Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Hii picha ya ya Arusha jengo la Remtula Pirbhai ni classic, imaging 1962 barabara lami safi taa za barabarani mitaa misafi.... halafu mtu akisema bora mkoloni mnakuja juu

No way, mkoloni ana uzuri na ubaya wake kama vile viongozi wetu wa sasa, lakini bado ni bora mkoloni aliondoka, tena on the right time, thanks kwa Mwalimu Nyerere na TANU,

Ni afadhali niwe masikini huru, kuliko kuwa tajiri under utumwa wa mkoloni, for that special thanx kwa viongozi kama Chifu Mkwawa, Kinjekitile, na the likes kwa their sacrifice, ili one day meaning leo mimi nije kua huru,

Wanasema asiyejua kufa, mwambieni achungulie kaburi!

Mkuu Mchongoma again heshima mbele kwa picha hizi saafi sana.
 
Jamani kuna mtu ana picha ya juu (overview/plan view) ya jiji la dar es salaam zamani au maeneo ya kariakoo? Tafadhali tuwekee tulinganishe mabadiliko ya jiji la DSM. Maana naona nyumba siku za karibuni zimeota kama uyoga na kupoteza kabisa picha ya miaka mingi ya dar es salaam na utamaduni wake!
 
FMES, Kichuguu na wengine,

Mnaukumbuka ule wimbo wa Msondo Ngoma Sakina

Saki i i Sakina, tulia dada nikueleze,
nimepata barua kutoka nyumbani
inayoeleza umepata mchumba
tafadhali Sakina....fanya haraka

Kibwagizo

Naukamuoe huyo kijana, dada Sakina, usimkatea,
umezoea kukataa wachumba, olewa dada
ulimwengu wa kisasa una matatizo

Kama kuna mmoja wenu mwenye huu wimbo na nyingine za nyakati hizo naomba!
 
Mkuu ninaikumbuka, lakini nafikiri ilijifia kifo cha mende maana ndombolo unajua iliua bendi nyingi sana ambazo zilishindwa kubadilika, hivi unajua siku hizi hata taarabu imeanza kugeuka kuwa na ndombolo kwa ndani yake.
Sana kabisa mkuu, nakupa tano kwa hilo. Na kila mtu eti anaimba taarabu siku hizi, sio kuwadhalilisha watu wa kutoka sehemu nyingine ila tu mambo mengi huwa yanakuwa na asili zake. Huwezi kumkuta msandawe akicheza mdumange; na vilevile sitaji kabila lakini utakuta nayeye anaimba taarabu. Taarab ilikuwa yenyewe ile orijino, tartiiiiib ya akina afro shirazi unapata maneno matamu huku umetulia na kikoi chako unashushia na kahawa na kashata. Lakini siku hizi ndio vidole juu mipasho na kupigana vijembe. Imeondolewa maana kabisa.
P.S. Na niliwahi kuomba before anayejua wapi naweza kupata nyimbo za Afro Shirazi Youth naombeni nipate kuzisikiliza........
Nawakilisha.
 
jamani nauliza,nasikia nyimbo za taarab ni matusi matupu,na inaitaji mtu wa mwambao au aliyebobea pwani kuzielewa,eti ile nyimbo ;pakacha hilo labeba kila kitu;ya juma balo,anamuimba shakila,eti ana sifa ya kubebe kilakitu,alaafu kwa majibu shakila akaja na wimbo;bunduki hiyo haina risasi;akiashiria kwamba juma b,mambo yapo lakini hayafanyi kazi,maana hizi ni kweli au watoto wa mjini wanaongezea utashi?
 
Tuwaenzi Viongozi wa Taifa letu

1) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP)
Mwanzilishi wa Taifa letu, alituunganisha Watanzania wote tukawa wamoja, sasa watanzania wengi hatuitani kwa makabila yetu bali tunaitana kwa utaifa wetu.
Aliwezesha Watanzania wote kuishi kwa Haki na Amani
Sisi Watanzania tulimpenda sana lakini Muumba wake/wetu alimpenda zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen

2) Mh. Alhaji Alli Hassan Mwinyi
Rais wa awamu ya pili wa Taifa letu.
Alipokea nchi ikiwa imedidimia kiuchumi.
Alikubaliana na masharti ya Shirika la fedha duniani pamoja na Benk ya Dunia.
Alituwezesha Watanzania Wengi (tusiokuwa na kitu) tukawa na fedha mfukoni.
Baadhi ya Wananchi waliacha kazi Serikalini, wakawa wafanya biashara, maana ilionekana kuwa kazi za serikalini hazina mshahara wa kutosha maisha ya leo.
Alituanzishia "Ruksa".
Aliendeleza utawala wa Haki na Amani.

3) Mh. Benjamen William Mkapa
Rais wa Awamu ya tatu ya Taifa letu.
Aliwezesha "Wasomi" kutambulika.
Aliwezesha Wasomi wengi kupata kazi
Aliwezesha Uchumi kukua hadi 9%
Aliwezesha Watanzania kutambulika nje ya nchi.
Aliendeleza Utawala wa Haki na Amani.

4) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wetu wa Awamu ya Nne ambayo ipo madarakani
Anaendeleza Utawala wa Haki na Amani
Ni Rais makini kuliko wote Afrika
Ni Rais anayewezesha Uchumi wa Nchi yetu kukua kwa kasi.
Ninamuomba Mungu amjalie ili atuongoze hadi mwaka 2015.
 
Mnaukumbuka ule wimbo wa Msondo Ngoma Sakina

Saki i i Sakina, tulia dada nikueleze,
nimepata barua kutoka nyumbani
inayoeleza umepata mchumba
tafadhali Sakina....fanya haraka

Kibwagizo

Naukamuoe huyo kijana, dada Sakina, usimkatea,
umezoea kukataa wachumba, olewa dada
ulimwengu wa kisasa una matatizo

Kama kuna mmoja wenu mwenye huu wimbo na nyingine za nyakati hizo naomba!

Nafikiri kama nakumbuka vizuri huu wimbo ulitolewa pamoja na wimbo wa "Kaka Selemani", mkuu ninahitaji kama wiki moja kujua uko kwenye CD ipi anyways, ninataku-PM.
 
Tuwaenzi Viongozi wa Taifa letu

1) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP)
Mwanzilishi wa Taifa letu, alituunganisha Watanzania wote tukawa wamoja, sasa watanzania wengi hatuitani kwa makabila yetu bali tunaitana kwa utaifa wetu.
Aliwezesha Watanzania wote kuishi kwa Haki na Amani
Sisi Watanzania tulimpenda sana lakini Muumba wake/wetu alimpenda zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen

2) Mh. Alhaji Alli Hassan Mwinyi
Rais wa awamu ya pili wa Taifa letu.
Alipokea nchi ikiwa imedidimia kiuchumi.
Alikubaliana na masharti ya Shirika la fedha duniani pamoja na Benk ya Dunia.
Alituwezesha Watanzania Wengi (tusiokuwa na kitu) tukawa na fedha mfukoni.
Baadhi ya Wananchi waliacha kazi Serikalini, wakawa wafanya biashara, maana ilionekana kuwa kazi za serikalini hazina mshahara wa kutosha maisha ya leo.
Alituanzishia "Ruksa".
Aliendeleza utawala wa Haki na Amani.

3) Mh. Benjamen William Mkapa
Rais wa Awamu ya tatu ya Taifa letu.
Aliwezesha "Wasomi" kutambulika.
Aliwezesha Wasomi wengi kupata kazi
Aliwezesha Uchumi kukua hadi 9%
Aliwezesha Watanzania kutambulika nje ya nchi.
Aliendeleza Utawala wa Haki na Amani.

4) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wetu wa Awamu ya Nne ambayo ipo madarakani
Anaendeleza Utawala wa Haki na Amani
Ni Rais makini kuliko wote Afrika
Ni Rais anayewezesha Uchumi wa Nchi yetu kukua kwa kasi.
Ninamuomba Mungu amjalie ili atuongoze hadi mwaka 2015.

Mengine ni yako! Usije tulisha sumu!
 
sasa katika hawa maraisi wanne,umesahau kutwambia nani ndio aliowapa wahindi nchi yetu? tunaomba jibu tafadhali
 
sasa katika hawa maraisi wanne,umesahau kutwambia nani ndio aliowapa wahindi nchi yetu? tunaomba jibu tafadhali

Ndio maana wengine hatukutaka hata kuigusa maana tulidhani labda ni April Fool!
 
Tuwaenzi Viongozi wa Taifa letu

1) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP)
Mwanzilishi wa Taifa letu, alituunganisha Watanzania wote tukawa wamoja, sasa watanzania wengi hatuitani kwa makabila yetu bali tunaitana kwa utaifa wetu.
Aliwezesha Watanzania wote kuishi kwa Haki na Amani
Sisi Watanzania tulimpenda sana lakini Muumba wake/wetu alimpenda zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen

2) Mh. Alhaji Alli Hassan Mwinyi
Rais wa awamu ya pili wa Taifa letu.
Alipokea nchi ikiwa imedidimia kiuchumi.
Alikubaliana na masharti ya Shirika la fedha duniani pamoja na Benk ya Dunia.
Alituwezesha Watanzania Wengi (tusiokuwa na kitu) tukawa na fedha mfukoni.
Baadhi ya Wananchi waliacha kazi Serikalini, wakawa wafanya biashara, maana ilionekana kuwa kazi za serikalini hazina mshahara wa kutosha maisha ya leo.
Alituanzishia "Ruksa".
Aliendeleza utawala wa Haki na Amani.

3) Mh. Benjamen William Mkapa
Rais wa Awamu ya tatu ya Taifa letu.
Aliwezesha "Wasomi" kutambulika.
Aliwezesha Wasomi wengi kupata kazi
Aliwezesha Uchumi kukua hadi 9%
Aliwezesha Watanzania kutambulika nje ya nchi.
Aliendeleza Utawala wa Haki na Amani.

4) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wetu wa Awamu ya Nne ambayo ipo madarakani
Anaendeleza Utawala wa Haki na Amani
Ni Rais makini kuliko wote Afrika
Ni Rais anayewezesha Uchumi wa Nchi yetu kukua kwa kasi.
Ninamuomba Mungu amjalie ili atuongoze hadi mwaka 2015.

LADISLAUS NI SENIOR MEMBER WA JF.HONGERA KWA UCHAMBUZI WAKO "MAKINI".JF INOGILE.Mhhhhh!!!
 
4) Mh. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wetu wa Awamu ya Nne ambayo ipo madarakani
Anaendeleza Utawala wa Haki na Amani
Ni Rais makini kuliko wote Afrika
Ni Rais anayewezesha Uchumi wa Nchi yetu kukua kwa kasi.
Ninamuomba Mungu amjalie ili atuongoze hadi mwaka 2015
.
[/QUOTE]

isije ikawa wewe mwenyewe ndio Kikwete unajipigia kampeni; nyoo, sifa zote hizo, hata ubalozi wa nyumba kumi mtaani kwetu hatumpi. Ptu..ptu..

unatania au...uko serious??

waberoya
 
..Yussuf Bana, Zamoyoni Mogela, katikati ni MUHIDIN CHEUPE wa Yanga.
Muhidini Cheupe "Nylon" baadaye alikwenda NDOVU ya Arusha iliyosumbua sana na akina Charles Mngodo,Mohamed Bob Chopa wakiungana Zamoyoni Mogella,Hamis Thobias Gaga " Gagarino" na James kisaka wakitokea Volkano ya Kenya.
 
...hiyoo ndio NDOVU ya arusha bwana ...chama kubwa...

...james kisaka..

...simon "kishoka"...aka "uruguay"

...lila shomari..

..mwanga luheya...

hamis thobious gaga "gaga-gagarhino"

mohamed "bob" chopa..

..mohamed mateneke "speed"

charles mngodo....

..ACHANENI NA HIYO LIST WAZEEE...ongezeeni mnaokumbuka..!!!
 
Ndugu zao huku Dar yaani PILSNER ya akina:
1.James Washokera
2.Charles Msami
3.Issack Mwakatika
4.Lindimu Muba "Charlton"
5."Zico wa Kilosa" Said Mrisho wakati huo ametokea Yanga
6.Kocha wao Silersaid Mziray
 
Sana kabisa mkuu, nakupa tano kwa hilo. Na kila mtu eti anaimba taarabu siku hizi, sio kuwadhalilisha watu wa kutoka sehemu nyingine ila tu mambo mengi huwa yanakuwa na asili zake. Huwezi kumkuta msandawe akicheza mdumange; na vilevile sitaji kabila lakini utakuta nayeye anaimba taarabu. Taarab ilikuwa yenyewe ile orijino, tartiiiiib ya akina afro shirazi unapata maneno matamu huku umetulia na kikoi chako unashushia na kahawa na kashata. Lakini siku hizi ndio vidole juu mipasho na kupigana vijembe. Imeondolewa maana kabisa.
P.S. Na niliwahi kuomba before anayejua wapi naweza kupata nyimbo za Afro Shirazi Youth naombeni nipate kuzisikiliza........
Nawakilisha.

Muheshimiwa sana na Taarab za Bara zipo pia! Umesahau 'Nkurukumbi'? Nenda Bujumbura hadi leo Taarab haina mpinzani! Nani wa kufananishwa na yule Mama wa Kigogo Elizabeth Sijila wa JKT aliyeimba, 'Manahodha wa Mashua kwa nini wakae nyuma?' Nasi wa Bara twajua namna ya kula chapati ati.

BTW: Hivi Wahaya wanavyovaa Kanzu siku ya Harusi huwa wanamaanisha nini? Na asili ya vazi hili walilitoa wapi?
 
Mengine ni yako! Usije tulisha sumu!

Mi mwenzio niko Mochuari naelekea Golgota! Watu wengine wanajifunza kutumia Kibodi kupitia JF nadhani! Phew!! Kama yote yaliyoandikwa hapo juu ni kutafuta UPENDO tu basi wacha niendelee kuwa na CHUKI kuliko kujiabisha.
 
Muhidini Cheupe "Nylon" baadaye alikwenda NDOVU ya Arusha iliyosumbua sana na akina Charles Mngodo,Mohamed Bob Chopa wakiungana Zamoyoni Mogella,Hamis Thobias Gaga " Gagarino" na James kisaka wakitokea Volkano ya Kenya.

Wote uliowataja ni sawa lakini Zamoyoni hajawahi kuchezea Ndovu ya Arusha, alipotoka Kenya alikwenda Uarabuni baadaye akarudi Simba na ndipo akaenda kumalizia mpira wake kule Jangwani kwa 'vijisenti' vya Gulamali.

Mogella ni miongoni mwa wachezaji wachache wa miaka hiyo wasio na elimu waliongalia mbele. Pamoja na mpira wa wakati ule mchezaji uliishiwa 'kusifiwa' yeye alitengeneza future yake. Ukiacha wachezaji wachache wenye elimu kama Tenga, Mtemi, Mwalusako, Gumbo na wachache wengine ambao wako au waliendelea kuwa kwenye ajira. Hivi mlishawahi kukutana na Jellah Mtagwa hivi karibuni? Kumbuka huyu ni mchezaji pekee ambaye picha yake iliwahi kuwekwa kwenye stamp. Hivi mmewahi kumuona Hussein Ngulungu hivi karibuni? Nani alikuwa kama Ngulungu pale Pan African, nasikia ni mlinzi wa Godown ya Mohamed Enterprises pale Morogoro. Ukimuona Peter Tino na mdogo wake Gebo pale Kariakoo utawasikitikia. Wale wenye elimu angalau ya kidato cha nne, Tenga amekuwa akijaribu kuwatumia pale TFF kama kuwa makamishna wa Mechi mbali mbali na kamati za ufundi au kufuatilia matukio. Ukienda pale TFF Karume utawakuta wamepanga foleni wakitaka kumuona Tenga, sasa sijui wote hao atawapeleka wapi?

Nenda Leaders Club siku za Jumamosi utawakuta wamejaa tele, kazi 'kubom' Safari Baridi. Nawashukuru sana TBC, ITV na Star TV angalau wamekuwa wakiwachukua kuwa makomenteta wa mechi mbali mbali zinazoonyeshwa na vituo hivyo. I hope huwa wanalipwa kidogo. Maana hii Bongo we iache tu! Kuonekana kwenye kioo ni 'ujiko' so sitashangaa nikisikia malipo huwa ni kuonekana kwenye Luninga tu! Ila sasa sio kila mchezaji anaweza kuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira, juzi TBC walimleta Dotto Ruta Mokili, nikajiuliza huyu jamaa wamemuokota wapi? Bulyaga au Imasco? Maana alikuwa hajui hata anachokisema sembuse anachotuambia!
 
Back
Top Bottom