Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

1. Wakati Tanzania inatambua Biafra nilikuwa Agha Khan Secondary School, ambayo baadaye mliita Tambaza. Sisi wanafunzi wa Kiafrika wote tuliounga mkono kujitenga kwa Biafra, lakini Wahindi, wakikumbuka kutenganishwa kwa India na Pakistan, walipinga kwa dhati.

2. Ojukwu bado yupo. Kilichosababisha Biafra kujitenga, ni pogrom waliyofanyiwa Waibo ambao ndio walikuwa kama Mayahudi wa Nigeria, hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1966.

3. Alichofanya Mwalimu, alifunga safari kukutana na Jemadari Gowon, akamsihi wajadiliane na Ojwuku, watafute muafaka kwa mauaji yaliyokuwa yanaendelea.

4. Gowon akakataa akisema hawezi kujadiliana na "junior officer." Unajua tena arrogance ya Sundhurst graduates. Mwalimu akaenda Ivory Coast kukutana na Houphoet Boigny ikaamuliwa kuwa Biafra itambuliwe kama njia ya kum "pressure" Gowon akubali kujadiliana na Ojwuku.

5. Zambia na Haiti nazo zikaitambua Biafra. Lakini unajua ndugu yangu mambo haya hayawezi kumalizika bila mwingilio wa wakubwa. Uingereza ilishajua kuwa kuna mafuta huko Biafra na haikutaka kuiachia Ufaransa inufaike na mafuta hayo kwa hiyo walimsaidia Gowon juu chini kuwamaliza Wabiafra. Ufaransa ilikuwa upande wa Biafra.

6. Marekani was neutral. Actually a lot of fundraising by Biafran students was done in the US.

7. Siku ambayo Tanzania imeitambua Biafra ilikuwa easter. Mwalimu alialikwa nyumbani kwa Butiku and I happened to be there, pamoja na akina Mgaya, na Mzee Munanka (rip) Butiku alikuwa na telegrams nyingi kutoka sehemu mbalimbali zikimpongeza Mwalimu kwa msimamo huo lakini Mwalimu alikuwa na swali moja tu: "will Africa understand?" Alilirudia hilo swali mara kadhaa.

8. Hii ya Delta nadhani ni uchungu wa kuona kuwa federal government inatajirika na mafuta ya eneo hilo wakati ambapo wakazi wa eneo wamefunikwa na ufukara uliokithiri. They want a share of the pie.

Mkuu Jasusi,

1. Darasa zito sana hili, ninaikumbuka Biafra na nyimbo tulizoimba sana shuleni za za kumsifu "Koloneli Ojukwu", lakini nilikuwa mdogo sana.

2. Nikiwa NY, niliwahi kuongea na M-Nigeria mmoja ambaye ninamua-admire sana, aliwahi kuwa balozi wao kule UN na sasa ni mkuu ndani ya UN, anaitwa Gen. Gambari, ambaye ni rafiki wa karibu sana na Gen. Gowon na Ojukwu, serikali ya Nigeria inamuogopa sana huyu mkulu na hata hutumia hela kumfanya asirudi Nigeria, kwa kweli baadhi ya aliyoniambia kuhusu Biafra ni sawa kabisa na unayosema,

Lakini nina wasi wasi kuwa kwenye ku-support Biafra, we were wrong na kama sikosei kuna wakati Mwalimu, akiwa hai aliwahi ku-apologize for, I mean leo Mwanza wanataka kujitenga na Tanzania, halafu ije nchi nyingine iwa-support, that was very wrong nafikri hata standing yetu katika international world Affairs, ninaamini tulichukua a bite kidogo, halafu pia ilitu-cost sana economically kwa sababu japo nilikuwa mdogo sana lakini ninakumbuka ile michango ya kusaidia Biafra,

Lakini ashante sana kwa kipande zaid cha historia.

(a) Nadhani huyu ni Professor Ibrahim Gambari; alikuwa Ahmadu Bello University kabla hajateuliwa na General Mohammed Buhari kuwa waziri wa mambo ya nje kufuatia mapinduzi ya mwaka 1983. Sidhani kama aliwahi kuwa mwanajeshi.

(b) Ni kweli hii vita ya Biafra iliiumiza sana Tanzania katika uhusiano wa kimataifa. Nyerere aliwahi kukiri wazi kabisa kuwa ni moja ya maamuzi ambayo anayajutia sana. Alimwambia hayo Peter Enahoro aliyekuwa editor wa Gazeti la Africa Now la mwaka 1983 muda mfupi baada ya mapinduzi yaliyofanywa na General Buhari. Alidai kuwa ulikuwa uamuzi mgumu sana kwake kuufanya kwa sababu ni kama alikuwa anaunga mkono Balkanization of Africa wakati lengo lao katika OAU ilikuwa ni kuunganisha nchi za Afrika, siyo kuzigawanya vipande vidogo vidogo. Sababu iliyomtuma kufanya hivyo, kulingana na maelezo hayo, ni kwamba aliona kama serikali ya Gowon ilikuwa inawachoche Biafra kujitenga kwa vile ilikuwa ianedesha mauaji ya raia wale kama Genocide. Kwa hiyo njia pekee ikawa ni kwa hao raia kujitafuatia namna ya kujilinda wenyewe kwa kuunda serikali yao, yaani wajitenge na Nigeria.

(c) Jina la Biafra lilivuma sana Tanzania wakati huo kwani najua kuwa hadi leo pale Musoma kuna kitongoji kinaitwa Biafra (Jasusi unapafahamu Biafra?). Vile vile pale Kibara kulikuwa na Baa inaitwa Biafra Bar (Mkandara upo hapo?), Mwanza pia kulikuwa na mtaa unaitwa Biafra Street. Nadhani sehemu nyingi za Tanzania zina kitu cha kukumbukia vita hiyo ya Biafra. Ila niliwahi kuongea na Mzee mmoja aliyewahi kushika nyadhifa kadhaa kwenye serikali ya Nigeria ambaye ni wa asili ya Biafra. Alikuwa anamsifu na kumpenda sana Nyerere kwa kuunga mkono vita ile. Mzee yule alionekana kulia machozi ya wazi kabisa, zaidi yetu watanzania wenyewe, kwenye ibada ya kumkumbuka Nyerere tuliyoandaa mwaka 1999 mara tu baada ya Nyerere kufariki.
 
BIAFRA,has come back to haunt us,zanzibar wants to do away with the union,is this not, the chickens coming back home to roost? history has always had a way of repeating itself,the fact of the matter is nyerere,as a staunch advocate of african unity,had made a serious political error in recognising biafra.in this history has allready vindicated him
 
Quote: Kichuguu

Quote: Weeekpedia

Gambari attended King's College, Lagos. At the London School of Economics he received a bachelor's degree in political science. From 1970 to 1974, he studied at Columbia University, New York, where he obtained both his M.A. degree and his Ph.D degree in political science/international relations.

[edit] Academic career

Gambari began his teaching career in 1969 at City University of New York before working at University of Albany. Later, he taught at Ahmadu Bello University, in Zaria, Kaduna State, the second largest university in Africa. From 1986-1989,

he was Visiting Professor at three universities in Washington, D.C.: Johns Hopkins School of Advanced International Studies, Georgetown University and Howard University. He has also been a Research Fellow at the Brookings Institution also in Washington D.C. and a Resident Scholar at the Bellagio Study and Conference Center,

the Rockefeller Foundation-run center in Italy. He was accorded, honoris causa, the title of Doctor of Humane Letters (D.Hum.Litt.) from the University of Bridgeport. He is a member of the Johns Hopkins University's Society of Scholars. He was decorated with the title of Commander of the Federal Republic (CFR) by the Government of Nigeria.

Mkuu ahsante kwa masahihisho, lakini nitakapomuona tena nitamuuliza kama aliwahi kuwa a soldier au hapana, maana ninajua kuwa siku zote wanam-refer kama General, nilimfahamu baada ya kukutana naye nyumbani kwa Mzee Masha, ambaye wakati huo alikuwa his spoke person, Gambari akiwa na nafasi kubwa sana UN, kama aliwahi kuwa soldier au hapana sina uhakika,

Lakini nilipomuuuliza maswali kuhusu Gowon na Ojukwu, alisema anawajua wote wawili as his personal friends, pia niliwahi kukutana na Binaisa pale kwa mzee Masha, naye akaniambia kua hakuwa rais wa Uganda ila alikuwa RC tu, siku hizi ninaamini kuwa ana-practice Law somewhere in Brooklyn.
 
BIAFRA,has come back to haunt us,zanzibar wants to do away with the union,is this not, the chickens coming back home to roost? history has always had a way of repeating itself,the fact of the matter is nyerere,as a staunch advocate of african unity,had made a serious political error in recognising biafra.in this history has allready vindicated him

Very strong point mkuu, yaani sasa atokee nchi au mtu wa kuwa-support wasiotaka muungano sijui tutasema nini?

Ndio maana sasa US, hawana ujanja na Georgia maana Russia, wanasema kuwa iwapo US imekwenda Middle East na kuwapiga Wa-Iraq, kwa nini na wao wasiingie jirani tu hapo Georgia?
 
Quote: Weeekpedia

Gambari attended King's College, Lagos. At the London School of Economics he received a bachelor's degree in political science. From 1970 to 1974, he studied at Columbia University, New York, where he obtained both his M.A. degree and his Ph.D degree in political science/international relations.

Mkuu ahsante kwa masahihisho, lakini nitakapomuona tena nitamuuliza kama aliwahi kuwa a soldier au hapana, maana ninajua kuwa siku zote wanam-refer kama General, nilimfahamu baada ya kukutana naye nyumbani kwa Mzee Masha, ambaye wakati huo alikuwa his spoke person, Gambari akiwa na nafasi kubwa sana UN, kama aliwahi kuwa soldier au hapana sina uhakika,

Lakini nilipomuuuliza maswali kuhusu Gowon na Ojukwu, alisema anawajua wote wawili as his personal friends, pia niliwahi kukutana na Binaisa pale kwa mzee Masha, naye akaniambia kua hakuwa rais wa Uganda ila alikuwa RC tu, siku hizi ninaamini kuwa ana-practice Law somewhere in Brooklyn.

Sikujua kuwa ana cheo cha kamanda wa jeshi, ila nilifahamu habari zake tangu alipoteuliwa na wale wanajeshi kuwa waziri wa Mambo ye nje huku akitokea moja kwa moja kutoka kwenye chaki; hakurudi tena ubaoni kuanzia wakati huo.

Yes, ninajua kuwa Godfrey Binaisa ana kampuni yake ya sheria hapo New York; sijui yeye ndiye aliemrithi Prof Lule au vipi. Je, ana-practice law ipi?
 
(a) Nadhani huyu ni Professor Ibrahim Gambari; alikuwa Ahmadu Bello University kabla hajateuliwa na General Mohammed Buhari kuwa waziri wa mambo ya nje kufuatia mapinduzi ya mwaka 1983. Sidhani kama aliwahi kuwa mwanajeshi.

(b) Ni kweli hii vita ya Biafra iliiumiza sana Tanzania katika uhusiano wa kimataifa. Nyerere aliwahi kukiri wazi kabisa kuwa ni moja ya maamuzi ambayo anayajutia sana. Alimwambia hayo Peter Enahoro aliyekuwa editor wa Gazeti la Africa Now la mwaka 1983 muda mfupi baada ya mapinduzi yaliyofanywa na General Buhari. Alidai kuwa ulikuwa uamuzi mgumu sana kwake kuufanya kwa sababu ni kama alikuwa anaunga mkono Balkanization of Africa wakati lengo lao katika OAU ilikuwa ni kuunganisha nchi za Afrika, siyo kuzigawanya vipande vidogo vidogo. Sababu iliyomtuma kufanya hivyo, kulingana na maelezo hayo, ni kwamba aliona kama serikali ya Gowon ilikuwa inawachoche Biafra kujitenga kwa vile ilikuwa ianedesha mauaji ya raia wale kama Genocide. Kwa hiyo njia pekee ikawa ni kwa hao raia kujitafuatia namna ya kujilinda wenyewe kwa kuunda serikali yao, yaani wajitenge na Nigeria.

(c) Jina la Biafra lilivuma sana Tanzania wakati huo kwani najua kuwa hadi leo pale Musoma kuna kitongoji kinaitwa Biafra (Jasusi unapafahamu Biafra?). Vile vile pale Kibara kulikuwa na Baa inaitwa Biafra Bar (Mkandara upo hapo?), Mwanza pia kulikuwa na mtaa unaitwa Biafra Street. Nadhani sehemu nyingi za Tanzania zina kitu cha kukumbukia vita hiyo ya Biafra. Ila niliwahi kuongea na Mzee mmoja aliyewahi kushika nyadhifa kadhaa kwenye serikali ya Nigeria ambaye ni wa asili ya Biafra. Alikuwa anamsifu na kumpenda sana Nyerere kwa kuunga mkono vita ile. Mzee yule alionekana kulia machozi ya wazi kabisa, zaidi yetu watanzania wenyewe, kwenye ibada ya kumkumbuka Nyerere tuliyoandaa mwaka 1999 mara tu baada ya Nyerere kufariki.

Swali: Niliwahi kuambiwa kuwa General Mayunga aliwahi kuongoza kikosi cha Tanzania kusaidia upande wa Ojukwu wakati wa vita ile. Je ni kweli kuwa Nyerere alipeleka jeshi letu kwenda kumsaidia Ojukwu? Je kama ni kweli, kuna anayejua ni wangapi waliouwawa?

Picha zimeishia wapi?
 
1.
Sikujua kuwa ana cheo cha kamanda wa jeshi, ila nilifahamu habari zake tangu alipoteuliwa na wale wanajeshi kuwa waziri wa Mambo ye nje huku akitokea moja kwa moja kutoka kwenye chaki; hakurudi tena ubaoni kuanzia wakati huo.

Huyu mkuu habari yake ni ya kutatanisha sana, kwa sababu hata pale kwenye uablozi wa Nigeria, yaani kwenye jengo lao la Nigeria Federal mitaa ya 37Th St. na 39Th St. jamaa ana power sana kwamba ana mpaka parking zake za magari yake mle ndani, na nasikia mpaka leo huletewa hela nyingi sana na serikali ili asirudi kwao, hata ukimuona uso kwa uso unaona tu kuwa mjanja mjanja tu! hata wa-Nigeria wenyewe humuogopa sana, na siku ya maombolezo ya Mwalimu, alikuwepo sana na akaongea kwa uchungu sana.

2.
Yes, ninajua kuwa Godfrey Binaisa ana kampuni yake ya sheria hapo New York; sijui yeye ndiye aliemrithi Prof Lule au vipi. Je, ana-practice law ipi?

Ninaamini ana-practice Comercial Law, kule Brooklyn unajua huko ma-Brooklyn ni noma tupu.
 
Dar-es-salaam US Embassy bombing, 7th Aug 1998 10:44:46 local time
attachment.php
 
Attachments

  • old-US Embassy.jpg
    old-US Embassy.jpg
    66.8 KB · Views: 776
View attachment 2241
MAY 3, 1963: Tanganyika's Ambassador to the Federal Republic of Germany, H.E. Mr Andrew K. Tibandebage, presents his credentials to the German President, Dr Heinrich Lubke in Bonn.

...Mmoja wa mabalozi wetu wa mwanzo mwanzo kabisa ughaibuni, sijui aliishia wapi huyu...

...pia Marehemu, Chief Lukumbuzya R.I.P
 
Wakati tukiendelea kujadili historia yetu ni vema kujadili wapi tulikosea kama anavyo uliza Mkandara

Baadhi ya makosa yetu ya wazi ni kuanzisha MASHIRIKA ya UMMA ku-AUDIT mashirika mengine ya umma. Shirika kama TAC, COASCO, na sasa CAG yamesaidia sana kuyaua mashirika mengine muhimu ya umma kama NBC, NMC, TBL, TOL, ATC, NUWA, RTCs, TRC,..., kwa kukagua na kutoa taarifa za UONGO na kuficha wizi wa wazi kabisa uliokuwa ukifanyika kwenye taasisi hizi za UMMA.
 
...Mmoja wa mabalozi wetu wa mwanzo mwanzo kabisa ughaibuni, sijui aliishia wapi huyu...

Mkuu huyu balozi, ninajua kuwa alikuwa na mtoto wake mmoja aliyekuwa ofisa wa ubalozi wetu pale Brussells, in the early 90s,

sikujua kuwa baba yake aliwahi kuwa balozi, duh ahsante kwa hiki kipande, nitazitafuta habari za baba yake leo.
 
Tizama haya maneno tuliyoyatumia kwenye kuhalalisha support yetu kwa Biafra, it is about time yakaturudia sisi wenyewe, I mean what is the tofauti?

1. For while people have a duty to defend the integrity of their state, and even to die in its defence this duty stems from the fact that it is theirs, and that it is important to their well-being and to the future of their children.

2. When the state ceases to stand for the honour, the protection, and the well-being of all its citizens, then it is no longer the instrument of those it has rejected.

3. In such a case the people have the right to create another instrument for their protection - in other words, to create another state.

Mkuu Mchongoma ukitaka habari zaidi za balozi Tibandebage, piga simu ubalozi wetu Canada, huyu mtoto wake yupo pale sasa.

Ahsante Mkuu!
 
R.I.P Mzee Kanyama Chiume. Huyu mzee mchango wake ni mkubwa pia kwenye historia ya nchi yetu.

Mkuu Mchongoma,

1. Heshima mbele, marehemu Chiume was a great human being, nilipata bahati ya ku-spend a lot of time karibu naye, mara kwa mara kwenye miaka ya mwishoni mwa 90s na mwanzoni mwa 2000s nilikuwa nikimtafuta kupata siasa.

2. Alikuwa Waziri wa nje wa serikali ya Banda, baadaye hawakuelewana akaishia kuwa mkimbizi bongo, aliwahi kuwa muandishi wa Daily News na Mzalendo, akifanya kazi na kina Mkapa.

3. Always straight, ni mtu ambaye asingeweza kukwambia uongo as far as siasa is concerned, aliwahi kusoma bongo zamani wakiwa darasa moja na balozi Lusinde, na pia aliwahi kutunga vitabu kadhaa, na pia amewahi kutungiwa vitabu kadhaa.

4. Nilipata nafasi ya kumuaga kwenye maombolezo, baada ya kutangulia kwake kwenye haki, na ameacha watoto imara sana na ninaamini kuwa mmoja wao atabeba tochi ya njia siasa, na Mungu amuweke mahali pema peponi.

A True African Hero!
 
Swali: Niliwahi kuambiwa kuwa General Mayunga aliwahi kuongoza kikosi cha Tanzania kusaidia upande wa Ojukwu wakati wa vita ile. Je ni kweli kuwa Nyerere alipeleka jeshi letu kwenda kumsaidia Ojukwu? Je kama ni kweli, kuna anayejua ni wangapi waliouwawa?

Picha zimeishia wapi?

Vipi, hakuna anayejua iwapo kweli Tanzania ilipeleka jeshi lake Biafra na kama kweli kikosi hicho kiliongozwa na Mayunga. Wazee wa shoka akina Mkandara, FMES, Jasusi, MMKJJ, JokaKuu, Rev Kishoka, Mtanzania, Insurgent, SteveD, Icadon, Masatu, Pundit,Mafuchila,Kitila Mkumbo na wachimabji wote wa majambo nisaidieni kujua jambo hili jamani, ingawa ni miaka mingio imepita. Wakati nikiwa pale Tabora chini ya command yake wakati akiwa Brigade Commander wa Brigade ya Magharibi wakati huo, tulikuwa tunaaminishwa na kutetemeshwa kuwa Brigedia Mayunga alikuwa na juju fulani kali sana aliyotoka nayo kwenye vita ya Biafra.
 
I salute IGP's wetu wazalendo, ambao kwa namna moja au nyingine walidumisha AMANI na utulivu nchini... Enzi hizo raia hana 'ushikaji' bure bure tu na IGP...

1964-1970 Elangwa Shaidi, 1970-1973 Hamza Azizi, 1973-1975 Samwel Pundugu, 1975-1980 Philemon Mgaya, 1980-1984 Solomon Liani

Mkuu Mchongoma, heshima tena bro:-

1. Ninaamini kuwa kati ya hwa wakuu ni Elangwa Sahidi na Pondugu tu ndio waliokuwa na clean record, na ukweli ni kwamba waliingia kwenye hzio nafasi wakiwa na mali chache sana na hata walipotoka, pia waliendelea kuwa na mali chache sana au kutokuwa nazo kabisa!

2. However, that was never the case na the rest, I mean Hamza Azizi, pamoja kukusanya mali nyingi sana pia alihusika na kuuwa kwa gari, kama ninakumbuka akiwa amelewa na hakusimama, kesi ikajaribu kusimama lakini ikazimwa tu kichini chini,

- Mgaya ndio hivyo sasa ni mmoja wa matajiri wakubwa sana mjini Dar, najua kuwa anamiliki makampuni makubwa mjini ya ulinzi wa mashirika ya private, ikwemo hata US Embassy, meaning kwamba hayuko peke yake huko!

- Then came Liani, ambaye original yake ilikuwa ni kutoka Kenya, a very close friend wa Apiyo, made a lot of cash kipindi cha wahujumu uchumi akajenga a big mansion kule Segerea, baada ya ku-retire he was os rich kwamba alifikia mahali alikorofishana na mkewe, akaishia kuishi hotelini for at least the last five years of his life, mpaka lipofikia kutangulia kwenye haki,

-Hela za wizi huwa hazina baraka kabisaa, sio siri kwamba alipata ugonjwa mkubwa, akaambukiza mpaka mkewe watoto wake wawili nao wakaukwaa, mtoto wake mmoja akashikwa akiiba kwa bunduki akaenda jela maisha, aliyebaki naye akafa kwa ngoma, ile manison yake ikaishia kuwa abandoned, mpaka leo limebaki gofu tu!
 
Sijui kama haya nayo bado yapo hapo Dar. Tulitamba nayo sana wakati wetu, na sidhani kama kweli Dar tuliwahi kuwa na usafri mzuri zaidi ya huu. je vijana wa leo mnayafahamu? tulikuwa tukiyaita kumbakumba

remonty_ikarus1.jpg
 
Ikarus kutoka Checkoslovakia au Romania!

Simon Kushoka alikuwa CEO wa Uda, yakiitwa Ikarus Kumbakumba au Bayankata wakiwa na UDA Jazz!

Nakumbuka ruti ya Temeke na Chang'ombe kulikuwa na yule mwanamama ambaye alikuwa hana masihara na tayari kukuchapa kofi ukileta ujinga!
 
Sijui kama haya nayo bado yapo hapo Dar. Tulitamba nayo sana wakati wetu, na sidhani kama kweli Dar tuliwahi kuwa na usafri mzuri zaidi ya huu. je vijana wa leo mnayafahamu? tulikuwa tukiyaita kumbakumba

remonty_ikarus1.jpg

Classic thanks
 
Back
Top Bottom