna haja ya kuongezea machungu imetosha utatuliza wengi!.. mimi nishakata tamaa kusema kweli ndio maana nimeipenda mada hii sana kama mapozeo.. na muda wote nimekuwa msomaji pamoja na kwamba nilikuwa na mengi ya kuchangia...hakuna raha duniani kama kusikiliza watu wakichambua kitu ambacho kinakugusa sana..
Majuzi tu nilikuwa Mall nikawasikia Wakenya kama sio Waganda wakizungumza kiswahili basi mkuu niliona raha za ajabu sana, kwanza ni lugha yangu halafu sisi tunashindwa kujivunia kabisa, ilibidi nimshukuru Mungu..
 
Hiki ndicho kikosi kamili cha Mzee Makassy (mzee Shughuli) mwaka 1981; amevaaa boogaloo.

attachment.php

Juu kabisa kushoto kwa Makassy ni Assosa (mtoto mzuri wa enzi hizo) na kulia kwa Makassy ni Mbomboka.
 

Attachments

  • makassy.jpg
    makassy.jpg
    30.3 KB · Views: 785
FMES,
We acha tu. Hata hatujui tuko wapi na tunakwenda wapi. Maneno ya Mkandara ni mazito.
 
Nyerere hakupenda nchi yetu itumike kama soko la bidhaa za nchi nyingine. Hii ni sababu mojawapo iliyofanya viongozi wa Kenya wamchukie Nyerere kwa vile Kenya ilishakuwa na viwanda vingi na ilikuwa inaitumia Tanzania kama soko lake. Kutokana na kutopenda hali hiyo ya kutumiwa kama soko la nje, Nyerere alisisitiza ujenzi wa viwanda kwa kasi sana. Karibu kila mkoa ulipangiwa kiwanda cha aina fulani angalau kimoja ingawa mkoa wa Morogoro na Dar-es Salaama walijipatia viwanda vingi zaidi.

Tangu Nyerere aondoke madarakani, sijasikia tena msisitizo wa nchi kujijenga kiviwanda. Ninachoona ni nchi kuuza viwanda vyetu na kujifungua kuwa soko la nje; hatuna cha kwetu tena. Nchi tunazosikia zinakuja juu kiuchumi, kama vile China na India, zinafanya hivyo siyo kwa sababu wao ni masoko ya nje, bali ni kwa sababau wanazalisha bidhaa wanazouza nje kutoka viwandani mwao. Kwenye picha hii hapa Nyerere anaonekana akiweka jiwe la msingi wakati wa ujenzi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki.

attachment.php
 

Attachments

  • nyerere-urafiki.jpg
    nyerere-urafiki.jpg
    28.8 KB · Views: 455
Back
Top Bottom