Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Mmmh, hivi niliwahi kupigwa kweli mm sidhani, lbd mambo ya fumanizi fumanizi ndiyo nimebobea sana [emoji12] [emoji12]
(Joking)
 
Kuna siku nilikuw nimeenda club bn..
Nikatumia bapa za kutosha mpk akili akiwa sio yangu tena. Pembeni angu kulikuw na mrembo , kama kawaida yetu nikamfata bana. Kumbe alikuw na jamaa ake
Yule jamaa ake akanikazia kidg, nikaona isiwe tabu bn nikamtia kitasa
Kumbe jamaa alikue na kundi lake kam la watu 12 iv. Wakanivamia, nahic nilikula scale kubwa zaid ambayo cjawahi kuipata tangu nianze vurugu mpk nikakata moto.
Nimekuja kustuka saa 10 alfajir nipo mtaroni tena mvua ndo ilikuw imeanza kunyesha.
Siku ile siwezi kuisahau mimi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
Au Daudi na Goliathi.

Nakumbuka nilikuwa Kariakoo mwaka mmoja, dunga dunga akataka kunigeuza kitoweo....mbona nilitaka kuondoka na dhakari zake.
Afu katikati ya soko
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
Maelezo yotee hayo nmeelewa kwenye wezere tu
 
Hahahahaha hii noma sana umenikumbusha time fulani kitambo tulikuwa na mechi za kitaa
Day moja hiyo tukajichanganya kuna watoto wa kota waliomba tucheze nao game tukazama kambini kwao kukisanua.
Game tulianza vizuri tu sasa tulivyo wapiga goal tu mpira ukaanza vurugu game ikawa na boot kinoma hapo unaombea game iishe tu maana boot zaidi ya league ya bundasliga ka kipindi kile.
Kumbe watoto wa kota game inaendelea wengine wafata faru na mikanda majumbani kwao mzee ilikuwa noma.
Game imeisha hivi ilibidi kila mtu ajue njia ipo wapi maana tupo kambini ila ilibidi tuanze kushughulika nao mmoja mmoja wakipita mtaani maana kambini walileta ubabe
Nasi tukawa tunawawinda kitaani tu.


Mtoto wa kambini kila akipita kitaani kazi alikuwa nayo ni kichapo tu.
 
Me hua nakinukisha tu kuliko vyoo vya baa hasa mtu anaponizingua na najua kabisa sina kosa ila anataka kuniletea za kinyonge sijui niwahadithie ipi?? Ila poa acha nianze na hii :

Ilikua shule ya msingi na ilikua kila siku naandikwa kwenye majina ya wapiga kelele kuna siku hiyo sasa nikasema nikae kimya siku nzima nione itakuwaje cha kushangaza bado nikawepo kwenye list ya noise maker japo sijawah kukanyaga arusha(joking) na kama kawa nikachezea kichapo cha mwalimu huyo anapiga kama kakufumania na mkewe basi kichwani nikajisemea leo mda wa kutoka mguu wa shingo mguu wa roho lazima huyu monitor anijue vizuri kama mimi mwenzake chekechea china

Itaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipewa pass ya kwenda kung'oa jino Mawenzi hospital, ilikuwa Ijumaa niliamua kuingia disco kbla ya kurudi shule J'mosi. Sasa kulikuwa na wavulana wawili wananifukuzia kheri si nikawakuta wote ndani, kila mtu anataka kuwa na mimi ugomvi disco lilifungwa.

Moshi si kuwa ninajulikana vijana walitaka sana kumjua manzi aliyesababisha disco kufungwa na police kuingilia, wakati huo nilishachukua tax na kutokomea.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] we ni kiboko ya uchafu; mi cjawahi kugombana jmn afu nikikasirika cwez kuongea nalia tyu mpka Leo!!ila nilikuwa na best yngu hyo ngumi mkononi c anajua mi muoga MTU akinichokoza tu ananunua ugomvi wee hakubali kushindwa wakawa wanamuita ngumi jiwe [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Nishaanzisha mavagi mengi saaana mana utata upo damuni ila sitasahau matukio matatu.
MOJA
Nikiwa darasa la tano tulikua na mobb tunazamia shughuli za watu hatar. Sasa siku moja form four kwny shule ya wilaya nlokuwepo walikua na graduation mm na mobb yangu tulifanya kila tuwezalo kuzamia ukumbini tukashindwa basi tukaamua tuvuruge ukumbi ulikua na fensi ya tofali ila juu wazi tukatafuta mayai viza tukayarusha ukumbini yakawapata watu kadhaa. Ebana nakumbuka ilikua jioni km saa moja ivi sasa walivotoka kutafuta walorusha mm nikajishtukia nikakimbia baba ili toka troop kunikimbiza nakumbuka enzi hizo nilikua kadogodogo nachomoka hatar ila ilitokea njemba moja mbele yangu ikanirukia km swala. Nilichezea kichapo hicho km mtu mzima nikiwa hoi full damu wakanipeleka kituoni. Sasa wasijue OCS ni mother angu na kipindi hicho bro wangu wa kwanza sahv marehemu alikua likizo ni mjeda na muda huo wananipeleka kituoni alikua huko na maza. Kufika kituoni watu km sita ndo wameniweka mtu kati mara ghafla bro hyu kwanza akajua nimepata ajali kumbe kichapo si wale jamaa wakajichanganya kusema wamenipiga kisa nimeharibu sherehe wakat huo na mother akatoka nje ananiona navuja damu ebana kibao kikawageukia walikula kichapo heavy na vichura na kugharaghara sana tu. Sema nilivyorudi home dingi alivyopewa udaku akanipa tena kipigo nilimind sana siku hyo.

PILI
Tulikua field ya mwaka wa kwanza Dodoma tumekula pombe saaana pale carribean bar karibu na bunge mida ya saa tisa tukakubaliana twende mnadani kula mbuzi. Tukapanda coaster sasa kutokana na nilikua maji nilikua nazingua kinoma ndani ya gari baada ya muda kidogo nikaanza msumbua dereva asimamishe gari nichimbe dawa raia wakawa wanadai asimamishe toka lini daladala ikasimamishwa kuchimba dawa nikatishia ntakojoa humohumo dereva ikabidi asimame wakat huo nitema lugha ya malkia tu sasa wakat nafika mlangoni kuna jamaa yanki tu akaniwekea mkono kifuani akidai siwez shuka dereva aondoe gari sasa mm nikiwa maji enzi hizo sifikirii Mara mbili nikampa BONGE ya ndoo kuna ni vile vijeda vilivyopo depo makotopora bana na vipo km sita mule nilichezea kipigo kitakatifu km niko arena vile na wakasema gari break ya kwanza kambini wakanionyeshe uanaume ulivyo dah pombe zilikata. Pona pona ni kuna bibi mmoja alikua amekaa siti moja na mm wakat huo nipo siti ya dirishani akaanza waambia anataka shukia kituo kinachofuata haiwezekan wampitishe na hana hela ya kurudi si ndo kosa lililofanyika hilo nikafungua dirisha huku gari linaelekea kusimama nilivojirusha nje hata wanajeshi wenyewe walisema kwel mm kamanda kila mtu alifumba macho basi speed nlotoka nayo hapo Mungu ndo anajua.

TATU
Nikiwa likizo home ndo ya kwanza tokea niajiriwe sasa nilijipanga kwel kwel kwenda kula likizo tulikua na braza angu na ndugu yangu mmoja tulikua tunakula bia 24/7 mana nilipanga kukaa wk mbili na niliandaa laki ya kila siku kula bia siunajua wilayan hakuna mambo mengi so ilitosha mno. Sasa mm sijulikani sana huko wilayan kwetu na kuna wanajeshi wengi na walikua wameshushwa km 600 kwny operation maalum so kumbe tule tuanajeshi vijana tulikua tunamind sana rohoni navyokula monde wakat vyenyewe ndo talk of the town. Siku moja km saa tano usiku ivi braza na yule ndugu yangu wakiwa chakari wakazinguana nikawa nawasuluhisha vile vijeda si ndo vikapatia upenyo wa kurevenge vikidai nawapiga ndugu zangu ambao ni rafiki zao vilinipa vinu vya hatar sema safar hii nami nilimuachia mmoja alama nilimpiga kichwa hicho nikatoka na jino lake kwny paji la USO hfu mi nduki asubuh nikaamkia barabarani hyoo Dar.
Baada ya matukio hayo yote nlitafakar pombe siwez acha ila nliamua kutokua nakunywa nagrp la watu especially kunywa na warembo, pili sinywi kwny bar za ushenzini na nikaanza kula bia expensive tu ambazo siwez kunywa nyingi sasa nastaarabika na mchumba ninae mwaka keshokutwa naoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jirani wewe ni mtata... hata ukiniita pm siji naogopa vaaagi
 
Halafu virampasi vyako vya sehemu za vilaji... wewe muumini mwenzetu tena dhehebu moja
 
Duuuh..
 
haha..! NYUMBU kweli wewe!
 
Mwanangu una-talent ya kuandka Shigongo aende course

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nooma aseeh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…