Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

gotee
Umewasahau akina Juma Mkambi,Mtemi Ramadhani, lila shomari,ninakumbuka sunday juma alikwana kijiosk pale msimbazi au ni malota soma yule sasahivi wako wapi?mavumbi omar na abuu omar,kassongo athumani,azizi nyoni, deo mkuki, michael kidilu,hamza maneno,geoge lucas,juma limonga,frank kassanga bwalya kilevi na weengii
 
Wote uliowataja ni sawa lakini Zamoyoni hajawahi kuchezea Ndovu ya Arusha, alipotoka Kenya alikwenda Uarabuni baadaye akarudi Simba na ndipo akaenda kumalizia mpira wake kule Jangwani kwa 'vijisenti' vya Gulamali.

Mogella ni miongoni mwa wachezaji wachache wa miaka hiyo wasio na elimu waliongalia mbele. Pamoja na mpira wa wakati ule mchezaji uliishiwa 'kusifiwa' yeye alitengeneza future yake. Ukiacha wachezaji wachache wenye elimu kama Tenga, Mtemi, Mwalusako, Gumbo na wachache wengine ambao wako au waliendelea kuwa kwenye ajira. Hivi mlishawahi kukutana na Jellah Mtagwa hivi karibuni? Kumbuka huyu ni mchezaji pekee ambaye picha yake iliwahi kuwekwa kwenye stamp. Hivi mmewahi kumuona Hussein Ngulungu hivi karibuni? Nani alikuwa kama Ngulungu pale Pan African, nasikia ni mlinzi wa Godown ya Mohamed Enterprises pale Morogoro. Ukimuona Peter Tino na mdogo wake Gebo pale Kariakoo utawasikitikia. Wale wenye elimu angalau ya kidato cha nne, Tenga amekuwa akijaribu kuwatumia pale TFF kama kuwa makamishna wa Mechi mbali mbali na kamati za ufundi au kufuatilia matukio. Ukienda pale TFF Karume utawakuta wamepanga foleni wakitaka kumuona Tenga, sasa sijui wote hao atawapeleka wapi?

Nenda Leaders Club siku za Jumamosi utawakuta wamejaa tele, kazi 'kubom' Safari Baridi. Nawashukuru sana TBC, ITV na Star TV angalau wamekuwa wakiwachukua kuwa makomenteta wa mechi mbali mbali zinazoonyeshwa na vituo hivyo. I hope huwa wanalipwa kidogo. Maana hii Bongo we iache tu! Kuonekana kwenye kioo ni 'ujiko' so sitashangaa nikisikia malipo huwa ni kuonekana kwenye Luninga tu! Ila sasa sio kila mchezaji anaweza kuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira, juzi TBC walimleta Dotto Ruta Mokili, nikajiuliza huyu jamaa wamemuokota wapi? Bulyaga au Imasco? Maana alikuwa hajui hata anachokisema sembuse anachotuambia!
Walipotoka Kenya wote watatu walifikia NDOVU.Zamoyoni alikaa muda mfupi sana pale kabla ya kusajiliwa na simba,kama kawaida yake kwani alikuwa haoni shida kuhama klabu moja kwenda nyingine au kukimbilia Oman wakati ameshasajili huku nyumbani.
By the way,nani anataarifa za Oscar Dan Korroso?
 
Walipotoka Kenya wote watatu walifikia NDOVU.Zamoyoni alikaa muda mfupi sana pale kabla ya kusajiliwa na simba,kama kawaida yake kwani alikuwa haoni shida kuhama klabu moja kwenda nyingine au kukimbilia Oman wakati ameshasajili huku nyumbani.
By the way,nani anataarifa za Oscar Dan Korroso?

Dan Korosso yuko Kyela ameamua kupumzika na shughuli za mpira.
 
1.
Mogella ni miongoni mwa wachezaji wachache wa miaka hiyo wasio na elimu waliongalia mbele. Pamoja na mpira wa wakati ule mchezaji uliishiwa 'kusifiwa' yeye alitengeneza future yake.

You got it right, huyu jamaa alikua mjanja sana, yeye na mchezaji mmoja kutoka Morogoro kama yeye kwa jina "Suzuki" Omar Hussein hawa walikuwa na akili sana, ninakumbuka Mogella alikua akiweka ahadi na watu wenye hela kuwa ataafunga goli, na watampa kama elfu kumi enzi zile kwa goli moja, duh jamaa bwana kifunga goli tu, utamuona kule kule kiwanjani akiwanyooshea mikono wale watu kuwa wajiweke tayari, maana mpira ukiiisha tu Mogella hutamuona kiwanjani, tayari ypuo kwa wale watu mpaka apewe ahadi yake, na hata siku moja usingemkuta kwenye kuagiza mapombe kama kina Tino na Jella, au Mambosasa,

I mean sijawaona hivi karibuni, lakini ninaamini kuwa popote walipo wana maisha mazuri sana, maana walikuwa wakimlilia sana enzi zile Virani na Gulamali, wawauzie share kwenye mali zao, na walikuwa ni mmoja ya wachezaji wachahce sana waliokuwa wakimiliki magari yao binafsi.


2.
Hivi mlishawahi kukutana na Jellah Mtagwa hivi karibuni? Kumbuka huyu ni mchezaji pekee ambaye picha yake iliwahi kuwekwa kwenye stamp. Hivi mmewahi kumuona Hussein Ngulungu hivi karibuni? Nani alikuwa kama Ngulungu pale Pan African, nasikia ni mlinzi wa Godown ya Mohamed Enterprises pale Morogoro. Ukimuona Peter Tino na mdogo wake Gebo pale Kariakoo utawasikitikia.

Hapa mkuu umenigusa sana, maana Gebo na ndugu zake ni washikaji wa karibu sana, wako watatu yaani Peter, Gebo na Imma, ambao wote waliwahi kucheza mpira kwenye timu kubwa kama Yanga na Simba, ninakumbuka enzi zile Peter yuko Pan na Taifa Stars, duh jamaa alikuwa ni mchuzi kibao lakini ugimbi tu, nilikuwa na mazoea sana ya kupita pita nyumbani kwao, pale mbele ya DDC Kariakoo, nakumbuka Baba yao ambaye alikua mstaafu wa Relwe, alijitahidi akajijengea kajumba kadogo sana kenye vyumba vinne na wote na dada zao walikuwa wakiishi humo humo, hata pale walipokuwa wachezaji wakubwa bado waliendelea kuishi humo,

Baadaye Peter alihamia Magomeni, lakini baada ya muda akarudi tena, mara ya mwisho nilipoenda kuwatembela washikaji, ilikuwa huzuni sana niliwakuta wote bado wapo pale, baba amekuwa mzee sana na mkewe nao wapo hapo hapo, Peter hana mbele wala nyuma, angalau Gebo yeye kuna Muarabu mmoja pale Kariakoo, amemuajiri kama mpiga dede wa duka lake kwa hiyo yeye husimama nje kupiga debe, huyu bwana mdogo Imma yeye alikuwa amelewa saa za asubuhi, halafu Jella huwa hawaaachani na Peter, yaani wakuu ukweli mbaya ni kwamba wanasubiri kutangulia kwenye haki tu maana hata ukiwaangalia usoni unaona hakuna hata hope ya maisha, kwa kweli machozi yalinitoka, very sad! Nilikuwa nimefuatana na mshikjai wangu mmoja hakuamini macho yake alismulia siku nzima,

I mean bado ninaendelea kuwasiliana na Gebo mpaka leo, lakini inasikitisha sana tena sana, sijui na hili nalo tutailaumu serikali au what?
 
FMES,
..nani anawakumbuka jamaa wa nyota nyekundu? wakina frank kasanga "bwalya", mohamed nyauba, stephen chibichi, dennis mdoe, feruzi udi, faustin kibingwa, ndunguru,..

..halafu kuna coastal union moja ilikuwa kali sana. sina uhakika kama walishinda kombe la afrika mashariki.

..coastal union ninayoiongelea ni ile ya kina Kassim Mwajeki,Hussein Mwakuruzo,Hassan Juma,Mohamed Mwameja,Juma Mgunda,...

..Zanzibar nako kulikuwa na Small Simba. wadau naomba mtukumbushe hawa vijana.
 
dennis mdoe,

I see huyu jamaa alikuwa Mlimani akiichezea Yanga, baadaye alihamia Botswana, sasa hivi yupo Canada pia nina mawasliano naye sana, alikuwa anasomea u-Engineer, kazi anayoifanya sasa,

Alipokuwa Tambaza High, alikuua roommate wa marehemu wa bwana mdogo wangu, that is how I came to know the guy, very nice guy na ana akili sana za shule na maisha.

Pia ninamkumbuka Chibichi na Mwameja, nakumbuka jinsi Mwameja walivyokuwa wakigombania ujiko wa goilikipa na Father Idd Pazi, kuna wakati ilikua patashika sana ndani ya timu ya Simba.
 
feruzi udi,

Huyu jamaa aliacha mpira na kwenda mlimani akalamba degree yake ya Engineering sasa yupo Tanesco kibosile fulani hivi na mambo yake superb!
 
I see huyu jamaa alikuwa Mlimani akiichezea Yanga, baadaye alihamia Botswana, sasa hivi yupo Canada pia nina mawasliano naye sana, alikuwa anasomea u-Engineer, kazi anayoifanya sasa,

Alipokuwa Tambaza High, alikuua roommate wa marehemu wa bwana mdogo wangu, that is how I came to know the guy, very nice guy na ana akili sana za shule na maisha.

Pia ninamkumbuka Chibichi na Mwameja, nakumbuka jinsi Mwameja walivyokuwa wakigombania ujiko wa goilikipa na Father Idd Pazi, kuna wakati ilikua patashika sana ndani ya timu ya Simba.

Mkuu FMES, umenikumbusha mbali sana! .... Dennis Mdoe tulikuwa wote kwenye timu kali ya soka ya UDSM, wakati na mimi nikiwa mwanafunzi pale ... hiyo timu ya UDSM nadhani ndiyo ilikuwa the best ever ... wachezaji wengine walikuwa Leonard Thadeo (kamishna wa Michezo hivi sasa), Lawrence Mwalusako, Mtemi Ramadhani, yours truly 🙂 , na wengine kibao!
 
Wakulu vipi siku hizi mbona naona kasi ya picha inapungua?????? Zimeisha au? Sio kama sithamini mchango wa mijadala iendeleayo hapa nyuzini basi na picha nazo zina utamu wake. FMES, Kichuguu, Mchongoma, na wengine vipiiiii, Picha wazee.......
 
Mkuu FMES, umenikumbusha mbali sana! .... Dennis Mdoe tulikuwa wote kwenye timu kali ya soka ya UDSM, wakati na mimi nikiwa mwanafunzi pale ... hiyo timu ya UDSM nadhani ndiyo ilikuwa the best ever ... wachezaji wengine walikuwa Leonard Thadeo (kamishna wa Michezo hivi sasa), Lawrence Mwalusako, Mtemi Ramadhani, yours truly , na wengine kibao!

Mkuu ahsante sana, jamaa yupo Canada na maisha mazuri sana kwa mchezaji wa zamani wa Yanga, nice guy na kichwa sana na down to earth, ahsante mkuu kwa hamsini zako.
 
Vipi wakuu waliopo uk tunasikia Nico Njohole yuko huko ni mgonjwa jee kuna yoyote anaefahamu habari zake
 
Vipi wakuu waliopo uk tunasikia Nico Njohole yuko huko ni mgonjwa jee kuna yoyote anaefahamu habari zake

Mara ya mwisho mkulu Chuma kama sikosei ndiye aliyetuletea habari, sasa sijui lakini aliahidi kua ataleta habari zaidi.
 
Duh!!!,

Sikujua kuwa thread hii bado inaendelea; nilipotea kidogo halafu leo nafungua na kukuta bado ianaelea juu juu. Kumbe kuna watu wengi wanaothamini tulikotoka?

Mkuu FMES aliyeianzisha na wachangiaji wote, pokeeni shukrani nyingi sana toka kwangu kwa kutukumbusha tulikotoka.
 
Sikujua kuwa thread hii bado inaendelea; nilipotea kidogo halafu leo nafungua na kukuta bado ianaelea juu juu. Kumbe kuna watu wengi wanaothamini tulikotoka?

Mkuu karibu tena mjadala haujaisha bado kabiaa maana soon ninakusudia ku-unleash picha kibao za historia, karibu tena mkuu na heshima wka wote na hasa wewe, Icadon, Mchongoma, na wengineo kwa michango mizito sana na tutakapotengeniza kitabu rasmi cha hii thread tutawa-dedicate kwa uhakika wale wote mliochangia kuliko the average,

Na pia nimshukuru sana Mkulu wangu Mwanzage, kwa uvumilivu wa hali ya juu katika hiki kipindi tunachojaribu ku-put things together, na pia niwashukuru Clouds kwa all thier support on this project, mkulu wangu Joe Mungu akubariki na ninakutakia mafanikio katika your next TV project ambayo inakaribia kujipa sooon, bravo!

Ahsanteni Wakuu JF mbele!.
 
wote uliowataja ni sawa lakini zamoyoni hajawahi kuchezea ndovu ya arusha, alipotoka kenya alikwenda uarabuni baadaye akarudi simba na ndipo akaenda kumalizia mpira wake kule jangwani kwa 'vijisenti' vya gulamali.

Mogella ni miongoni mwa wachezaji wachache wa miaka hiyo wasio na elimu waliongalia mbele. Pamoja na mpira wa wakati ule mchezaji uliishiwa 'kusifiwa' yeye alitengeneza future yake. Ukiacha wachezaji wachache wenye elimu kama tenga, mtemi, mwalusako, gumbo na wachache wengine ambao wako au waliendelea kuwa kwenye ajira. Hivi mlishawahi kukutana na jellah mtagwa hivi karibuni? Kumbuka huyu ni mchezaji pekee ambaye picha yake iliwahi kuwekwa kwenye stamp. Hivi mmewahi kumuona hussein ngulungu hivi karibuni? Nani alikuwa kama ngulungu pale pan african, nasikia ni mlinzi wa godown ya mohamed enterprises pale morogoro. Ukimuona peter tino na mdogo wake gebo pale kariakoo utawasikitikia. Wale wenye elimu angalau ya kidato cha nne, tenga amekuwa akijaribu kuwatumia pale tff kama kuwa makamishna wa mechi mbali mbali na kamati za ufundi au kufuatilia matukio. Ukienda pale tff karume utawakuta wamepanga foleni wakitaka kumuona tenga, sasa sijui wote hao atawapeleka wapi?

Nenda leaders club siku za jumamosi utawakuta wamejaa tele, kazi 'kubom' safari baridi. Nawashukuru sana tbc, itv na star tv angalau wamekuwa wakiwachukua kuwa makomenteta wa mechi mbali mbali zinazoonyeshwa na vituo hivyo. I hope huwa wanalipwa kidogo. Maana hii bongo we iache tu! Kuonekana kwenye kioo ni 'ujiko' so sitashangaa nikisikia malipo huwa ni kuonekana kwenye luninga tu! Ila sasa sio kila mchezaji anaweza kuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira, juzi tbc walimleta dotto ruta mokili, nikajiuliza huyu jamaa wamemuokota wapi? Bulyaga au imasco? Maana alikuwa hajui hata anachokisema sembuse anachotuambia!

jellah mtagwa anaishi pale nyuma ya friends corner hotel na alikuwa mwajiriwa wa murtaza dewji kwenye ile kampuni yake ya tasia. Kuna kipindi alikuwa anaumwa. Ukweli ni kwamba huyu mzee anaishi eneo ambalo hata gari haliwezi kuingia ,wewe unaweza jua aina ya life anayoishi hapo. Mungu ambariki , maana kuna wakati huwa napenda kuamini sisi wa morogoro tuna letu jambo ila kwa kumuangalia sahau kambi na mogellah kidogo naona bado tupo ila ipo haja ya kujipanga
 
Kwanini hatufili kwamba mafisadi hawa walimtanguliza Mwalimu hakini, iliuwanja uwe wazi kwao, kwani kansa ya damu ni moja ya silaha, zilizotumika na KGB. Mchezo haukuanza kwa Balali tuu.
 
Vipi wakuu waliopo uk tunasikia Nico Njohole yuko huko ni mgonjwa jee kuna yoyote anaefahamu habari zake

Ni kweli Nico bado ni mgonjwa kule UK; ila uzuri ni kwamba maumivu yamepungua kiasi cha kwamba ametoka hospitali (ICU), na sasa anajiuguza nyumbani. Nitaendelea kuwapa maendeleo ya hali yake kwa kadri nitakavyozipata toka uingereza.
 
Ni kweli Nico bado ni mgonjwa kule UK; ila uzuri ni kwamba maumivu yamepungua kiasi cha kwamba ametoka hospitali (ICU), na sasa anajiuguza nyumbani. Nitaendelea kuwapa maendeleo ya hali yake kwa kadri nitakavyozipata toka uingereza.

Mkuu ahsante kwa hizi habari ubarikiwe, na uendelee kutuletea zaidi.
 
Hii siyo ya Kitaifa, bali ni katika msululu wote wa kukumbuka tulikotoka; this time mimi personally.

Mimi nawatafuta rafiki zangu tuliokuwa tunapiga mUziki pamoja kwenye bendi ya Kizigo Jazz ya Tabora Boys kati ya mwaka 1975 na 1978. Ningependa kujua akina Simon Kasembe-mkali wa solo (huyu sijui aliishia wapi mara ya mwisho alikuwa akaungane na kaka yake aliyekuwa Super Volcano lakini mara baada ya kifo cha Mbaraka sijui aliishia wapi). Vile vile namtafuta Bob aliyekuwa mshenzi wa Rythm (mara ya mwisho miaka zaidi ya 15 iliyopita niliambiwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa NBC Kilosa). Bob aligawa wimbo fulani wa Kizigo Jazz kwa Tabora Jazz alikokuwa akifanya part time; sina uhakika kama wimbo ule ulikuwawa Serafina au wa Mariamu. Kuna Makongoro Nyerere aliyekuwa mpiga bass mkuu na kiongozi wa bendi (nadhani yeye bado ni mwenyekiti wa CCM Mara), halafu kuna Ndonde (nadhani bado ni ofisa wa jeshi kikosi cha vifaru pale Lugalo), na yule jamaa aliyekuwa na machunusi mengi sana lakini alikuwa mkali sana wa kupapasa tumba-sikumbuki jina lake, sijui naye yuko wapi sasa. Niliwahi kukutana na Luteni Maneno Nguruhi aliyekuwa fundi mitambo wetu wakati huo, nadhani bado anaishi Australia kwa vile alikuwa na skendo kubwa sana Tanzania baada ya kutorosha ndege ya jeshi kwenda Komoro mwaka 1981. Kuna Msuya aliyekuwa akipuliza alto sax nadhani na yeye alijiunga na NBC miaka hiyo ya sabini. Mwingine ni rafiki yangu Katute alikuwa msaidizi wa Nyerere kwenye bess; mwishoni mwa miaka ya themanini nilimkuta Musoma akiwa ofisa wa benki. Kuna marafiki zangu wengi tuliokuwa tunakula good time pale TS, ningependa kujua wako wapi. Kama kuna anayejuwa jamaa waliokuwa wakipigia Kizigo Jazz ya Tabora School miaka hiyo, naomba tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom