Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Hapa nipite kimya kimya tu mana tv yenyewe ya kuvizia kwa watu enzi hizo utakachokuta ndicho utakachoangalia
Inamana hata kipindi kimoja hicho cha kuvizia hukumbuki kilikuwa nikipi mkuu?
 
Hiyo CTN tunaijua wahenga tu na kisha tuliokulia jiji la Makamba wa mkoani TV zilikuwa ndio zinanusa.Hata humu wa mkoa watakumbuka ITV tu na kidogo DTV.
CTN jengo la SUKITA kitambo kidogo,kwa akina Ephraim Kibonde?
 
Dah! Nakumbuka kipindi hicho 95, 96, 97 niko primary tunafuga ng'ombe wa maziwa kila jioni natumwa kupeleka maziwa kota za Tiper kigamboni, home kwetu hakuna umeme tunatumia generator linawashwa saa mbili usiku hadi saa nne, so nikitoka mida ya saa moja kupeleka maziwa nilishachagua nyumba moja wenyewe hawana longo longo inakuwa ya mwisho nikifika nawakabidhi maziwa yao halafu nasimama hapo kucheck tv hapo ndio nilipoanza kuona isidingo, ikiiasha faster na baiskeli yangu nawahi home nakuta generator imewashwa nacheck news itv. Maisha ni safari.
 
Kuna vipindi kama Egoli, Hiki kipindi kilikuwa kinarushwa ITV, Ni kama isidingo ya sasa. Pia kuna Channel ilikuwa inaitwa ITV2 kwasasa nadhani ndio Channel 5, hii channel ilikuwa ni miziki tu tena ya Mbelembele.

Vipindi vya Maigizo kilikuwa kinajina sana kilikuwa Mambo hayo, waigizaji wake walikuwa wakina Bishanga, Aisha, Waridi na Rich mtambalike.

Enzi hizo channel bomba ilikuwa ITV kwa maigizo, hakuna bongo movie kabisa. Na mastar wa Movie bongo nzima hawakuzidi 15.

Mtaa mzima Tv ziko mbili, Vipindi vya michezo watoto mnajazana kwa jirani hadi kero kwa mwenye nyumba.

Ilivyo ingia miaka ya 2000, Ndio wasanii wengine wakaanza kuibuka kama wakina Muhogo, Mchungu, Cheni, Nyamayao, kibakuli, Bi hindu etc.

Sijui kwann ITV hawairudii hii michezo ya zamadi katika tasnia ya uigizaji, Ingetuburudisha sana sisi wahenga.
 
Jumamosi itv walikuwa na hekaya za journey to the west a.k.a brother monkey sun wukong, zhu bajie nguruwe na master shifo hsuan tsan. Pia katuni za kina john quest, silver hawks na popeye the dreamer.

Nakumbuka pia tangazo la michael power na katili hekta dekta kama movie flani hivi ya kuitangaza bia ya guiness

Kule ctn na ndugu yake cen katuni network kila saa kumi jioni. Tangazo la tritel watu wamebeba bonge la simu.

Dtv tulikuwa tunaona ligi ya uingereza kila wiki mchambuzi dakta leakey stori nyingi. Pia kulikuwa na vitimbi vya mzee majuto, mwanachia, mangushi na gladys zipompapompa
Bila kusahau DTV walikua wanaonesha mieleka ya kina hulk organ na sting
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.

Isidingo the need , na bado kitu kinawasha moto hatare
Egoli, the place of Gold. Hii ndiyo ilianza kwanza halafu ndiyo Isidingo ikafuata!
 
Days of our lives, mtangazaji namkumbuka Rahma azizi, tangazo la mwanachia la mafuta ya korie mafuta bora ya kupikia, jaman nimeamini Old is Gold

Hii nilikuwa naangalia yote weekend wakati wa marudio, maana weekdays lazima uwe shule. Kulikuwa na SOLID STATE PHYSICS enzi izo ya Dr. Kashinje. Nawakumbuka wahusika hadi leo km akina mzee Victotr Kirikisi, Stephano, Marlena, Carry, Sami, Lucas, Bo Brady, John Blake, Mzee Roman (mume wa marlena) Hope Brady.... ilikuwa enzi hizo za ujana wetu

Naona kama bdo ipo ila wahusika wote kama walishabadilika, sura zote ngeni sasa hivi

Watch Days of our Lives Episodes - NBC.com
 
NIMEANZA KUANGALIA TV 1999 KWA MAZISHI YA NYELELE TENA KWA JILANI MTAA WA 4 KUTOKA KWETU HAHAHA ZAMAN BHANA
 
Africa Bambataa!! hiki kipindi mtangazaji wake alifariki (Redio one) eti siku ya msiba mademu zake wakawa wanagombana msibani (wanamgombea mtu ambaye keshafariki) hahahahahah
 
unaangalia stesheni kwa sasa / nina kingamuzi cha azam ni steshesheni gani naweza angalia days of our lives
Hii nilikuwa naangalia yote weekend wakati wa marudio, maana weekdays lazima uwe shule. Kulikuwa na SOLID STATE PHYSICS enzi izo ya Dr. Kashinje. Nawakumbuka wahusika hadi leo km akina mzee Victotr Kirikisi, Stephano, Marlena, Carry, Sami, Lucas, Bo Brady, John Blake, Mzee Roman (mume wa marlena) Hope Brady.... ilikuwa enzi hizo za ujana wetu

Naona kama bdo ipo ila wahusika wote kama walishabadilika, sura zote ngeni sasa hivi

Watch Days of our Lives Episodes - NBC.com
 
Back
Top Bottom