residentura
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,146
- 11,434
Ila chuo kulikuwa na mambo mengi ya kujifunza nje ya masomo. Mfano kulikuwa na kaka mmoja anauza 'chupi' , akipita nje ya vyumba anaita pichu pichu. Kuna siku nikamuuliza hii kazi inakunufaisha? Akasema anasomesha wadogo zake kadhaa kwa biashara ya chupi na mambo madogo madogo hayampigi chenga! Alikuwa anavaa smart na begi lake la chupi km kabeba laptop kumbe anapiga business na inamuingizia. Heko kwake, anaambia wadada "nunueni chupi jamani , sio unavaa chupi imeisha, imechokaa, ukisimama mbele ya feni mjupi unapepea ", hahahaaaaa
Huyo jamaa inabidi mchango wake utambuliwe na kupewa shahada ya heshima ya B. W. Mkapa.