Tukumbushane maisha ya UDSM enzi hizo, wazee wa Bibo na Main Campus

nipo hapa ilikuwa bumu likitoka lazima nimpeleke manzi wangu wa kichagga kula Hill Park, bumu likikata naenda kwa Bwashee pale Coet cafteria elfu 25 nakula bure semester nzima 😂😂😂
Nmekula sana ukoko udsm jameni, we acha tuu maisha haya, buku kwa siku mwezi 30k, na sikupunyuka nywele, show ilikuwa ni kali
 
Ilikuwa ikibaki wiki moja boom litoke, tulikuwa tunatoka pale njee kwenye parking ya mabibo hostel usiku tunaanza kulia
Njaaaaa njaaaa njaaaaa njaaaa
Kumbe nilikuwa najilaani nimekuja mtaani njaa imenipiga nusu kufa
Ulikuwa mtu wa makundi sana na kufuata mikumbo. Kifupi hukuwa na msimamo binafsi na ndio maana njaa inakuua huku mtaani, na iwe fundisho kwa vijana wapuuzi kama wewe, wasiojua wamekwenda kufanya nini chuo.
 
Pale sisi tulikuwa hatuangalii uandishi ni intergral tu kila sehemu ,ndi maana sizingatii uandishi .A ya Mathematics na Physics ndio zilinipeleka pale kugonga miaka yangu minne kule bondeni Coet ,wala sio Kiswahili ambacho niliginga D O-level.
Upo wapi kwa sasa, na unajishughulisha na nini?
 
Maliza kwanza chuo dogo ndio uje kunitolea shombo. Hizo ni akili za boom zinakusumbua
Unajuaje kama nina boom? Je kama sina? Huo ndio uhalisia, wengi mnajisahau na kuishi maisha yasiyo yenu, unaonekana tu kuwa ulikuwa mzee wa sosho, makundi kwa sana, clubs n.k, mkija DSM ushamba wenu wa mikoani kwenu muuache, fuateni kilichowaleta. Unaonekana hukujua kuwa baada ya chuo utakuwa peke yako.
 
Unanipa tabu sana kukujibu dogo, kwani kielimu nimekuzidi mbali sana. Halafu pili wewe sio udsm member sababu ya ufaulu mdogo uliokuwa nao.
Ndio maana nakwambia maliza kwanza chuo ndio uje kunipa ushauri.
 
Unanipa tabu sana kukujibu dogo, kwani kielimu nimekuzidi mbali sana. Halafu pili wewe sio udsm member sababu ya ufaulu mdogo uliokuwa nao.
Ndio maana nakwambia maliza kwanza chuo ndio uje kunipa ushauri.
Nani kakuambia kila asiyesoma UD ana ufaulu mdogo kaka? Unakosea sana, sasa kam mpaka div 3 wapo wanaosoma UD, sasa mimi nikihitaji kwa nini nishindwe? Hoja dhaifu hiyo bro, pia hujui nasomea kozi gani na hujui kama hapo UD ipo au haipo.
 
Ni aibu huu uzi tunakumbushana mambo tuliopitia udsm members. Mtu anasoma sijui teifilo kisanji anakuja kujifanya mshauri humu
 
Ni aibu huu uzi tunakumbushana mambo tuliopitia udsm members. Mtu anasoma sijui teifilo kisanji anakuja kujifanya mshauri humu
Naomba uniambie bro, kwa nia njema tu. Ulisoma kozi gani na ni mwaka gani?
 
Mie sitosahau vyoo vya hall5..nyaa nje nje nawee unaenda jazia lakoo...

Sie wengne tulikua tunakula cafeteria 1 RB mshikak m1 halaf tunaenda tena cafeteria 2 wali njegere mshikak m1...

Nilikua na madem wawil bcom na wote wanakaa hall3
 
Mimi nilisoma wakati boom ni 3000, eneo la Mlimani city kulikuwa na mapori tu, off campus hostel ilikuwa blocks za CRDB Kijitonyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…