Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
1. Wakati Tanzania inatambua Biafra nilikuwa Agha Khan Secondary School, ambayo baadaye mliita Tambaza. Sisi wanafunzi wa Kiafrika wote tuliounga mkono kujitenga kwa Biafra, lakini Wahindi, wakikumbuka kutenganishwa kwa India na Pakistan, walipinga kwa dhati.
2. Ojukwu bado yupo. Kilichosababisha Biafra kujitenga, ni pogrom waliyofanyiwa Waibo ambao ndio walikuwa kama Mayahudi wa Nigeria, hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1966.
3. Alichofanya Mwalimu, alifunga safari kukutana na Jemadari Gowon, akamsihi wajadiliane na Ojwuku, watafute muafaka kwa mauaji yaliyokuwa yanaendelea.
4. Gowon akakataa akisema hawezi kujadiliana na "junior officer." Unajua tena arrogance ya Sundhurst graduates. Mwalimu akaenda Ivory Coast kukutana na Houphoet Boigny ikaamuliwa kuwa Biafra itambuliwe kama njia ya kum "pressure" Gowon akubali kujadiliana na Ojwuku.
5. Zambia na Haiti nazo zikaitambua Biafra. Lakini unajua ndugu yangu mambo haya hayawezi kumalizika bila mwingilio wa wakubwa. Uingereza ilishajua kuwa kuna mafuta huko Biafra na haikutaka kuiachia Ufaransa inufaike na mafuta hayo kwa hiyo walimsaidia Gowon juu chini kuwamaliza Wabiafra. Ufaransa ilikuwa upande wa Biafra.
6. Marekani was neutral. Actually a lot of fundraising by Biafran students was done in the US.
7. Siku ambayo Tanzania imeitambua Biafra ilikuwa easter. Mwalimu alialikwa nyumbani kwa Butiku and I happened to be there, pamoja na akina Mgaya, na Mzee Munanka (rip) Butiku alikuwa na telegrams nyingi kutoka sehemu mbalimbali zikimpongeza Mwalimu kwa msimamo huo lakini Mwalimu alikuwa na swali moja tu: "will Africa understand?" Alilirudia hilo swali mara kadhaa.
8. Hii ya Delta nadhani ni uchungu wa kuona kuwa federal government inatajirika na mafuta ya eneo hilo wakati ambapo wakazi wa eneo wamefunikwa na ufukara uliokithiri. They want a share of the pie.
Mkuu Jasusi,
1. Darasa zito sana hili, ninaikumbuka Biafra na nyimbo tulizoimba sana shuleni za za kumsifu "Koloneli Ojukwu", lakini nilikuwa mdogo sana.
2. Nikiwa NY, niliwahi kuongea na M-Nigeria mmoja ambaye ninamua-admire sana, aliwahi kuwa balozi wao kule UN na sasa ni mkuu ndani ya UN, anaitwa Gen. Gambari, ambaye ni rafiki wa karibu sana na Gen. Gowon na Ojukwu, serikali ya Nigeria inamuogopa sana huyu mkulu na hata hutumia hela kumfanya asirudi Nigeria, kwa kweli baadhi ya aliyoniambia kuhusu Biafra ni sawa kabisa na unayosema,
Lakini nina wasi wasi kuwa kwenye ku-support Biafra, we were wrong na kama sikosei kuna wakati Mwalimu, akiwa hai aliwahi ku-apologize for, I mean leo Mwanza wanataka kujitenga na Tanzania, halafu ije nchi nyingine iwa-support, that was very wrong nafikri hata standing yetu katika international world Affairs, ninaamini tulichukua a bite kidogo, halafu pia ilitu-cost sana economically kwa sababu japo nilikuwa mdogo sana lakini ninakumbuka ile michango ya kusaidia Biafra,
Lakini ashante sana kwa kipande zaid cha historia.
(a) Nadhani huyu ni Professor Ibrahim Gambari; alikuwa Ahmadu Bello University kabla hajateuliwa na General Mohammed Buhari kuwa waziri wa mambo ya nje kufuatia mapinduzi ya mwaka 1983. Sidhani kama aliwahi kuwa mwanajeshi.
(b) Ni kweli hii vita ya Biafra iliiumiza sana Tanzania katika uhusiano wa kimataifa. Nyerere aliwahi kukiri wazi kabisa kuwa ni moja ya maamuzi ambayo anayajutia sana. Alimwambia hayo Peter Enahoro aliyekuwa editor wa Gazeti la Africa Now la mwaka 1983 muda mfupi baada ya mapinduzi yaliyofanywa na General Buhari. Alidai kuwa ulikuwa uamuzi mgumu sana kwake kuufanya kwa sababu ni kama alikuwa anaunga mkono Balkanization of Africa wakati lengo lao katika OAU ilikuwa ni kuunganisha nchi za Afrika, siyo kuzigawanya vipande vidogo vidogo. Sababu iliyomtuma kufanya hivyo, kulingana na maelezo hayo, ni kwamba aliona kama serikali ya Gowon ilikuwa inawachoche Biafra kujitenga kwa vile ilikuwa ianedesha mauaji ya raia wale kama Genocide. Kwa hiyo njia pekee ikawa ni kwa hao raia kujitafuatia namna ya kujilinda wenyewe kwa kuunda serikali yao, yaani wajitenge na Nigeria.
(c) Jina la Biafra lilivuma sana Tanzania wakati huo kwani najua kuwa hadi leo pale Musoma kuna kitongoji kinaitwa Biafra (Jasusi unapafahamu Biafra?). Vile vile pale Kibara kulikuwa na Baa inaitwa Biafra Bar (Mkandara upo hapo?), Mwanza pia kulikuwa na mtaa unaitwa Biafra Street. Nadhani sehemu nyingi za Tanzania zina kitu cha kukumbukia vita hiyo ya Biafra. Ila niliwahi kuongea na Mzee mmoja aliyewahi kushika nyadhifa kadhaa kwenye serikali ya Nigeria ambaye ni wa asili ya Biafra. Alikuwa anamsifu na kumpenda sana Nyerere kwa kuunga mkono vita ile. Mzee yule alionekana kulia machozi ya wazi kabisa, zaidi yetu watanzania wenyewe, kwenye ibada ya kumkumbuka Nyerere tuliyoandaa mwaka 1999 mara tu baada ya Nyerere kufariki.