Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kichuguu,Jasusi,FMES,Rev.Kishoka,son-of-alaska,
..hii thread nimeipitia na kila kumbukumbu tunayoletewa ni ya WANASIASA tu.
..kulikuwa na thread nyingine ambapo member walijaribu ku-list idols/mashujaa wao, basi huko nako kulijaa wanasiasa.
..hivi katika jamii yetu hakuna watu wengine wa kuwaenzi zaidi ya wanasiasa? hakuna madaktari, ma-injinia, bankers, wachumi, industrialists, wanasheria, mathematicians,physicists,biologists,...ambao tunaweza kuwaenzi kwa utumishi na michango yao?
Picha ya juu hapo ni Idi Amin alikuwa akitowa hotuba na kuna kitu kilimchekesha mwalimu pale...Labda mzee Malecela anaweza kutuambia ni kiti gani mwalimu alikuwa akisema hapo wakati wa hotuba ya hasimu wake mkuu....Kwasababu hata sura yake inaonuesha kama kicheko flani hivi cha kiubezaji...
Nyani Ngabu,
..nadhani hatuheshimu tu michango ya wataalamu wetu ndiyo maana unafikiri hatuna wa kuwaenzi.
..kwani hao wanasiasa tunaowaenzi na kuwatukuza wamefanya nini cha maana?
NB:
..on the other hand, if i could agree with you, tufanye nini kama taifa ili kuwa na wataalamu wa uhakika watakaoenziwa na wenetu na wajukuu zetu?
Kweli ni vizuri kukumbuka tuliotoka
Nyani Ngabu,
..nadhani hatuheshimu tu michango ya wataalamu wetu ndiyo maana unafikiri hatuna wa kuwaenzi.
..kwani hao wanasiasa tunaowaenzi na kuwatukuza wamefanya nini cha maana?
Jasusi,
..it is almost half a century tangu tupate uhuru.
..what happened kipindi chote hicho hatuna la kusifia kwa wanataaluma wa kitanzania?
NB:
..on the other hand, if i could agree with you, tufanye nini kama taifa ili kuwa na wataalamu wa uhakika watakaoenziwa na wenetu na wajukuu zetu?
..hivi katika jamii yetu hakuna watu wengine wa kuwaenzi zaidi ya wanasiasa? hakuna madaktari, ma-injinia, bankers, wachumi, industrialists, wanasheria, mathematicians,physicists,biologists,...ambao tunaweza kuwaenzi kwa utumishi na michango yao?
Wanasiasa wanaoenziwa hakuna chochote cha maana walichokifanya zaidi ya kuongoza juhudi za kugombea uhuru. Hatuna wataalamu wa maana ktk hizo fani zote ulizozitaja. Tungekuwa nao tungekuwa tumeendelea. Ngoja nikuulize, hivi kuna mtaalam gani wa maana ktk uchumi ambaye angeendelea kukumbatia sera ya ujamaa na kujitegemea huku akiona kuwa haifanyi kazi? Hao ma injinia unaotaka tuwaenzi wameshindwa hata kutatua matatizo ya kilimo, umeme, maji masafi, n.k. Sasa tuwaenzi kwa kitu gani? Watu bado wanaugua magonjwa kama ya kichocho, utapiamlo, kisonono, na mengine mengi tu. Hao wataalamu wa afya na tiba wamefanya nini kuangamiza magonjwa kama hayo yanayoweza kuangamizwa? Jibu ni hakuna!! Sasa tuwaenzi wataalamu wa fani ulizotaja kwa minajili ipi?
Doctors: Mwaisela - Alileta mapinduzi katika sekta ya afya ya kikoloni
Economist/Industrialist: Rweyemamu - alianzisha Kituo cha Ubunifu cha IPI
Mathematicians: Shayo - alianzisha Kijiji cha Teknolojia
Physicst: Njau - alivumbua njia mbadala ya kutabiri hali ya hewa
Biologist: Mshigeni -alivumbua aina fulani ya mimea
Bankers: Msuya - alianzisha benki maarufu ya watu wa Mwanga
Lawyers: Nyalali- aliongoza tume iliyoyeta mabadiliko ya kisiasa nchini
Engineers: Kinjeketile - alivumbua mtambo wa kugeuza risasi kuwa maji
Dah,Doctors: Mwaisela - Alileta mapinduzi katika sekta ya afya ya kikoloni
Economist/Industrialist: Rweyemamu - alianzisha Kituo cha Ubunifu cha IPI
Mathematicians: Shayo - alianzisha Kijiji cha Teknolojia
Physicst: Njau - alivumbua njia mbadala ya kutabiri hali ya hewa
Biologist: Mshigeni -alivumbua aina fulani ya mimea
Bankers: Msuya - alianzisha benki maarufu ya watu wa Mwanga
Lawyers: Nyalali- aliongoza tume iliyoyeta mabadiliko ya kisiasa nchini
Engineers: Kinjeketile - alivumbua mtambo wa kugeuza risasi kuwa maji
HII NI KATI YA THREADS ZINAZOONGOZA....! bravoooooo.......!
Nyani Ngabu,
..umezungumza ya msingi kabisa. kwa kiasi kikubwa tuko pamoja.siamini kama wataalamu wote wa uchumi waliunga mkono hata mambo yalipokuwa yanaenda kombo. i would like to hear about DISENTERS waliopinga uendeshwaji mbaya wa uchumi wetu.
..labda nitoe mifano michache midogo tu:
..kuna kipindi Tanzania tulikuwa tunaongoza ktk literacy kwa nchi changa. sasa mtaalamu aliyeandaa na kusimamia elimu ya watu wazima kipindi hicho definetely ana mchango mkubwa kwa Taifa kuliko hawa wanasiasa tunaowasifia kila kitu.
..pia nchi yetu iliwamiwa na Iddi Amini wa Uganda. siyo kwamba tulikomboa ardhi yetu tu, bali tulimuondoa Amini, tukaweka serikali ya mpito, tukaandaa na kuendesha uchaguzi Uganda, tuka-train polisi na jeshi, na kuondoka kwa heshima zote. hivi hakuna makamanda na wapiganaji wanaopaswa kuenziwa hapa, tuna-list wanasiasa waliofeli tu.
NB:
..ndiyo maana sasa hivi vijana wanamaliza chuo kikuu moja kwa moja wanataka kujiingiza kwenye siasa.
..ukienda mashuleni hatuna watoto wanao-dream kuwa waalimu.
..nadhani kinachoendelea hapa ni matokeo ya propaganda za muda mrefu za wanasiasa kwamba they were doing something for the country, lakini leo hii hamna cha kuonyesha.
Mkuu Icadon,
Heshima mbele bro, duh tuendelee kuweka vitu hapa maana so far tunakula elimu safi na ya bure, Ashante sana mkuu,
Mkuu Jasusi,
Please, acha kupoteza muda wako, maana ukiona bin-adam anapigana na picha zisizosema, basi utajua ni kwa nini tuna matatizo kwenye muungano! Sio kwamba hatujamuona na hiyo crying yake for attention, ila tumemdharau,
Najua kuwa unazo picha nyingi za kumbu kumbu, please weka picha hapa achana na kelele za mlango!
Mkuu Invisible,
Ahsante kwa marekebisho naomba uipitie hii topic mara kwa mara kurekebisha picha na maneno yasiyokuwa sawia kuambatana na hizi picha, za viongozi wetu mashuhuri waliotuwekea msingi wa taifa hili, ambalo some of us we are proud citizens wake.