Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

No mkuu naomba kupingana na wewe katika hili. Ni katika yalee ya kukumbushana zilizopendwa katika Taifa hili. Mbona suala hili lipo wazi tu halina ubishi. Na wakati ule huyo muheshimiwa alipojiingiza kwenye siasa, alishawahi kuulizwa suala hilo wakati wa kampeni katika mkoa fulani nyanda za juu kaskazini; akajiumauma hakutoa majibu yaliyonyooka.
Ni mada tu imeibuka katika kijiwe hiki, na kama zilivyo nyingine ambazo wadau huchangiachangia kutokana na kumbukumbu zao. Au umeguswa binafsi nini mkulu? sema kama imekugusa na unashauri tuiachilie hapa hapa kamanda, nitaheshimu ombi lako.
 

Mwanzange,

..siwezi kumhukumu Tamimu, lakini naamini aliipenda nchi yake na alikuwa na uchungu nayo. after all alijitolea mhanga kama askari wakati wa vita vya Kagera.

..pia ninaamini hata wale waliotumwa kwenda kumkamata, naamini walikuwa wakiitumikia nchi yao kwa mapenzi yale yale aliyokuwa nayo Tamimu.

..naamini Afisa Usalama yeyote wa wakati ule angeweza kuwepo ktk mkasa ule.

..nitakuwa mzito kidogo kunyoosha kidole kwamba fulani ndiyo alimfyatua risasi iliyomuua Cpt.Mohamed Tamim.
 
mnaonge sana balada ya kuleta picha



mazishi ya Ustadh Saleh Issa who was killed at Mwembechai on 13 February, 1998.
 
Mwanafunzi CHUKI ATHUMANI alyepiwa risasi ya moto na polisi akiwa muhimbili ambako aliendelea kupigwa pingu huku akiwa kitandani pale Muhimbili





Chuki Athumani risasi aliyopigwa ilivunja sehemu ya mfupi eneo la kifuani ikawa kipande cha mfupa kinakandamiza mishipa ya fahamu katika uti wa mgongo (Spinal cord).

Hiyo ilikuwa ni kwa mujibu wa uchunguzi wa awali na hivyo maelekezo yalikuwa kufanyika uchunguzi zaidi ambao ingepelekea kuondolewa kipande hicho cha mfupa kisiendelee kukandamiza mishipa ya fahamu. Kilichoendelea ni kuwa mtoto huyo alifungwa pingu kitandani na watu kuzuiliwa kumwona.

wauguzi walishindwa kumpeleka Chuki Athumani kwenye chumba cha uchunguzi kwa sababu kafungwa pingu kitandani

Kilichofuatia ni Chuki kupooza na kupoteza kabisa fahamu katika sehemu zake za chini na akawa hapewi tena matibabu yoyote ya tatizo hilo la msingi.

Lakini pamoja na kupooza huko akaendelea kufungwa pingu na huku ndugu na jamaa zake wakizuiliwa kukaa naye kumpa msaada.

Matokeo yake mifupa ikakaribia kuwa nje kutokana na madonda yaliyotokana na kukosa msaada wa kuhudumiwa akiwa na hajandogo na kukalia sehemu moja muda mrefu.

Wakati wauguzi wanashindwa kumtibia Chuki kwa kufungwa pingu na wakati anaendelea kukatika madonda kwa kukosa msaada, serikali iliibuka na dai kwamba wapo vijana waliofundishwa kuleta vurugu na ilionekana vijana hao ni hatari sana kiasi kwamba risasi za moto za polisi zisingetosha tena ila zitumike zile za jeshi la wananchi (Tazama gazeti la watu makini Mtanzania No. 706 la Februari 20, 1998 na gazeti la nguvu ya Hoja, Rai No. 225 la Februari 19, 1998). Na maamuzi haya kuelezwa kuwa yalifikiwa katika vikao vilivyoendeshwa chini ya Uenyekiti wa Rais Benjamin William Mkapa.
 
GT,

Lete basi picha CLEAR 1998 sio zamani ubora wa picha ulikuwa mzuri zaidi ya hizi...
 
Hivi nini kilichosababisha sokomoko la Mwembechai? Sikuwepo Bongo wakati huo.
 

Hii hapana, kipindi kile cha Mwalimu umiliki mabasi uliyopewa bakshish kwa kununua mabasi serikali haiwezekani naikataa 100%
 
Jasusi,

Nilikuwepo na kuyashuhudia. Nangoja ma Spin doctors waanze nianze kuwaweka mstari sawa.
 
Hii hapana, kipindi kile cha Mwalimu umiliki mabasi uliyopewa bakshish kwa kununua mabasi serikali haiwezekani naikataa 100%

Mkuu Heshima yako, na ni haki yako kuikataa lakini haina maana haikutokea na viongozi wengi walinufaika na huu mpango wa kupewa zawadi na makampuni ya nje,

Mabasi sita toka Hungary, yaliyokuja na mabasi mengine ya UDA yalilikuwa na rangi tofauti na mengine ikiwa ni uamuzi wa kampuni hiyo huko Hungary kuwapa hawa wananchi wetu mabasi hayo, sijui la umiliki ulipolitoa ni wapi mkuu maana hakuna aliye-mention maneno ya umiliki,

Kilichosmewa ni kwamba walipewa hayo mabasi na UDA iliwafidia ingawa sio hela sawa na thamani ya mabasi yenyewe, lakini walilipwa na pia ukapewa mfano wa jinsi viongozi wetu walivyotumia hizo nafasi kuepeleka watotow ao kusoma nje hasa US, na US waliposhiotuka waliwarudisha nyumbani watoto wote, mpaka wa Mkapa, Mahalu, na hata Warioba,

I mean kukataa 100% ni one thing, na kwamba jamaa walipewa mabasi ni another 100% truth, na kwamba viongozi wengi walipewa zawadi mbali mbali akiwemo Mwalimu mwenyewe, kuna safari moja Japan alipewa TV moja la 50' "inch" kutoka kampuni ya Sony, ambayo alimpa Madaraka, yalikuwa ni mambo ya kawaida na sio ya rushwa, kama siku hizi!

Ahsante Mkuu!
 
tutasahu vipi mwaka 1999 ambako MALECELA aliamua kumbatiza kwa maji Mr. Issa Juma kuingia CCM

AMA KWELI TUMETOKA MBALI

 
Weka picha za mafisadi katika ufisadi yaani ulipoanza kwani tutakumbukia vizuri zaidi. Mwenya nazo amwage hapa
 
MALECELA huyo huyo aliwaita waliokuwa wakipinga mabucha ya NGURUWE kwenye residential areas kuwa wana VICHWA MAJI




Nakumbuka siku hii ilikuwa ni ijumaa 1993 nje ya mahakam ya Kisutu
 
mnaonge sana balada ya kuleta picha

Mkuu Heshima yako, kama una picha iweke hapa, kama huna basi unaweza kula historia na picha hapa, hatuna mashindano wala mandate kwenye hii thread na wala hatuna malumbano kwa sababu, tunajaribu ku-put together habari mbali mbali na kuzichambua na kumuachia mwananchi msomaji aamue mwenyewe ukweli na mapungufu ya habari, understanding kwamba wengi tulikuwa wadogo sana ki-umri na kama kawaida kwenye siasa hakuna permanent truth,

So far so good, binafsi niliyeanzisha huu mjadala nimeridhika na the goal ya kuanzisha hii thread, infact nimetumiwa ujumbe na viongozi wengi sana wa taifa wakiwa wamefurahishwa sana na hii thread kwa sababu ukweli mwingi umekuwa set straight, na hata wananchi wengi wamefurahishwa sana na hii historia na picha,

Mkuu GT, naomba tu ujiunge nasi katika kujaribu kuichambua historia yetu na picha zake, hapa hakuna mashindano wala ubingwa.

Ahsante Mkuu na Tunaendelea mbele.
 
GAME THEORY Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

MALECELA huyo huyo aliwaita waliokuwa wakipinga mabucha ya NGURUWE kwenye residential areas kuwa wana VICHWA MAJI

The truth is:- On the Back Cover

1. On Friday 13 February, 1998 at the instigation of a Catholic priest of Mburahati parish in Dar es Salaam, the Tanzania government ordered its para-military police force to open fire on unarmed Muslims at Mwembechai area, killing at least four of them.

2. It was soon discovered that the seditious claims made by the Catholic priest and repeatedly broadcast on a Catholic radio that Muslims were ridiculing Jesus were a sheer fabrication.

3. Muslims’ demands for an independent probe team to investigate the killings were immediately rejected by the Minister for Home Affairs. The government also banned a meeting organised by Muslim women to speak out about the sexual humiliations and indignities they suffered at the hands of male police officers while in remand prison.

In this book Dr. Njozi looks at the Mwembechai killings as a manifestation of a simmering political crisis in Tanzania. The book provides unsettling details about religious discrimination in a country which is thought by many as setting a shining example to rest of the world. Tha author’s analysis of the looming political tragedy in Tanzania is both illuminating and sympathetic.
 


Mlundwa



Nuti



Tesha

Baadhi ya Mabondia wa TZ waliovuma enzi hizo.
 
Dar es salaama kuna mtaa unaitwa Shaaban Robert, na vile vile kuna shule ya sekondari inayoitwa Shaaban Robert Secondary School.

Shaaban Robert alikuwa mtu mwenye akili sana na mtaalamu mwanzilishi wa fasihi ya kiswahili. Aliandika vitabu vingi sana vya riwaya (novels) pamoja na vitabu vyenye mkusanyiko wa mashairi (anthologies) aliyotunga mwenyewe. kati ya vitabu nivikumbukavyo ni pamoja na:

  1. Wasifu Wa Siti Binti Saad, Mwimbaji wa Unguja. Diwani Ya Shaaban 3:
  2. Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini,
  3. Utenzi wa Vita ya Uhuru: 1939 Hata 1945.
  4. Insha, Na Mashairi
  5. Mapenzi Bora
  6. Kufikirika
  7. Kusadikika
  8. Kielezo Cha Fasili
  9. Masomo Yenye Adili
  10. Adili na Nduguze
  11. Utubora Mkulima (Diwani Ya Shaaban 8)

Shaaban Robert alikuwa mzaliwa wa Tanga, lakini katika vitabu vyake amezungumzia characters wengi wa kutokea Unguja, kwa mfano yule Siti wa Sitawa kwenye kile kitabu cha Wasifu wa Siti bint Saad alikuwa ni mwanamke wa Zanzibar, na kiliandikwa mwaka 1958. Hii inaonyesha jinsi gani wabara na wazenj walivyokuwa na uhusiano wa karibu tangu zamani, siyo wa kisiasa. Ninawashangaa sana hao wanaodai kutaka kuitenga zanzibar kutoka kwenye muungano wa nchi yetu, kwa kudhani kuwa wabara ni watu wabaya sana wanaoionea Zanzibar.

Picha mojawapo ya Shaaban Robert

Hili hapa ndilo kaburi lake


Limeachwa kama vile la mtu asiye kumbukwa tena.
 
GT,

Lete basi picha CLEAR 1998 sio zamani ubora wa picha ulikuwa mzuri zaidi ya hizi...

Nafikiri kazinyofoa kutoka magazetini tu hizo. Kitu hiki ndio kinachonishangaza sana hasa kwenye haya mablogu yetu ya kibantu. Wanasubiri mtu mmoja aweke picha halafu utaona msururu wa mablogu wanasubiri wanyonye kutoka kwa mmoja. hazina hata mvuto. Mi nasubiria hapa kijiweni tu; mavituuuz mapyamapya yananyunyizwa daily. Si mchezo!!!
Kamanda FMES na wengineo endeleeni kukaza buti. Kamulieni tu.
 

Mkulu ES hapana hii imepinda sihitaji data wala maelezo marefu kuthibitisha kuwa sio sahihi. Nakubaliana na maelezo ya Mwalimu Kichuguu hapa chini


Na kama ilivyoweka kwa msisitizo na Jokakuu hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…