Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Hii ndio ya yule bibi mchawi?


Yeah, bibi tabitha na timmy, ila timmy alikuja kufa akapata mtoto nae alikuwa kiziwi but mwenye maajabu, akaungana na kay but kay uchawi wake ulikuwa ni mzuri na akamshawishi tabitha aache uchawi amrudie mungu, mwisho kabisa tabitha anabatizwa halafu yule mchungaji kipofu anakuja kuona, anaponywa na kay ambaye anaolewa na miguel wa charity
 
Tusisahau na kipindi cha mapishi pamoja na kile cha hawavumi Lakin wapo.
 
Hyo rinorenz 21jumpstreet umenikumbusha mbali sana ndugu yangu natamani one day virudiwe big up mkuu kwa kunikumbusha ujana


Rinorenz ilikuwa ni jumatano saa tatu na nusu, jamaa kafanana na NICO alikuwa anapiga sana mkono na pikipiki yake
 
Ni mengi na pia nimepoteza kumbukumbuku ila E. Kibonde akiwa CTN mtangazaji wa habari za michezo, alikuwa so creative katika utangazaji. Alinifanya nipende soka na zaidi soka la Hispania na Italia.
 
Naitafuta sana hii tamthilia iliishia wap?

Je mtandaon ipo kweli


Ingia youtube andika the passions full episode 1

Itakuja episode ya kwanza na ukiifungua automatically itakuja na ya pili kama next to watch, ukiifungua ya 2 ya tatu itakuwa next to watch, hivyohvyo, YouTube ipo full pia unaweza angalia kama season, unaandika passions season 1,then ukimaliza unaandika passions season 2 na kuendelea

You are the fire burning inside of me, you are my passions for life
 
Sijawahi kutazama telenovela za ukweli kama Camila na La muje de Lorenzo,tangu hapo sijaangalia tena,kwa matangazo la jambo lotion lilitisha...na wewe je? Mimi naitwa jambo doogoo


Kulikuwa na lamujer de mi vida, wakina barbaritha na katyuska acha kabisa
 
Back
Top Bottom