Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

0f3a58970e6c277e4c6bd30c04caa38e.jpg
a57f35a72de6558d503f63d3c50989da.jpg
Lugendo hii nilikuwa movie gani mkuu
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
[emoji23] [emoji23] Utawajua tu Wakongwe ktk ubora wao... Watu adimu wako mbioni kutoweka... Hii ni hazina kubwa mkuu kuwa na watu kama ninyi for reference.... Tisha sanaa.
 
umetisha mwanangu
me napenda movie ya V
journey to west AKA SHIVOOOOO
QUEEN OF SOAD
THE CROW
BEAST MASTER
KARTOON YA POPEYA JAMAA ANABUGIA VITU FLANI ALAFU ANAVIMBA MIKONO NA MIGUU HAHAHAAAAAAA
 
hivi africa journal iliishiwa wapi ilikua saa moja itv enzi izo yan kama ujaoga uangalii tv
 
Nakumbuka ITV kulikuwa na vipindi vya mpira vya Italian football na football made in German.
 
hivi ile movie ya V ikiitwaje maanaa since wayback naisaka siioni
Hii movie bana ilikuwa na ma character ambao wananyofoka ngozi ikivutwa tuu inatoka yotee then damu ya mwilini nilikuwa yakijani tuu. Aidha walipenda kuvaa nguo rangi nyekundu na kusafiri kwenda angani kwa mtambo kama sahani hivi. That's V
 
[emoji23] [emoji23] Utawajua tu Wakongwe ktk ubora wao... Watu adimu wako mbioni kutoweka... Hii ni hazina kubwa mkuu kuwa na watu kama ninyi for reference.... Tisha sanaa.
Hahaha mkuu hatutaki kizazi chetu kumbukumbu zake zipotee hivihivi. Hii ni hazina tofauti na miaka ya 90's mkuu. Mimi wa 80's ktkt humo hatuwezi kusahau uhondo wetu
 
Channel 10 kulikuwa na movie ya Mr T na Knight Rider (maarufu kama maiko, maiko - jamaa ana gari lake hilo lina fujo balaa) pia kulikuwana igizo la kutisha lilikuwa linaitwa Mmsai na Ng'ombe Wake

ITV kwanza picha linaanza matangazo yanafunguliwa saa 12 jioni hadi saa 6 usiku, walikuwa na vichekesho vya Perfect Strangers, Hang in with Mr. Cooper pia kulikuwana movie ya TimeTrax, Beast Master, Pointman na kipindi cha Jackpot Bingoooo!!!

Dah kulikuwaga raha sana.
 
Hii movie bana ilikuwa na ma character ambao wananyofoka ngozi ikivutwa tuu inatoka yotee then damu ya mwilini nilikuwa yakijani tuu. Aidha walipenda kuvaa nguo rangi nyekundu na kusafiri kwenda angani kwa mtambo kama sahani hivi. That's V
Kwa mbaali hiyo kitu nadhani ilikuwa inaonyeshwa jmosi mchana kabla ya fukoto/radi kwenye 1999, dizain hizo pipo wengine walikuwa na ngozi kama ya chui hivi.. enzi ya marehemu Nasma khamis kidogo na mtu mzima hovyo on fireee!..
 
Back
Top Bottom