Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Tukumbushane maisha yalivyokuwa kabla ARV hazijaanza kutolewa

Aya marazi niyakutengenezwa pia kunasiri nyingi najalibu kufikilia kama ugonjwa alipatikana kagera kwa mtu mmoja ulienea vip? Maan ilikua rahisi kuzibiti kupitia uyo mgonjwa? nawaza mbali zaid miaka ya 70 miundo mbinu haikua rafiki kusababisha muingiliano wawatu wengi, je ilikua vip ugonjwa kufika dar au mtwara? na vip kuhusu watu wa vijijini?
Ugonjwa umekaa pabaya kala wanawake na wanawake wakaliwa na watu wengine ikasambaa. Ni uthibitisho kuwa uaminifu katika ndoa na maisha ya mapenzi haupo kwa watu wote.
 
ni kweli mkuu makete ilikuwa balaa jingine kuliliza watu sana adi media za

Nakumbuka kijijini kwetu mgonjwa wa kwanza alikuwa mwanajeshi akaletwa akiwa hoi mwaka 1987 majira ya kiangazi.Elimu ilitolewa kwa wanafamilia katika kumtunza mgonjwa wa AIDS(ilitamkwa kama edisi).Kama ni unyanyapaa mtu yule alipitia tena wa kutisha kwani iliaminika kwamba akikugusa tu unapata edisi.Wengine tulikuwa kinda na hivyo tulionywa juu ya uzurulaji twawezakutana naye akatugusa tukapata edisi.Mpaka mwaka 1992 ugonjwa wa edisi ukapewa jina la UKIMWI.Kwa kweli tuliowauguza wagnjwa wa UKIMWI mpaka hatima ya maisha yao,kumbukumbu zikirejea mpaka hamu ya mbususu inapungua maana shughuli ilikuwa pevu.
Unyanyapaa ulikuwa wa kutisha enzi hizo. Kaka yangu RIP alikosa hata mtu wa kumuogesha akawa anaogeshwa na mama yake mzazi, maana mama RIP alisema mwanangu nilimwogesha alipokuwa mdogo basi na sasa bado ni mwanangu tu. Sasa fikiria mwanaume wa miaka 40 unaogeshwa na mama yako unajisikiaje?
 
Mdogo wake rafiki angu alipotea
Tumekuja kumpata kumbe alienda house party huko wamejifungia siku 5 ni uzinzi tu nadhani walikuwa wanafanya group sex
Aisee watoto wa chuo wanapukutika na tamaa ndo zinawaponza
Wanafanya mambo ya kina Pdidy
 
Mgenii, mgenii ili mgeni huyu mgeniii, mgeni kwetu ameingiaaaaa, mgeni mgenii mgeni huyu balaaaa..... huu wimbo ulikuwa unausikiliza kwa umakini mkubwa sana
 
Sasa hivi wanaimiza kutumia mipira,,kuwa na mpenzi mmoja,sio kuacha zinaa!!!!,,washauri nasahaa na watu wengine wa ajabu kweli kweli,, mhimu kuacha zinaa baasi,ndo ushauri bora sana.
Nyege mbaya na walio oa pia wana zini nje so bora watumie mpira buko nje ila ukimwi miaka ile ulikua wa kutisha sana sahv kama haupo kumbe una tu zoom tufanye ujuha na trump kazima msaada
 
Unyanyapaa ulikuwa wa kutisha enzi hizo. Kaka yangu RIP alikosa hata mtu wa kumuogesha akawa anaogeshwa na mama yake mzazi, maana mama RIP alisema mwanangu nilimwogesha alipokuwa mdogo basi na sasa bado ni mwanangu tu. Sasa fikiria mwanaume wa miaka 40 unaogeshwa na mama yako unajisikiaje?
iyo ilikuwa kawaida sana ishu kama iyo au kukuta kaka anamuuguza dadaake mtu mzima uko wa 30+ au dada kumuuguza kaka mtu mzima hadi anakata roho. hali ilitisha sana acheni kabisa. asante mkuu Azizat i hope wengine wanajifunza kitu kwa kusoma shuhuda kama hizi.
 
- Hizi ARV zimeanza kutolewa kwenye mwaka 2003 au 2004 hapa wenye kumbukumbu sahihi mtanirekebisha. kabla ya hapo hapakuwa na dawa za kufubaza.

- Ugonjwa huu uliogopesha sana kiasi ambacho jamii haikuwa tayari kuuzungumzia. kimya kikuu kilitanda bila shaka kila mmoja akiomba kwa mola wake amuepushe na kikombe.

- Elimu kwa jamii zilitolewa zikichagizwa na picha za kilichokuwa kinaendelea mkoa wa kagera. kwa mujibu wa taswira zìle huko kagera ugonjwa ulimaliza watu wengi na wengine hata nyumba zilifungwa hakuna aliyebaki. nyumba zingine nyingi zilibaki zikiendeshwa na watoto mayatima baada ya wazazi wote kufariki.

- Kimya kingi kilitanda huku ugonjwa ukiendelea kutafuna watu kimyakimya.

- Kwenye hatua za mwanzoni wagonjwa wengi walikuwa wakionekana kupata mkanda wa jeshi yani miaka hiyo kama wewe una mkanda wa jeshi tu basi ilikuwa ni uthibitisho tosha tayari una tatizo hilo.

- Ukiona jirani yako flani haonekani hapo mtaani hiyo ilikuwa ni ishara tosha kuwa kama jirani uyo hajasafiri basi tayari uenda mambo yameshaharibika.

- Ugonjwa ulikuwa haufichiki. Ukiwa nao utajulikana tu apo kitaani kwenu. maana mwanzoni utajifungia ndani kwako lakini bdae lazma utoe ukahemee au kupata matibabu nk. ukitoka tu habari zako zinaanza kusambaa kama moto wa nyika.

- Ili kuepuka macho na vidole vya walimwengu familia nyingi ziliwapeleka mahospitali wapendwa wao mapema alfajiri sana au hata usiku.

- Familia nyingi zilikuwa zinaepuka kuwapima wagonjwa wao maana unampimaje mtu wakati unajua ugonjwa wenyewe hauna dawa. hivyo basi familia nyingi ziliishia kuuguza tu wagonjwa wao kimyakimya hadi wagonjwa anapokutana na mwisho wake.

- Wagonjwa wengi waliisha sana miili yao. hata kama ulikuwa kibonge kama pipa mwili wote utaisha kabisa unabaki kichwa ngozi na mifupa mitupu tu. ilikuwa sio ajabu kukuta mtu mwenye mwili mkubwa kama wale mabaunsa kaisha mwili wote kiasi hata usiweze kumtambua.

- Ilikuwa kawaida tu mtu mzima kabisa mwenye mwili uliojengeka vema akamalizwa na kubaki makongoro tu kiasi ambacho akilala kitandani hlf wewe ukapita apo usimuone au kujua kama pale kitandani kuna mtu amelala. najua kuna wanaozani natania lakini iyo ndio hali ilivyokuwa wakati huo.

- Watoto wengi waliozaliwa na maambukizi hawakuweza kuishi wengi walifariki baada ya muda mfupi na wachache kwa kudra za mwenyezi waliweza kuishi na wengine wako hai hata leo hii.

Hapa tunakumbushana tu hatutishani ukimwi upo tujilinde.

***Tafadhali msiuunge uzi huu tuna vijana damu changa wengi humu wanapaswa kupata ufahamu wa kule tulikotoka.
Ukiugua ugonjwa mwingine tofauti na kuanza kuharisha tu,basi taarifa zinasambaaaa kama moto wa chini ya mti wa mwembe kuwa unao.
 
Jamaa akiendelea kukaza,hali itakua mbaya sana,kuna watu wamejaa kumbe ni ARVs,na wanakufa vifo vya ghaflaghafla tu,wanaacha utata.
wahusika wameshatia neno
👇👇
Screenshot_20250208-102604_Instagram Lite.jpg
 
Haahaa mkuu Deception na theory zake. kitambo sana hajaonekana humu.
Deception "HIV is hoax it never exists, there is no undisputed scientific evidence that proves the existence of HIV virus",

ARVs ndio zinasababisha ukimwi

Aisee nimemmiss sana deception hasa kwenye ule msiguano wake na mainstream doctors ilikuwa ni fire.
 
Deception "HIV is hoax it never exists, there is no undisputed scientific evidence that proves the existence of HIV virus",

ARVs ndio zinasababisha ukimwi

Aisee nimemmiss sana deception hasa kwenye ule msiguano wake na mainstream doctors ilikuwa ni fire.
😁😁😁jamaa kapotea sikuhiz. sijui kapatwa na nini.
 
Ukiugua ugonjwa mwingine tofauti na kuanza kuharisha tu,basi taarifa zinasambaaaa kama moto wa chini ya mti wa mwembe kuwa unao.
ndio maana izo ndo zilikuwa homa zinazotokea sana kwa iyo shida kwaiyo ukipata maradhi tofauti ukakonda na kuhara watu walikuwa wanakuunganisha tu
 
Back
Top Bottom