Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Mkuu hii ni biashara ya wazungu🀣🀣🀣🀣🀣
 
Watu walipukutika sana aisee. Mimi nilikuwa UDSM tukawa tunazika karibu kila baada ya siku mbili; pale Kinondoni makaburini kulikuwa na baa moja ya container wakatuzowea sana kwani baada ya mazishi wengi wetu tulikuwa tunapata moja baridi pale kabla ya kurudi zetu mlimani.

Wakati huo serikali ya Kenya ilitupatia Kemron lakini haikusaidia
 
najaribu kufikiria kama ugonjwa alipatikana kagera kwa mtu mmoja ulienea vip?
Siyo kwa mtu mmoja bali mtu wa kwanza alipatikana Kagera lakini haimaanishi ndiye mtu pekee aliyekuwa na UKIMWI.

Mashujaa kama Philly Lutaya wa Uganda wangejua kama zama hizi Kuna kizazi kingekuja kusema kuwa UKIMWI ni jambo feki, wangefanya zaidi kuliko walivyofanya.
 
Aisee, umenikumbusha Kuna jirani yetu kule home alikuwa na mdogo wake alikuwa na huu ugonjwa alikonda kias kwamba alikuwa kama amelala kwenye godoro chini(kwasababu kitandani alikuwa hawezi hata kupanda) na akijifunika shuka basi huwezi kuhisi kama Kuna mtu amelala mahali hapo.

Sasa Kuna hizo arv nadhani ndyo zilikuwa zinatoka ilikuwa ni mwaka 2006 kama sikosei, Kuna sister anaitwa Anjela(wa kizungu) ndyo alikuwa anamletea hizo dawa.

Shida yule dada(mgonjwa) alikuwa akipewa zile dawa alikuwa anatapika na kidonge kilikuwa kinaruka kutoka mdomoni kwenda nje mithiri ya jiwe lililorushwa kwa kutumia manati na hiyo ilikuwa ni kutokana na ukubwa wa vidonge veynyewe maana vikuwa vikubwa sana.

Haikupita hata mwezi tangu afike pale kwa ndugu yake yule dada aliaga dunia.
 
upo sahihi mkuu miaka hiyo muingiliano wa watu haukuwepo sana kama sasaivi lakini haimaanishi watu walikuwa hachangamani kabisa,,,binadam ni tofauti na milima
 
Mdogo wake rafiki angu alipotea
Tumekuja kumpata kumbe alienda house party huko wamejifungia siku 5 ni uzinzi tu nadhani walikuwa wanafanya group sex
Aisee watoto wa chuo wanapukutika na tamaa ndo zinawaponza
Hivi ndyo wanaita three some? 😭😭😭
 
Huku towns hii ilikuwa ni kawaida sana mnazika hapa, hapo nyumba za jirani kuna wagonjwa kadhaa wapo ndani hoi mahututi wanasubiri masaa tu wakate kamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…