Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Hahaha we jamaa umenikumbusha nilivyokesha siku moja hadi saa 11 asubuhi nikazidiwa na usingizi nikakosa pambano la Tyson aiseee
Mi siku ile alivyodundwa na Holyfield nakumbuka tulikuwa kama wagonjwa wiki nzima kijiwe chetu chote hakukaa mtu.Kila mmoja alijifungia nyumbani anaugulia😀
 
Kweli mkuu hebu waambie warudie
 
Mwenye picha angalau ya Time Trax atuwekee hapa wadau
 
Mimekumbuka pia Tangazo la Coca cola la father krismas ITV lilikuwa la msafara mrefuu wa magari ya coca cola nilikuwa nalipenda sana wakati wa krismas
 
Tangazo la Revola da sijui kwanini walilitoa bora hata wangeliacha you tube alikua miriam odemba yule nazani
Hakuna mdau anaeweza kulisaka popote atuwekee hapa
 
enzi hizo epl iko live dtv, hakuna cha king'amuzi wala malipo labda itokee mgao wa umeme ...lakini tv inakuwa moja mtaa mzima!
Nakumbuka ilikuwa bureee kabisaa mkuu
 
Sijui jengua yupo wapi
Jengua yupo mkuu ameludi tena kwenye hizi bongo movie kuna siku nilimbahatisha nilikua kwenye basi naenda moro waliweka movie yake mi huwa sio mpenzi wa bongo movie sana kwasababu utakuta mtu anawaza miaka kumi iliyopita alafu unakuta picha ya magufuli ukutani kama rais
 
Ila ITV wajitahidi warudishe Vioja mahakamani kile kipindi licha burydani kinaelimisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…