William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
- Thread starter
-
- #1,001
Hii picha ya ya Arusha jengo la Remtula Pirbhai ni classic, imaging 1962 barabara lami safi taa za barabarani mitaa misafi.... halafu mtu akisema bora mkoloni mnakuja juu
maneno mazito sana hayo.
Sana kabisa mkuu, nakupa tano kwa hilo. Na kila mtu eti anaimba taarabu siku hizi, sio kuwadhalilisha watu wa kutoka sehemu nyingine ila tu mambo mengi huwa yanakuwa na asili zake. Huwezi kumkuta msandawe akicheza mdumange; na vilevile sitaji kabila lakini utakuta nayeye anaimba taarabu. Taarab ilikuwa yenyewe ile orijino, tartiiiiib ya akina afro shirazi unapata maneno matamu huku umetulia na kikoi chako unashushia na kahawa na kashata. Lakini siku hizi ndio vidole juu mipasho na kupigana vijembe. Imeondolewa maana kabisa.Mkuu ninaikumbuka, lakini nafikiri ilijifia kifo cha mende maana ndombolo unajua iliua bendi nyingi sana ambazo zilishindwa kubadilika, hivi unajua siku hizi hata taarabu imeanza kugeuka kuwa na ndombolo kwa ndani yake.
Mnaukumbuka ule wimbo wa Msondo Ngoma Sakina
Saki i i Sakina, tulia dada nikueleze,
nimepata barua kutoka nyumbani
inayoeleza umepata mchumba
tafadhali Sakina....fanya haraka
Kibwagizo
Naukamuoe huyo kijana, dada Sakina, usimkatea,
umezoea kukataa wachumba, olewa dada
ulimwengu wa kisasa una matatizo
Kama kuna mmoja wenu mwenye huu wimbo na nyingine za nyakati hizo naomba!
Tuwaenzi Viongozi wa Taifa letu
1) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP)
Mwanzilishi wa Taifa letu, alituunganisha Watanzania wote tukawa wamoja, sasa watanzania wengi hatuitani kwa makabila yetu bali tunaitana kwa utaifa wetu.
Aliwezesha Watanzania wote kuishi kwa Haki na Amani
Sisi Watanzania tulimpenda sana lakini Muumba wake/wetu alimpenda zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen
2) Mh. Alhaji Alli Hassan Mwinyi
Rais wa awamu ya pili wa Taifa letu.
Alipokea nchi ikiwa imedidimia kiuchumi.
Alikubaliana na masharti ya Shirika la fedha duniani pamoja na Benk ya Dunia.
Alituwezesha Watanzania Wengi (tusiokuwa na kitu) tukawa na fedha mfukoni.
Baadhi ya Wananchi waliacha kazi Serikalini, wakawa wafanya biashara, maana ilionekana kuwa kazi za serikalini hazina mshahara wa kutosha maisha ya leo.
Alituanzishia "Ruksa".
Aliendeleza utawala wa Haki na Amani.
3) Mh. Benjamen William Mkapa
Rais wa Awamu ya tatu ya Taifa letu.
Aliwezesha "Wasomi" kutambulika.
Aliwezesha Wasomi wengi kupata kazi
Aliwezesha Uchumi kukua hadi 9%
Aliwezesha Watanzania kutambulika nje ya nchi.
Aliendeleza Utawala wa Haki na Amani.
4) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wetu wa Awamu ya Nne ambayo ipo madarakani
Anaendeleza Utawala wa Haki na Amani
Ni Rais makini kuliko wote Afrika
Ni Rais anayewezesha Uchumi wa Nchi yetu kukua kwa kasi.
Ninamuomba Mungu amjalie ili atuongoze hadi mwaka 2015.
sasa katika hawa maraisi wanne,umesahau kutwambia nani ndio aliowapa wahindi nchi yetu? tunaomba jibu tafadhali

Muhidini Cheupe "Nylon" baadaye alikwenda NDOVU ya Arusha iliyosumbua sana na akina Charles Mngodo,Mohamed Bob Chopa wakiungana Zamoyoni Mogella,Hamis Thobias Gaga " Gagarino" na James kisaka wakitokea Volkano ya Kenya...Yussuf Bana, Zamoyoni Mogela, katikati ni MUHIDIN CHEUPE wa Yanga.
Ndugu zao huku Dar yaani PILSNER ya akina:...hiyoo ndio NDOVU ya arusha bwana ...chama kubwa...
...james kisaka..
...simon "kishoka"...aka "uruguay"
...lila shomari..
..mwanga luheya...
hamis thobious gaga "gaga-gagarhino"
mohamed "bob" chopa..
..mohamed mateneke "speed"
charles mngodo....
..ACHANENI NA HIYO LIST WAZEEE...ongezeeni mnaokumbuka..!!!
Sana kabisa mkuu, nakupa tano kwa hilo. Na kila mtu eti anaimba taarabu siku hizi, sio kuwadhalilisha watu wa kutoka sehemu nyingine ila tu mambo mengi huwa yanakuwa na asili zake. Huwezi kumkuta msandawe akicheza mdumange; na vilevile sitaji kabila lakini utakuta nayeye anaimba taarabu. Taarab ilikuwa yenyewe ile orijino, tartiiiiib ya akina afro shirazi unapata maneno matamu huku umetulia na kikoi chako unashushia na kahawa na kashata. Lakini siku hizi ndio vidole juu mipasho na kupigana vijembe. Imeondolewa maana kabisa.
P.S. Na niliwahi kuomba before anayejua wapi naweza kupata nyimbo za Afro Shirazi Youth naombeni nipate kuzisikiliza........
Nawakilisha.
Mengine ni yako! Usije tulisha sumu!
Nasi wa Bara twajua namna ya kula chapati ati.
Muhidini Cheupe "Nylon" baadaye alikwenda NDOVU ya Arusha iliyosumbua sana na akina Charles Mngodo,Mohamed Bob Chopa wakiungana Zamoyoni Mogella,Hamis Thobias Gaga " Gagarino" na James kisaka wakitokea Volkano ya Kenya.