Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

wana jamboForums,

..nadhani suala la kukamatwa Tamimu lilikuwa ni secret-operation na nadhani siyo vizuri kuwataja kwa majina wale waliohusika.

..naamini Afisa Usalama yeyote aliyehusika katika operation hiyo alikuwa mtu wa chini sana na alikuwa akitekeleza amri na maagizo ya wakubwa wake wa kazi.
No mkuu naomba kupingana na wewe katika hili. Ni katika yalee ya kukumbushana zilizopendwa katika Taifa hili. Mbona suala hili lipo wazi tu halina ubishi. Na wakati ule huyo muheshimiwa alipojiingiza kwenye siasa, alishawahi kuulizwa suala hilo wakati wa kampeni katika mkoa fulani nyanda za juu kaskazini; akajiumauma hakutoa majibu yaliyonyooka.
Ni mada tu imeibuka katika kijiwe hiki, na kama zilivyo nyingine ambazo wadau huchangiachangia kutokana na kumbukumbu zao. Au umeguswa binafsi nini mkulu? sema kama imekugusa na unashauri tuiachilie hapa hapa kamanda, nitaheshimu ombi lako.
 
Mwanzange said:
No mkuu naomba kupingana na wewe katika hili. Ni katika yalee ya kukumbushana zilizopendwa katika Taifa hili. Mbona suala hili lipo wazi tu halina ubishi. Na wakati ule huyo muheshimiwa alipojiingiza kwenye siasa, alishawahi kuulizwa suala hilo wakati wa kampeni katika mkoa fulani nyanda za juu kaskazini; akajiumauma hakutoa majibu yaliyonyooka.
Ni mada tu imeibuka katika kijiwe hiki, na kama zilivyo nyingine ambazo wadau huchangiachangia kutokana na kumbukumbu zao. Au umeguswa binafsi nini mkulu? sema kama imekugusa na unashauri tuichilie hapa hapa kamanda, nitaheshimu ombi lako.

Mwanzange,

..siwezi kumhukumu Tamimu, lakini naamini aliipenda nchi yake na alikuwa na uchungu nayo. after all alijitolea mhanga kama askari wakati wa vita vya Kagera.

..pia ninaamini hata wale waliotumwa kwenda kumkamata, naamini walikuwa wakiitumikia nchi yao kwa mapenzi yale yale aliyokuwa nayo Tamimu.

..naamini Afisa Usalama yeyote wa wakati ule angeweza kuwepo ktk mkasa ule.

..nitakuwa mzito kidogo kunyoosha kidole kwamba fulani ndiyo alimfyatua risasi iliyomuua Cpt.Mohamed Tamim.
 
mnaonge sana balada ya kuleta picha

Image21.jpg


mazishi ya Ustadh Saleh Issa who was killed at Mwembechai on 13 February, 1998.
 
Mwanafunzi CHUKI ATHUMANI alyepiwa risasi ya moto na polisi akiwa muhimbili ambako aliendelea kupigwa pingu huku akiwa kitandani pale Muhimbili

Image24.jpg


Image25.jpg


Chuki Athumani risasi aliyopigwa ilivunja sehemu ya mfupi eneo la kifuani ikawa kipande cha mfupa kinakandamiza mishipa ya fahamu katika uti wa mgongo (Spinal cord).

Hiyo ilikuwa ni kwa mujibu wa uchunguzi wa awali na hivyo maelekezo yalikuwa kufanyika uchunguzi zaidi ambao ingepelekea kuondolewa kipande hicho cha mfupa kisiendelee kukandamiza mishipa ya fahamu. Kilichoendelea ni kuwa mtoto huyo alifungwa pingu kitandani na watu kuzuiliwa kumwona.

wauguzi walishindwa kumpeleka Chuki Athumani kwenye chumba cha uchunguzi kwa sababu kafungwa pingu kitandani

Kilichofuatia ni Chuki kupooza na kupoteza kabisa fahamu katika sehemu zake za chini na akawa hapewi tena matibabu yoyote ya tatizo hilo la msingi.

Lakini pamoja na kupooza huko akaendelea kufungwa pingu na huku ndugu na jamaa zake wakizuiliwa kukaa naye kumpa msaada.

Matokeo yake mifupa ikakaribia kuwa nje kutokana na madonda yaliyotokana na kukosa msaada wa kuhudumiwa akiwa na hajandogo na kukalia sehemu moja muda mrefu.

Wakati wauguzi wanashindwa kumtibia Chuki kwa kufungwa pingu na wakati anaendelea kukatika madonda kwa kukosa msaada, serikali iliibuka na dai kwamba wapo vijana waliofundishwa kuleta vurugu na ilionekana vijana hao ni hatari sana kiasi kwamba risasi za moto za polisi zisingetosha tena ila zitumike zile za jeshi la wananchi (Tazama gazeti la watu makini Mtanzania No. 706 la Februari 20, 1998 na gazeti la nguvu ya Hoja, Rai No. 225 la Februari 19, 1998). Na maamuzi haya kuelezwa kuwa yalifikiwa katika vikao vilivyoendeshwa chini ya Uenyekiti wa Rais Benjamin William Mkapa.
 
GT,

Lete basi picha CLEAR 1998 sio zamani ubora wa picha ulikuwa mzuri zaidi ya hizi...
 
Hivi nini kilichosababisha sokomoko la Mwembechai? Sikuwepo Bongo wakati huo.
 
1.

sio kwamba huyu meneja alijaribu kuyachukua, isipokuwa huyu bwana alinyamaza kimyaa, ukweli ni kwamba yale mabasi sita yalikuja yakiwa na rangi ya Blue, kwa sababu mabasi yote yaliwekwa pale Ubungo, enzi zile ukiwa Mlimani Park au Hapa pembeni yaani kwenye Bendi ya Kyauri Voice, ulikuwa unayaona yote yakiwa pale,

Kuna watu ndani ya UDA walioona wivu na kumaua kuyapaka rangi haraka haraka, lakini Manager wa UDA then simjui alikuwa ni nani, lakini najua kuwa he was a very fair man, kwani nilikuwa na washikaji waliokuwa wakipigia bendi ya UDA na kuichezea mpira timu ya UDA, ndiye aliyeingilia kati na kutaka kujua kuhusu the whole deal ya yale mabasi sita, ndio akashia kuwalipa something ambacho hakikukubalika na wakubwa wake wa kazi, lakini hawa wenye mabasi sita mmoja wao yaani huyu John, alikuwa na connection na Kawawa wa kusini mwenziwe, alienda kumuona na ishu ikawa dead!

2. Kuhusu zawadi kwa viongozi, ukweli ni kwamba viongozi wa juu walikuwa wanapewa zawadi kila siku na wala hata siku moja hawakuwahi ku-surrender kwa serikali, I have seen it all hizi sheria zilikuwa ni kwa wanyonge tu sio kwa wakubwa, infact ni hii tabia mbaya ndio iliyowafanya US kuwafukuza watoto wote wa wakubwa kule kwao waliokuwa wana-scholarship za zawadi, hata watoto wa Mkapa na Mahalu walikuwa involved na hii deal!

Hii hapana, kipindi kile cha Mwalimu umiliki mabasi uliyopewa bakshish kwa kununua mabasi serikali haiwezekani naikataa 100%
 
Jasusi,

Nilikuwepo na kuyashuhudia. Nangoja ma Spin doctors waanze nianze kuwaweka mstari sawa.
 
Hii hapana, kipindi kile cha Mwalimu umiliki mabasi uliyopewa bakshish kwa kununua mabasi serikali haiwezekani naikataa 100%

Mkuu Heshima yako, na ni haki yako kuikataa lakini haina maana haikutokea na viongozi wengi walinufaika na huu mpango wa kupewa zawadi na makampuni ya nje,

Mabasi sita toka Hungary, yaliyokuja na mabasi mengine ya UDA yalilikuwa na rangi tofauti na mengine ikiwa ni uamuzi wa kampuni hiyo huko Hungary kuwapa hawa wananchi wetu mabasi hayo, sijui la umiliki ulipolitoa ni wapi mkuu maana hakuna aliye-mention maneno ya umiliki,

Kilichosmewa ni kwamba walipewa hayo mabasi na UDA iliwafidia ingawa sio hela sawa na thamani ya mabasi yenyewe, lakini walilipwa na pia ukapewa mfano wa jinsi viongozi wetu walivyotumia hizo nafasi kuepeleka watotow ao kusoma nje hasa US, na US waliposhiotuka waliwarudisha nyumbani watoto wote, mpaka wa Mkapa, Mahalu, na hata Warioba,

I mean kukataa 100% ni one thing, na kwamba jamaa walipewa mabasi ni another 100% truth, na kwamba viongozi wengi walipewa zawadi mbali mbali akiwemo Mwalimu mwenyewe, kuna safari moja Japan alipewa TV moja la 50' "inch" kutoka kampuni ya Sony, ambayo alimpa Madaraka, yalikuwa ni mambo ya kawaida na sio ya rushwa, kama siku hizi!

Ahsante Mkuu!
 
tutasahu vipi mwaka 1999 ambako MALECELA aliamua kumbatiza kwa maji Mr. Issa Juma kuingia CCM

AMA KWELI TUMETOKA MBALI

Image37.jpg
 
Weka picha za mafisadi katika ufisadi yaani ulipoanza kwani tutakumbukia vizuri zaidi. Mwenya nazo amwage hapa
 
MALECELA huyo huyo aliwaita waliokuwa wakipinga mabucha ya NGURUWE kwenye residential areas kuwa wana VICHWA MAJI


Image34.jpg


Nakumbuka siku hii ilikuwa ni ijumaa 1993 nje ya mahakam ya Kisutu
 
mnaonge sana balada ya kuleta picha

Mkuu Heshima yako, kama una picha iweke hapa, kama huna basi unaweza kula historia na picha hapa, hatuna mashindano wala mandate kwenye hii thread na wala hatuna malumbano kwa sababu, tunajaribu ku-put together habari mbali mbali na kuzichambua na kumuachia mwananchi msomaji aamue mwenyewe ukweli na mapungufu ya habari, understanding kwamba wengi tulikuwa wadogo sana ki-umri na kama kawaida kwenye siasa hakuna permanent truth,

So far so good, binafsi niliyeanzisha huu mjadala nimeridhika na the goal ya kuanzisha hii thread, infact nimetumiwa ujumbe na viongozi wengi sana wa taifa wakiwa wamefurahishwa sana na hii thread kwa sababu ukweli mwingi umekuwa set straight, na hata wananchi wengi wamefurahishwa sana na hii historia na picha,

Mkuu GT, naomba tu ujiunge nasi katika kujaribu kuichambua historia yetu na picha zake, hapa hakuna mashindano wala ubingwa.

Ahsante Mkuu na Tunaendelea mbele.
 
GAME THEORY Re: Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha

MALECELA huyo huyo aliwaita waliokuwa wakipinga mabucha ya NGURUWE kwenye residential areas kuwa wana VICHWA MAJI

The truth is:- On the Back Cover

1. On Friday 13 February, 1998 at the instigation of a Catholic priest of Mburahati parish in Dar es Salaam, the Tanzania government ordered its para-military police force to open fire on unarmed Muslims at Mwembechai area, killing at least four of them.

2. It was soon discovered that the seditious claims made by the Catholic priest and repeatedly broadcast on a Catholic radio that Muslims were ridiculing Jesus were a sheer fabrication.

3. Muslims’ demands for an independent probe team to investigate the killings were immediately rejected by the Minister for Home Affairs. The government also banned a meeting organised by Muslim women to speak out about the sexual humiliations and indignities they suffered at the hands of male police officers while in remand prison.

In this book Dr. Njozi looks at the Mwembechai killings as a manifestation of a simmering political crisis in Tanzania. The book provides unsettling details about religious discrimination in a country which is thought by many as setting a shining example to rest of the world. Tha author’s analysis of the looming political tragedy in Tanzania is both illuminating and sympathetic.
 
mlundwa.jpg

Mlundwa

nuti.jpg

Nuti

tesha.jpg

Tesha

Baadhi ya Mabondia wa TZ waliovuma enzi hizo.
 
Dar es salaama kuna mtaa unaitwa Shaaban Robert, na vile vile kuna shule ya sekondari inayoitwa Shaaban Robert Secondary School.

Shaaban Robert alikuwa mtu mwenye akili sana na mtaalamu mwanzilishi wa fasihi ya kiswahili. Aliandika vitabu vingi sana vya riwaya (novels) pamoja na vitabu vyenye mkusanyiko wa mashairi (anthologies) aliyotunga mwenyewe. kati ya vitabu nivikumbukavyo ni pamoja na:

  1. Wasifu Wa Siti Binti Saad, Mwimbaji wa Unguja. Diwani Ya Shaaban 3:
    wasifu_wa_sitti.gif
  2. Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini,
    Maisha-Yangu.gif
  3. Utenzi wa Vita ya Uhuru: 1939 Hata 1945.
  4. Insha, Na Mashairi
  5. Mapenzi Bora
    Mapenzi-Bora.gif
  6. Kufikirika
    Kufikirika.gif
  7. Kusadikika
    Kusadikika.gif
  8. Kielezo Cha Fasili
    Kielezo-cha-Fasili.gif
  9. Masomo Yenye Adili
  10. Adili na Nduguze
  11. Utubora Mkulima (Diwani Ya Shaaban 8)

Shaaban Robert alikuwa mzaliwa wa Tanga, lakini katika vitabu vyake amezungumzia characters wengi wa kutokea Unguja, kwa mfano yule Siti wa Sitawa kwenye kile kitabu cha Wasifu wa Siti bint Saad alikuwa ni mwanamke wa Zanzibar, na kiliandikwa mwaka 1958. Hii inaonyesha jinsi gani wabara na wazenj walivyokuwa na uhusiano wa karibu tangu zamani, siyo wa kisiasa. Ninawashangaa sana hao wanaodai kutaka kuitenga zanzibar kutoka kwenye muungano wa nchi yetu, kwa kudhani kuwa wabara ni watu wabaya sana wanaoionea Zanzibar.

Picha mojawapo ya Shaaban Robert
srobert_jpg_w300h501.jpg

Hili hapa ndilo kaburi lake

srobert1_jpg_w560h351.jpg

Limeachwa kama vile la mtu asiye kumbukwa tena.
 
GT,

Lete basi picha CLEAR 1998 sio zamani ubora wa picha ulikuwa mzuri zaidi ya hizi...

Nafikiri kazinyofoa kutoka magazetini tu hizo. Kitu hiki ndio kinachonishangaza sana hasa kwenye haya mablogu yetu ya kibantu. Wanasubiri mtu mmoja aweke picha halafu utaona msururu wa mablogu wanasubiri wanyonye kutoka kwa mmoja. hazina hata mvuto. Mi nasubiria hapa kijiweni tu; mavituuuz mapyamapya yananyunyizwa daily. Si mchezo!!!
Kamanda FMES na wengineo endeleeni kukaza buti. Kamulieni tu.
 
Mkuu Heshima yako, na ni haki yako kuikataa lakini haina maana haikutokea na viongozi wengi walinufaika na huu mpango wa kupewa zawadi na makampuni ya nje,

Mabasi sita toka Hungary, yaliyokuja na mabasi mengine ya UDA yalilikuwa na rangi tofauti na mengine ikiwa ni uamuzi wa kampuni hiyo huko Hungary kuwapa hawa wananchi wetu mabasi hayo, sijui la umiliki ulipolitoa ni wapi mkuu maana hakuna aliye-mention maneno ya umiliki,

Kilichosmewa ni kwamba walipewa hayo mabasi na UDA iliwafidia ingawa sio hela sawa na thamani ya mabasi yenyewe, lakini walilipwa na pia ukapewa mfano wa jinsi viongozi wetu walivyotumia hizo nafasi kuepeleka watotow ao kusoma nje hasa US, na US waliposhiotuka waliwarudisha nyumbani watoto wote, mpaka wa Mkapa, Mahalu, na hata Warioba,

I mean kukataa 100% ni one thing, na kwamba jamaa walipewa mabasi ni another 100% truth, na kwamba viongozi wengi walipewa zawadi mbali mbali akiwemo Mwalimu mwenyewe, kuna safari moja Japan alipewa TV moja la 50' "inch" kutoka kampuni ya Sony, ambayo alimpa Madaraka, yalikuwa ni mambo ya kawaida na sio ya rushwa, kama siku hizi!

Ahsante Mkuu!

Mkulu ES hapana hii imepinda sihitaji data wala maelezo marefu kuthibitisha kuwa sio sahihi. Nakubaliana na maelezo ya Mwalimu Kichuguu hapa chini

Mabasi yale yalinunuliwa na bwana mmoja nadhani aliyekuwa meneja wa UDA akijulikana kwa jina la Mahimbo katikati ya miaka ya sabini, nadhani kati ya mwaka 1975 na mwaka 1976 hivi baada ya yale mabasi ya ghorofa ya DMT kuishia. Wakati huo kipindi cha mikingamo kilikuwa hakijaanza, hiki kilikuja mwanzoni mwa miaka ya themanini hivi, nadhani mwaka 1982 au 1983.

Mabasi aliyopewa bwana Mahimbo yalichukuliwa na UDA kwa sababu mbili: Kwanza alifanya makosa kuyaacha yakaletwa yakiwa na rangi (nadhani pamoja na nembo) ya UDA. Pili serikali ilisema kuwa mabasi hayo yalitolewa na kiwanda cga Ikarus kama bakshishi kwa mteja wake, ambaye alikuwa ni UDA siyo Mahimbo; yeye alikuwa ameiwakilisha UDA kama mtumishi wake tu.

Na kama ilivyoweka kwa msisitizo na Jokakuu hapa

.taratibu za utumishi wa umma zinaelekeza kwamba zawadi kama hiyo inapaswa kuwa-surrendered serikalini.

..kwa jinsi hali ilivyokuwa wakati ule siamini kama huyo meneja alithubutu kuyachukua mabasi hayo.

..tatizo kubwa lilikuwa ni "zawadi za wananchi" kwa viongozi wanapotembelea mikoani na wilayani.

..wananchi walikuwa wakilazimishwa kutoa zawadi kama mifugo na mazao kwa viongozi wa chama na serikali waliowatembelea.

..Mzee Mwinyi alikuja kuusitisha utamaduni huo ambao kwa kweli naona ulikuwa unyonyaji wa mchana kweupe.

NB:

..viongozi pia walikuwa na tabia ya kujichotea bidhaa za viwandani kila walipofanya ziara zilizokuwa zikiitwa "ziara za ukaguzi."
 
Back
Top Bottom