Mwanzilishi FMES na wachangiaji wengine wote. Thread hii imneivutia sana kwa kutukumbusha tulikotoka. Ngoja sasa niwageuzie upande wa mpira wa Miguu. Kwa bahati mbaya wachezaji wengi siwafahamu kwa vile tulizowea kukariri majina zaidi wakati huo. Anayejua majina asaidie kutukumbusha.
Hii ni Timu ya African Sports ya Tanga mwaka 1974: Waliopo ni pamoja na kipa Omar Mahadhi, Mwabuda, Sharif, Abdallah Luo(mrefu) Hemedi Seif, Omar Zimbwe, Zacharia Kinanda
Na hii ni Coastal Union ya Tanga mwaka huo huo wa 1974. Waliopo ni pamoja na Salim Amri, Jalala, Omar Bafadhili, Mohamed Salim.
Hii ni timu ya yanga wakiwa ziarani Brazil mwaka huo huo wa 1974; waliopo ni pamoja na Bona Max, Maulid Dilunga, Michael Clement, Moshi Dayan na Gibson Sembuli, Leodgar Tenga, Athumani Kilambo, Elias Michael, Said Sanga, Abdulrahman Juma na Omar Kapera. Nadhani kuwa sunday Manara alikuwa keshaenda Austria kucheza kandanda ya kulipwa wakati huo.
Sikuweza kupata picha za Simba na Cosmo wakati huo. Nadhani timu za Red Devils na Pan African zilikuwa hazijaanzishwa mwaka huo wa 1974.