Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Wakulu mie natafuta proceedings za ile kesi ya uhaini hasa zile cross examinations alizokuwa anazimwaga Wakili Murtaza Lakha. Nilikuwa mdogo zama zile lakini nakumbuka alivyokuwa anawahenyesha mashahidi kwa maswali ya provocations.
Halafu kama kuna mtu anajua the so called shahidi X, Y and the like walikuwa akina nani? kuna mtu aliniambia shahidi X alikuwa ni Mzee Apson mkurugenzi mstaafu wa usalama not sure abt that though
Mmojawapo kati ya shahidi X na Y alikuwa jamaa mmoja wa huko Bunda; namfahamu sana ametokea kijiji kimoja na Wasira. Alikuwa ni shushushu mkali sana. Kusema ukweli ile timu ya security ya Nyerere ilikuwa kali sana, na jamaa walikuwa tayari kubeba dhoruba yoyote katika kutafuta habari za kipelelezo. Kwa mfano, katika upepelezi wa ile kesi, huyu jamaa wa Bunda naye aliwekwa ndani pamoja na watuhumiwa kwa takribani miezi minne hivi akiwa anawapeleleza. Alipotoka kule jela akaja na burungutu la fedha na kuzamia nje kidogo kabla kesi haijaanza. Sijui siku hizi yuko wapi tena, ila najua kuwa mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzni mwa miaka ya tisini alikuwa asumbuliwa na kupooza upande mmoja wa mwili; aliepelekwa Ulaya kwa matibabu ila sijuia hatima yake iliishia wapi.



