Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Foma iloyona powerfom plus je gladness wa kesho ana yapi ya kusema
'Inatia muujiza sabuni kidogo tuu inafua nguo nyingi.................hili tangazo likinivutia sana enzi hizo
 
Ile tamthilia imewaharibu sana Bongo Movie hadi kesho! Kwavile kwenye geti la mmoja wa wale Characters (sijui kwa akina Mjiba vile, ckumbuki) kulikuwa na mlinzi mchizi chizi basi hadi kesho walinzi wa magetini kwenye Bongo Movies ni machizi chizi...
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
yani naitafuta sana kampuni ya waliotengeneza lile tangazo la revola na Air Tanzania enzi hizo wanaimba kilimanjarooo kilimajaroooo basi anapita twiga so nice hii nchi nani sijui kaiharibu zamani mambo yalikua safi sana
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
Perfect stranger we acha tu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent from my HTC Desire 626GPLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
Hahaha umenikumbusha sana akina mzee small, bi chai, tupatupa
Na kenya walikuwepo masakuu, mama kayayi, masanduku, mzee ujwango, makanyaga...
Wote hao walikuwepo yani ilikuwa full raha walikuwa wanachekesha sana tofauti na miaka ya hivi karibuni aisee
 
hawa jamaa kuna siku waliweka katuni kuanzia asubui mpaka jioni siku iyo sikutoka nje ni kula katuni kwa kwenda mbele
Hahahhahha yaelekea hata kula hukula siku hiyo
 
Kwenye DTV tangazo bomba lililokuwa linanivutia ni lile Tangazo la sabuni ya Komoa,jamaa ananawa miguu.

ITV kuna mchezo makini sana wa wakenya ulikuwa unajulikana kwa jina maarufu la HASSAN NA HUSNA. Mtoa uzi wakati huo nina hakika hujazaliwa ww na hata kama ulizaliwa bas ulikuwa bado unavaa nepi. Kama unabisha niambie mwanachia alikuwa anaekti mchezo gan?
Hahhahahha mwanachia daah unajua kitambo ila jina nalikumbuka sana aisee mie mhenga mkuu mfano world Cup ya 1994 niliiangalizia itv enzi hizo bado kinda
 
Ile tamthilia imewaharibu sana Bongo Movie hadi kesho! Kwavile kwenye geti la mmoja wa wale Characters (sijui kwa akina Mjuba vile, ckumbuki) kulikuwa na mlinzi chizi chizi basi hadi kesho walinzi wa magetini kwenye Bongo Movies ni machizi chizi...
Hahhahhaha yani hakujawahi bongo movie kuwa na mlinzi ambaye sio chizi yani wote machizii
 
Foma iloyona powerfom plus je gladness wa kesho ana yapi ya kusema
'Inatia muujiza sabuni kidogo tuu inafua nguo nyingi.................hili tangazo likinivutia sana enzi hizo
Dah umenikumbusha Gladisi wa kesho mama flani hivi wamakamo tangazo nalikumbuka sana lile
 
yani naitafuta sana kampuni ya waliotengeneza lile tangazo la revola na Air Tanzania enzi hizo wanaimba kilimanjarooo kilimajaroooo basi anapita twiga so nice hii nchi nani sijui kaiharibu zamani mambo yalikua safi sana
Huwezi amimi tangazo la revola nalitafutaga hadi kesho, itv sijui walilifutaga? Nimelitafuta hadi you tube bila mafanikio daaah lilikuwa zuri sanaaa
 
ntamwambia dogo mmoja yuko itv anichekie kwenye library yao kama watakua na haya matangazo nilikua nayapenda sana
Hebu mwambie huyo dogo alisake tangazo la revola ulitupie humu mkuu, tutakuzawadia zawadii
 
Back
Top Bottom