Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Jina Halisi ni Jaleel Ahmad White!

Jina la kuigizia "Steve" Urkel!

View attachment 402212
Huyu Jamaa niliaminishwa kitambo kuwa alikufa nadhani hadi Magazeti ya Bongo yaliandika kundei kwake... mida hii nimetizama kwenye wikipedia naona hakuna sehemu inayoonesha kandei na Picha yake ya Mwaka 2010 ipo kuonesha ana miaka 40 tosha kabisakuwa yupo hai.. hivi ule uzushi wa kiba katimiza miaka 40 yaani ni sawa na huyu?

220px-JaleelWhiteDec10.jpg
 
CTN kulikuwa na movie za TCM nilikuwa nakesha nazo!
Mkuu ile channel waliyokuwa wakijiunga mwanzo iliitwa TNT nimezicheki sana zile movie maana ilikuwa haman namna ila nikazizoea na nikawa nazipenda zaidi maana uongo kidogo story kidogo action kidogo hapo hapo unakuta movie ni black and white... kuna movie moja demu wa kizungu kipofu akanogewa kupiga story na jamaa garden like mnazi mmoja kipofu alipokuwa akipenda kupumzika akakutana na mtu wakaelewana mno siku ya siku ndugu za mzungu wakamuambia unaelewana na nigga nigga ni watu weusi na hatari sana lakini kipofu hakuweza amini..

Ila kuna movie ya kichaw mtoto anavutwa kwenye TV niliipenda mno Tawi la Mti linajikunja hadi dirishani si mchezo vitu vyote vya ndani ya nyumba vinanyenyuka na kuelea kama sayari dah inatisha
 
Mtangazaji Bisanya Bingi na O yake kipindi cha music
 
Unakumbuka tamthiria ya the BEAUTY & THE BEAST........yule zimwi aliitwa vicent alikuwa anampenda mdada anaitwa Catherine ( star wa teminator 2 aliyeigiza kama sarah corner mama wa john corner)........nilikuwa naiogopa sana hii tamthiria maana Vicent usoni yupo kama simba.....aisee natamani ITV wairudie.
 
ITV kulikuwa na Tamthilia fulani ya kikenya iliitwa Tamasha, movie flan ya jamaa aliitwa Vicent na alikuwa na sura ya cjui paka cjui simba, cheka na ctn ya kna mzee small,futbol mundial,
Vicent.......ile inaitwa BEAUTY & THE BEAST ......mwanamke alikuwa anaitwa catherine.....yaani ukitaka kukorofishana na vicent akurarue we mguse catherine wake.
 
Aiseee nilikuwa nampenda sana Yule dada aliyekuwa anatutangazia filamu yaani kifuatacho .....alikuwa anaitwa manuel elias kama sikosea.......nilikuwa napenda sana anavyoelezea filamu kabla hawajaweka........nakumbuka sana alipokuwa anaintroduce filamu kama GHOST BUSTERS.....SUPERMAN.......BEATLE JUICE.......aisee those days wacha tu ving'amuzi havikuwapo lakini tulivyo enjoy sidhani kama madogo watainjoy kama sisi miaka ile.
 
Suzan Mungi......Faudhia Taabod.......Hayati John Ngahyoma ( alikuwa sana kwenye habari za biashara)…………… Auntie Tumaini kipindi cha watoto wetu.....nakumbuka katuni ya sonic the hedgehog......captain planet.......the Flistones.......
 
CTN wakat huo nakumbuka ilikuwa jumapili saa nane mchana ilikuwa wanaweka picha za kihind!!akna san deo,bab deo,salman khan nk
walikuwa wananiboa maana muda wanaweka hiyo filamu mdingi anakomaa tuende kanisani misa ya jioni inaanza saa kumi kasoro na wao movie inaanza saa nane na ikianza ni masaa mawili hadi matatu hadi iishe
 
View attachment 402149hivi mnamkumbuka jina huyu jamaa..? ...vichekesho vyake vilikua itv miaka hio sijui vilikua vinaitwaje
The Family Maters.......ninayo hapa kwenye laptop huwa naicheki sana......ha ha ha ha ha anaitwa STEVEN ULCER ........jembe la mr. winslow.....admirer wa Laura binti wa mzee winslow na dada yake Edward.......

Halafu kama utakumbuka vizuri katika episodes za mwanzo katika familia ya mr. winslow kulikuwa na binti mtoto wa familia pale inapoanza utamuona nadhani huyo dada nikaja kujua juzi kati kuwa aliacha kuigiza episodes na seasons zilizobaki kwasababu aliabza kuigiza pornography nadhani ndio sababu ya kusitisha mkataba wa kuigiza ile series.
 
Hyo rinorenz 21jumpstreet umenikumbusha mbali sana ndugu yangu natamani one day virudiwe big up mkuu kwa kunikumbusha ujana
Ile series ilikuwa inaitwa THE RENEGADE......star alikuwa jamaa anaitwa Lorenzo Lamas au Rynorenze.......mimi nilikuwa namwita stering manywele.....yaani bora nikose chakula kuliko kuikosa ili thamthiria.
 
Daaaaaah umenikumbusha football mundal na movie ya Vicent jamaa alikuwaa na kichwa cha simba alikuwa na demu wake mzuri sanaa hivi
Catherine.....huyu dada ndiye aliyecheza filamu ya Terminator 1&2 kama Sarah corner
 
Neighbours ITV ilikuwa bonge la tamthilia
Kabisa sijui kwanini waliikata........namkumbuka sana dogo yule alikuwa anaitwa TOBBY.......na baba yake wanaishi kisela......na jamaa m'moja anamanywele halafu anacheka kama beberu.
 
Alikuwa anaitwa Martin
Wewe acha urongo Martin alikuwa ni acter katika comedy nyingine kabisa ibaitwa THE MARTIN akiwa na demu wake Geena.......rafiki zake TOMY na wakina SHenay nay........Dragon fly joness ( fundi gereji anayejifanya mcheza kareti halafu anachezea kichapo kila akitest mziki wa kupigana na asistant wake ambaye ni professional fighter) .....halafu kuna mzee Otis yeye hapendi dharau kutoka kwa vijana anawatembezea dozi kila wakizingua. Kuna scene moja martin alikutana na michael jackson wacha wapeane kichapo
 
Hanging with Mr. Cooper
View attachment 402157
Perfect strangers
View attachment 402158
Family Matters
View attachment 402159
Robocop
View attachment 402160

Dark Justice
View attachment 402161

Pointman
View attachment 402162

Kwa kipindi hicho local TV zetu zilikuwa na vipindi vizuri sana mtu hata hufikirii kutafuta channel za nje
Kweli kabisa yaani nikikumbuka back in those days huwa najisikia amani moyoni yaani as if ilikuwa ni heaven natamani kurudi those days niishi tena.
 
Nakumbuka CTN walikuwa wanaonyesha sana vipindi vya Cartoon Networks. Enzi hizo hata sijui kama Cartoon Network nayo ni channel.
Nilikuwa naifurahia cartoon network msimu wa Christmas......wanachagua katuni moja halafu inaonyeshwa mfululizo nakumbuka christmas ya 1997 kama sio ya 1998 ilichaguliwa DEXTER's Laboratory........John Bravo......the Jetsons.....Looney tunes.....top cat......tom & jerry....ed,edd & eddy........
 
John Black, Marlena Evans, Bo brad,Bill, Stefano Dimera,Jenifer, Victor Kiriakis,Hope,Austin,Christina Dimera,Sami Brady,Lucas nk...Haki ya nani ulikuwa hunitoi sebulani ikishaanza
Mzee Dimera alikuwa ananiudhi yaani kila john black akitaka kumkamata anafanikiwa kumtoroka.........alikuwa anampenda Marlena mama yake Sammy na Carry......baba yao alikuwa rafiki na john black. Vivian Demu wa dimera.
 
Back
Top Bottom