Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Nawakumbuka watangazaji kama kina Misanya Bingi,Sunday Simba Shomari na John Delinga Marklow wakihudumu ITV na Radio one,bila kumsahau Othman Njaidi.
John Delinga saizi anapiga maflash back pale legency yupo na DJ Fast Eddie wapo vzr sn
 
Ephraim kibonde habari za michezo CTN, mzee majuto marehem mwanachia DTV, waridi, Aisha, sumbi, bocha, bishanga, the robocop, urban angel, uefa itv, epl dtv,
Daaah umeweka udambwi wooote hahha afu EPL ilikuwa bure aisee
 
DTV-kipindi cha vichekesho,marehemu mwanachia alikua na kigugumizi kikali ile mbaya akiwa na the legend king majuto..........
 
Nimekumbuka Cheka na CTN

Mzee small, tupatupa, bi chau.

Kingine ninachokumbuka haswa ni tangazo la sabuni ya Kodry, jamaa alikuwa anaenda kuosha ugoko wa mguu bombani na sabuni yake ya Kodry.

Kulikuwa na tangazo la magari aina ya Musso.

Aisee kumbe na mimi ni muhenga eee.

Kipindi hicho mwaka 1994 nilikuwa kila nikiangalia taarifa ya habari ITV nilikuwa naona habari za wakimbizi wa Rwanda tuu. Nikawa namuuliza mdigi, Baba hawa watu kila siku wanaoneshwa wanatembea tuu hawafiki huko wanakoendaa..??

DTV nilikuwa naipena picha ya Mr T, na ITV walikuwa na movie series ya Renegade staring akiwa Lorenzo Lamas kama sijakosea, huku Kukiwa na movie series nyingine ya Michael night, humu gari ilikuwa inatumwa kama binadamu. Hahaaah.
 
Back
Top Bottom