Wote uliowataja ni sawa lakini Zamoyoni hajawahi kuchezea Ndovu ya Arusha, alipotoka Kenya alikwenda Uarabuni baadaye akarudi Simba na ndipo akaenda kumalizia mpira wake kule Jangwani kwa 'vijisenti' vya Gulamali.
Mogella ni miongoni mwa wachezaji wachache wa miaka hiyo wasio na elimu waliongalia mbele. Pamoja na mpira wa wakati ule mchezaji uliishiwa 'kusifiwa' yeye alitengeneza future yake. Ukiacha wachezaji wachache wenye elimu kama Tenga, Mtemi, Mwalusako, Gumbo na wachache wengine ambao wako au waliendelea kuwa kwenye ajira. Hivi mlishawahi kukutana na Jellah Mtagwa hivi karibuni? Kumbuka huyu ni mchezaji pekee ambaye picha yake iliwahi kuwekwa kwenye stamp. Hivi mmewahi kumuona Hussein Ngulungu hivi karibuni? Nani alikuwa kama Ngulungu pale Pan African, nasikia ni mlinzi wa Godown ya Mohamed Enterprises pale Morogoro. Ukimuona Peter Tino na mdogo wake Gebo pale Kariakoo utawasikitikia. Wale wenye elimu angalau ya kidato cha nne, Tenga amekuwa akijaribu kuwatumia pale TFF kama kuwa makamishna wa Mechi mbali mbali na kamati za ufundi au kufuatilia matukio. Ukienda pale TFF Karume utawakuta wamepanga foleni wakitaka kumuona Tenga, sasa sijui wote hao atawapeleka wapi?
Nenda Leaders Club siku za Jumamosi utawakuta wamejaa tele, kazi 'kubom' Safari Baridi. Nawashukuru sana TBC, ITV na Star TV angalau wamekuwa wakiwachukua kuwa makomenteta wa mechi mbali mbali zinazoonyeshwa na vituo hivyo. I hope huwa wanalipwa kidogo. Maana hii Bongo we iache tu! Kuonekana kwenye kioo ni 'ujiko' so sitashangaa nikisikia malipo huwa ni kuonekana kwenye Luninga tu! Ila sasa sio kila mchezaji anaweza kuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira, juzi TBC walimleta Dotto Ruta Mokili, nikajiuliza huyu jamaa wamemuokota wapi? Bulyaga au Imasco? Maana alikuwa hajui hata anachokisema sembuse anachotuambia!