Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


Sikonge,

Alikuwa ni Peter Enahoro au Ralph Uwechue wakiwa New African au Africa Now waliandika makala moja miaka ya 80 iliyokuwa ikisema "100 days that made Tanzania"!

Hii stori ya CIA na Warusi si ya kuzusha ni ya kweli na nafikiri nyaraka za CIA ambazo zilikuwa classified, zimefunguliwa na zinatamka wazi ni jinsi gani walisukuma Tanganyika au Kenya waungane na Zanzibar.

Sasa kwa mkao wa Pan-Africanism na One Afrika, nafikiri hii ilikuwa opportunity nzuri kwa Mwalimu katika zile njozi zake za Afrika moja. Labda ushawishi wa Marekani kwa Karume, ulimrahisishia kazi Nyerere ambaye aliona opportunity ya kuonyesha umma na dunia kuwa Afrika moja inawezekana.

Kuna haja kubwa sana ya kupata hizo de-classified nyaraka za CIA na ziwekwe hadharani ili tuachane na udanganyifu wa wanasiasa wetu na tuamue kwa mazingira ya sasa kama tunataka muungano au la!
 

Kwenye Picha: Salim, Graca,Mama Maria, Butiku,Jumbe,Mwalimu na Samora.

Jumbe
 
Nakumbuka sana somo letu la siasa shule ya msingi...eti siku hizi wanaliita 'uraia' sijui....
 
mkuu kichuguu,

hapo msaaada, najua kuna mwalimu, mkapa lakini huyu wa pembeni amefanana na pinda ila sijui ni nani mkuu weka msaaada!

hahaaaaaaaaaaaaa, yaani zama hizo pinda alikuwemo naye? Au ndio duniani wawiliwawili, kumbe mshikaji tangu ujanani alikuwa serious
 
Thread hii inatuliza sana ubongo kama ile ya Icadon ya walinzi wa viongozi. Ni watu kama "Mwiba" ndio wanaojaribu kuvuruga mtiririko huu muhimu wa kihistoria. Kumbe hati ya Muungano wetu ilifikishwa hadi BUNGENI? Zanzibar wakati huo hawakuwa na Baraza la Wawakilishi hadi 1980.
 

Mkuu Bob,

Haya maneno yako ni mazito sana na yanaongeza nguvu sana katika kujaribu kupata picha kamili ya wapi matatizo ya muungano wetu yalipoanzia, mpaka kutufikisha hapa tulipo.

Ahsante Mkuu.
 
hivi huyu sokoine,amepata kila aina ya wasifa,was he that effective,au by virtual of his life being cut short in mitigating curcumstances,ndiyo iliyomuelevate to a cult status.
Nimesoma somewhere in the capitalist press,kwamba KAMBONA was the good president that tanzania never had. i take this to mean had kambona become a president in the roaring 60's or 70's tanzania could not have been in the rot it currently finds itself in - hii argument does it really hold water au
 
Mwenyezi Mungu azidi kuziweka roho ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere & Moringe Sokoine Mahali pema peponi. Amina.....

Asanteni mliotuwekea picha hizi kutuliwaza, i feel like crying!
 

Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.

Mwiba,hio signature yako really sums it all up soo nicely......
 
cheki pete hilo wakati huwo mwalimu alikuwa na kaufisadi.
 
Son of A,
Don't believe everything you read in the capitalist press. Wakianza kukusifia ujue kuna kitu hapo. Mwalimu aliwadisappoint by going east. Jiulize ni kwa nini walimwuua Lumumba na kumjenga Mobutu?
 


Derek Bryson

Picha ya juu hapo ni Idi Amin alikuwa akitowa hotuba na kuna kitu kilimchekesha mwalimu pale...Labda mzee Malecela anaweza kutuambia ni kiti gani mwalimu alikuwa akisema hapo wakati wa hotuba ya hasimu wake mkuu....Kwasababu hata sura yake inaonuesha kama kicheko flani hivi cha kiubezaji...
 
Kichuguu, Jasusi, FMES, Rev. Kishoka, Son of Alaska,

..hii thread nimeipitia na kila kumbukumbu tunayoletewa ni ya WANASIASA tu.

..kulikuwa na thread nyingine ambapo member walijaribu ku-list idols/mashujaa wao, basi huko nako kulijaa wanasiasa.

..hivi katika jamii yetu hakuna watu wengine wa kuwaenzi zaidi ya wanasiasa? hakuna madaktari, ma-injinia, bankers, wachumi, industrialists, wanasheria, mathematicians,physicists,biologists,...ambao tunaweza kuwaenzi kwa utumishi na michango yao?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…