Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Ikarus Kumba Kumba, yalikuwa ni kutoka Hungary, mkuu ahsante sana kwa hii historia, ubarikiwe!
 
Huyu mzee ni alikuwa mtanzania wa kwanza kuwapanda mlima kilimanjaro hapa akiwa na Chifu Lemne wa Uchagani
 
Mkuu Mchongoma,

...4. Nilipata nafasi ya kumuaga kwenye maombolezo, baada ya kutangulia kwake kwenye haki, na ameacha watoto imara sana na ninaamini kuwa mmoja wao atabeba tochi ya njia siasa, na Mungu amuweke mahali pema peponi.

A True African Hero!

...Yes Indeed!

Mkuu, huyu ni baba yao mzazi kina Tasi na Bosi Chiume? Nawakumbukia hawa jamaa enzi hizo mitaa ya Upanga. Sijui ndio hao unaowazungumzia? Great Guys.
 
1. Ohhh yah, siku hizi mkulu Tass yuko UN, Darfour halafu nadhani unakumbuka enzi zile jinsi alivyokuwa bingwa Breakdance, hasa Msasani Beach (JPP & Choggy),

2. Mkulu Boss siku hizi majuzi juzi alikuwa pale Tanzania Investment, ni msomi aliyeboeba na mambo ya uchumi, alishaanza kusifika sana pale lakini kumbe napo pia kuna another Nchimbi's like, kama kawaiada yakaaanza majungu kwanza sasa ikawa inakaribia the whole deal,

- Wananchi wenye nia njema na taifa na wakamuwahi na kumsihi atoke pale kabala hajafa au kwenda jela, bila makosa what a waste kwa taifa?

Sasa mkulu ni Consultant!
 
Mkuu huyu balozi, ninajua kuwa alikuwa na mtoto wake mmoja aliyekuwa ofisa wa ubalozi wetu pale Brussells, in the early 90s,

sikujua kuwa baba yake aliwahi kuwa balozi, duh ahsante kwa hiki kipande, nitazitafuta habari za baba yake leo.
[/QUOTE

FMES,

Mtoto wake unayemsema hivi sasa ni afisa wetu wa ubalozi Ottawa, Canada.
 
Ikarus Kumba Kumba, yalikuwa ni kutoka Hungary, mkuu ahsante sana kwa hii historia, ubarikiwe!

Yap, FMes,
Na si tu kuwa YALIKUWA yanatoka ila ni kuwa YANATOKA. Hiki kiwanda hadi leo bado kipo na wanatesa na mabasi yao hadi leo Ulaya. Nilishawahi kuona ki-BUS chao Sweden. Nilishangaa kuwa hadi kinanipita sisikii sauti ya injini zaidi ya mairi du na ndipo nikajua kuwa ni mabasi yanayotumia GAS. Nilikuwa nafikiri kuwa kwa kuwa Tanzania tuna GAS basi ungelifanyika mpango tena kununua mabasi kwa hawa jamaa. Hayana kelele, hamna CO2 na takataka nyingine. Ila nasikia hata kununua hizo Kumbakumba jamaa aliyenunua na yeye ghafla akawa na mabasi sijui mawili ya Ikarus? Hizi 10% zimeanza siku nyingi? Ila siku hizi hata TARISHI anafahamu na anataka. Hebu angalieni hapa wengine wanaotumia mabasi ya GAS. http://en.wikipedia.org/wiki/Ikarus_Bus
 
Ule mpango wa RAPID BUS kwa mji wa Dar, hii kitu ingelifaa pia. Hasa kama kunafanyika mpango kuwa Injini zitoke kwao na baadhi ya vitu. Asembling na baadhi ya vitu vitoke Tanzania ili na sisi tupete AJIRA kidogo. Wao wanafaidika na sisi tunafaidika. Kama kuna vituo vya GAS basi hata miji ya karibu na Dar inaweza kuwa inatumia mabasi ya GAS.
-----------------------------------------------------------------------------

In 2002, Ikarus placed the Natural Gas (CNG) 18 meter articulated bus in Colombia, which is currently in operation in Transmilenio Rapid Bus Mass Transit System in the Capital City of Bogota. The company has come out in 2007 with a new low-floor model which they plan to produce in Hungary (200-400 per year), Russia (1000-2000 per year) and China (10,000 per year).

In 2006, Mr. Gary Urteaga, a business entrepreneur from Peru, initiated a project with Ikarus to penetrate the Latin American Market. The Project involves the supply of Natural Gas (CNG) Buses of 8 meters, 12 meters and articulated 18 meters together with the investment in Bus Assembly Plants for the Latin American region. Offers have been made to bidders of the Metropolitano Rapid Bus Transit System of the City of Lima in Peru which is to awarded in 2007 and implemented in 2008-2009. Also, the Government of Venezuela has initiated dialogue with Ikarus derived from the strong interest in the market for Natural Gas Buses shown by President Hugo Chavez Frias.
 
Ila nasikia hata kununua hizo Kumbakumba jamaa aliyenunua na yeye ghafla akawa na mabasi sijui mawili ya Ikarus? Hizi 10% zimeanza siku nyingi? Ila siku hizi hata TARISHI anafahamu na anataka.

Mkuu ni kweli, yule jamaa liyeenda kuyaleta alipatiwa mabasi mawili nusu sio marefu kama haya, lakini ninaamini kuwa enzi zile ilikuwa ni procedure za viwanda vingi na makampuni makubwa sana huko majuu, haikuwa rushwa wala hongo,

ninakumbuka hata yale mabasi yalipokuja kuna waliotaka kumletea noma kwenye kipindi cha Radio kama unakikumbuka cha Mikingamo, lakini in the end wakaishia kumuachia mabasi yake,

However, mimi ninaheshimu sana one thing kwamba nenda pamoja na waliokuwa wanachukua 10%, angalau kulikuwa na something to show kwa wananchi na taifa, lakini siku hizi hawa wanakula mpaka mbegu bwana!

Aaahggggrrr hawafai kabisa hawa wa sasa!
 
Nasikia na Mrema pia alihusika na ile operation, au?
Sina hakika sana na Mrema, lakini Marando?....ndiye mwenyewe. Hadi mama yake mzazi Mohamed Tamim anafariki in early 2000s, alikuwa so proud to her son for that. Alikuwa tayari kumweleza yeyote atakayesikiliza stori ya mwanawe, tokea anapewa last warning na mwanawe kuwa asikilize redio within following weeks, hadi alipopelekwa mochwari Muhimbili kuutambua mwili wa mtoto wake. Lakini wapi hakukuwa na mwandishi yeyote aliyejaribu kumuinterview kwa stori hiyo. Ni alikuwa bibi mmoja mcheshi mno pale Tanga mjini. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Aaaamin!!
 
Mwanzange said:
Sina hakika sana na Mrema, lakini Marando?....ndiye mwenyewe. Hadi mama yake mzazi Mohamed Tamim anafariki in early 2000s, alikuwa so proud to her son for that. Alikuwa tayari kumweleza yeyote atakayesikiliza stori ya mwanawe, tokea anapewa last warning na mwanawe kuwa asikilize redio within following weeks, hadi alipopelekwa mochwari Muhimbili kuutambua mwili wa mtoto wake. Lakini wapi hakukuwa na mwandishi yeyote aliyejaribu kumuinterview kwa stori hiyo. Ni alikuwa bibi mmoja mcheshi mno pale Tanga mjini. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Aaaamin!!

wana jamboForums,

..nadhani suala la kukamatwa Tamimu lilikuwa ni secret-operation na nadhani siyo vizuri kuwataja kwa majina wale waliohusika.

..naamini Afisa Usalama yeyote aliyehusika katika operation hiyo alikuwa mtu wa chini sana na alikuwa akitekeleza amri na maagizo ya wakubwa wake wa kazi.

..tukirudi kwenye hili jaribio la kutaka kumpindua Baba wa Taifa, nadhani alitumia busara kuachia ngazi mwaka 85.

..laiti kama timu ya Mwalimu na Sokoine ingeendelea kutawala nchi ile, wakiendeleza sera zao za maduka ya kaya, uhujumu uchumi, kufunga mikanda, hakuna fedha za kigeni, bidhaa adimu, etc etc, naamini kabisa within 3 yrs wangeondoshwa madarakani kwa nguvu.

..kuna minong'ono kwamba nchi wafadhili ndizo zilizomlazimisha Baba wa Taifa kuachia hatamu za uongozi.
 
Mindhali tunakumbuka historia ya nchi yetu basi na mabaya nayo tuyakumbuke

Mfano ni MAUAJI YA MWEMBECHAI
 
Hivi kwa nini tulikuwa na kipindi cha Mikingamo? Maana kilikuwa ni kipindi cha Unoko eti kupiga vita walanguzi, lakinindicho kilichotumika kujenga chuki na kuanzisha matabaka ya uchumi ambayo yako sasa hivi.

It was funny to hear stories being reported on radio!
 
Mkuu ni kweli, yule jamaa liyeenda kuyaleta alipatiwa mabasi mawili nusu sio marefu kama haya, lakini ninaamini kuwa enzi zile ilikuwa ni procedure za viwanda vingi na makampuni makubwa sana huko majuu, haikuwa rushwa wala hongo,

ninakumbuka hata yale mabasi yalipokuja kuna waliotaka kumletea noma kwenye kipindi cha Radio kama unakikumbuka cha Mikingamo, lakini in the end wakaishia kumuachia mabasi yake,

However, mimi ninaheshimu sana one thing kwamba nenda pamoja na waliokuwa wanachukua 10%, angalau kulikuwa na something to show kwa wananchi na taifa, lakini siku hizi hawa wanakula mpaka mbegu bwana!

Aaahggggrrr hawafai kabisa hawa wa sasa!


Mabasi yale yalinunuliwa na bwana mmoja nadhani aliyekuwa meneja wa UDA akijulikana kwa jina la Mahimbo katikati ya miaka ya sabini, nadhani kati ya mwaka 1975 na mwaka 1976 hivi baada ya yale mabasi ya ghorofa ya DMT kuishia. Wakati huo kipindi cha mikingamo kilikuwa hakijaanza, hiki kilikuja mwanzoni mwa miaka ya themanini hivi, nadhani mwaka 1982 au 1983.

Mabasi aliyopewa bwana Mahimbo yalichukuliwa na UDA kwa sababu mbili: Kwanza alifanya makosa kuyaacha yakaletwa yakiwa na rangi (nadhani pamoja na nembo) ya UDA. Pili serikali ilisema kuwa mabasi hayo yalitolewa na kiwanda cga Ikarus kama bakshishi kwa mteja wake, ambaye alikuwa ni UDA siyo Mahimbo; yeye alikuwa ameiwakilisha UDA kama mtumishi wake tu.
 
Ila nasikia hata kununua hizo Kumbakumba jamaa aliyenunua na yeye ghafla akawa na mabasi sijui mawili ya Ikarus? Hizi 10% zimeanza siku nyingi? Ila siku hizi hata TARISHI anafahamu na anataka.

..taratibu za utumishi wa umma zinaelekeza kwamba zawadi kama hiyo inapaswa kuwa-surrendered serikalini.

..kwa jinsi hali ilivyokuwa wakati ule siamini kama huyo meneja alithubutu kuyachukua mabasi hayo.

..tatizo kubwa lilikuwa ni "zawadi za wananchi" kwa viongozi wanapotembelea mikoani na wilayani.

..wananchi walikuwa wakilazimishwa kutoa zawadi kama mifugo na mazao kwa viongozi wa chama na serikali waliowatembelea.

..Mzee Mwinyi alikuja kuusitisha utamaduni huo ambao kwa kweli naona ulikuwa unyonyaji wa mchana kweupe.

NB:

..viongozi pia walikuwa na tabia ya kujichotea bidhaa za viwandani kila walipofanya ziara zilizokuwa zikiitwa "ziara za ukaguzi."
 
Mabasi aliyopewa bwana Mahimbo yalichukuliwa na UDA kwa sababu mbili: Kwanza alifanya makosa kuyaacha yakaletwe yakiwa na rangi nadhani pamoja na nembo ya UDA. Pili serikali ilisema kuwa mabasi hayo yalitolewa na Ikarus kama bakshishi kwa mteja wake, ambaye alikuwa ni UDA siyo Mahimbo; yeye alikuwa ameiwakilisha UDA tu.


Mkuu ninaamini kuwa huyo mkuu alikiri kutoweza kuyamudu yeye binafsi na hasa matengenezo yake, hivyo UDA wakampa hela zake na hata ma-Engineer wanne waliokwenda kuyasomea kwa miaka zaidi ya minne, ambao ndio waliorudi nayo mmoja wao alikuwa mshikaji wangu mmoja anaitwa John Hatia, ambaye sasa anamiliki karakana yake binafsi kubwa ya utengenezaji magari,

yupo karibu na Bar moja maarufu mjini inaitwa Hil-Tech, hawa nao pia walipewa basi moja moja, lakini na wao waliyauza kwa UDA, Mikingamo hakikuwa kipindi kilichokuwa kinajali time line wala facts, ilikuwa ni majungu, period!

Infact, hii ishu pia iliwahi kutokea hata kwenye treni za TAZARA, za mtu kupewa kichwa na behewa, TAZARA hakukuwa na mjadala, wao waliamua kumnyang'anya tu mkulu akanona bora sikose mali yake akaamua kukivizia usiku kule bandarini ili akichukue alipokamatwa ilikuwa ni the biggest joke of the century!
 
Kuna unafiki mkubwa mabao ulifanywa na Wanasiasa wa Tanzania waliokimbilia kuvunja Azimio la Arusha na kutuletea Azimio la Zanzibar.

Wao walikuwa wakifanya "ziara za ukaguzi' viwandani, mashirikani, mashambani, wilayani, mikoani, vijijini, mijini na kila walikopita walikomba "zawadi". Mafuta ya kupikia, mchele, unga wa ngano, mbuzi, kuku, sabuni, toilet paper, sahani, bia, soda, mvinyo, madaftari na kadhalika, huku wakiishi kwenye nyumba za Serikali bila kulipa umeme, simu, maji au wafanyakazi, wakiendehswa kwa magari ya Serikali na kupewa maderva na kujaza mafuta!

Hawa mishahara yao ilikuwa imetulia ikinona kama si kuungua kwenye lete kama tulivyo na moja baridi kama si kwenye tu-nyumba tudogodogo!
 
..taratibu za utumishi wa umma zinaelekeza kwamba zawadi kama hiyo inapaswa kuwa-surrendered serikalini.

..kwa jinsi hali ilivyokuwa wakati ule siamini kama huyo meneja alithubutu kuyachukua mabasi hayo.

..tatizo kubwa lilikuwa ni "zawadi za wananchi" kwa viongozi wanapotembelea mikoani na wilayani.

..wananchi walikuwa wakilazimishwa kutoa zawadi kama mifugo na mazao kwa viongozi wa chama na serikali waliowatembelea.

..Mzee Mwinyi alikuja kuusitisha utamaduni huo ambao kwa kweli naona ulikuwa unyonyaji wa mchana kweupe.

NB:

..viongozi pia walikuwa na tabia ya kujichotea bidhaa za viwandani kila walipofanya ziara zilizokuwa zikiitwa "ziara za ukaguzi."

Jokakuu,
Hii niliishuhudia kwetu huko Tabora. Kwanza kujenga uwanja wa mpira pale mjini tulichangishwa kila kitu. Ukienda kusaga mahindi, nauli ya mabasi, ukiuza kitu na michango ya lazima mingine. Uwanja kuisha eti ni wa CCM, khaaa!! Nyerere kajiuzulu tukachang'ishwa Ng'ombe kibao, mbuzi nk. Kawawa naye akafuata ..... Sasa akija mkulu fulani basi atapikiwa chakula, na kupewa MICHANGO ya maendeleo ya mkoa. Siku moja katika msafara huo alikuwemo dada yangu kwa baba mkubwa. Nikaja kusikia kuwa walipotoka tu kijijini, walifungua bahasha hilo. Hilo bahasha lilikabidhiwa na mzee mmoja aitwaye Mwana Fungameza. Huyu mzee alipiga Magoti kwa Wakulu hao wa umri wa Wanae na kuwakabidhi hilo bahasha huku watu wakipiga makofi. Kiliniudhi sana kitendo hicho hasa muda huo nilikuwa nimemaliza form4 na kaukorofi fulani kichwani. Zaidi kiliniuma kuwa BAHASHA hilo lilifunguliwa na wakagawana HELA zote zilizokuwa ndani hata kabla ya kufika mjini. Sasa sijui za ujenzi wa uwanja walikomba kiasi gani? Kujenga Makao makuu Dodoma huko ndiyo hata tusiseme.
 
1.
..taratibu za utumishi wa umma zinaelekeza kwamba zawadi kama hiyo inapaswa kuwa-surrendered serikalini...kwa jinsi hali ilivyokuwa wakati ule siamini kama huyo meneja alithubutu kuyachukua mabasi hayo.

sio kwamba huyu meneja alijaribu kuyachukua, isipokuwa huyu bwana alinyamaza kimyaa, ukweli ni kwamba yale mabasi sita yalikuja yakiwa na rangi ya Blue, kwa sababu mabasi yote yaliwekwa pale Ubungo, enzi zile ukiwa Mlimani Park au Hapa pembeni yaani kwenye Bendi ya Kyauri Voice, ulikuwa unayaona yote yakiwa pale,

Kuna watu ndani ya UDA walioona wivu na kumaua kuyapaka rangi haraka haraka, lakini Manager wa UDA then simjui alikuwa ni nani, lakini najua kuwa he was a very fair man, kwani nilikuwa na washikaji waliokuwa wakipigia bendi ya UDA na kuichezea mpira timu ya UDA, ndiye aliyeingilia kati na kutaka kujua kuhusu the whole deal ya yale mabasi sita, ndio akashia kuwalipa something ambacho hakikukubalika na wakubwa wake wa kazi, lakini hawa wenye mabasi sita mmoja wao yaani huyu John, alikuwa na connection na Kawawa wa kusini mwenziwe, alienda kumuona na ishu ikawa dead!

2. Kuhusu zawadi kwa viongozi, ukweli ni kwamba viongozi wa juu walikuwa wanapewa zawadi kila siku na wala hata siku moja hawakuwahi ku-surrender kwa serikali, I have seen it all hizi sheria zilikuwa ni kwa wanyonge tu sio kwa wakubwa, infact ni hii tabia mbaya ndio iliyowafanya US kuwafukuza watoto wote wa wakubwa kule kwao waliokuwa wana-scholarship za zawadi, hata watoto wa Mkapa na Mahalu walikuwa involved na hii deal!
 
Rev,

Hapo kuna one thing una-miss ni kwamba safari ndio uti wa mgongo wa kufanya kazi serikali toka enzi hizo mpaka leo, kwa hivyio viongozi wetu hutegemea sana safari, kwenye per-diem,

Sasa can you imagine safari na tena ni kiwanda cha soda ua bia? Halafu hebu nimabie kwenye kila msiba wa viongozi huwa kuna kuja malori ya soda na bia ni nani huwa analipia? Kwa sababu kikitokea tu kilio kwa kiongozi within one hour utayaona malori yakishusha, zamani yalikuwa yakiletwa na Tanzania Railways exactly ni nani aliyekuwa akilipia au siku hizi anyelipa ni nani hasa?

Kwenye hizi lines za kusafiri, kwenye maofisi yetu ya serikali kuna ambo ya aibu sana, mimi nimeona balozi analazimisha safari kwa nguvu, safari ile inatakiwa waende maofisa wa vyeo vya chini, lakini mkulu anag'ang'ania tu, haya anakwenda kuel kwenye mkutano anaambiwa kuwa hawezi kuingia kwa sababu rank yake inazidi zinazotakiwa kwenye mkutano ule,

Mkutano ni wa wiki nzima, mkulu anakaa pale kwenye chumba kimoja kwa ndugu yake huko majuu na ku-save, hii sasa serikalini imekuwa ni kawaida tu wala siop siri tena! Wewe niambie muungwana toka aanze kusafiri ameshakusanya hela ngapi za perdiem?
 
Back
Top Bottom