Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Walikuwa wanaunga TNT, hapo lazima watu wapigane mikasi
Halafu hawaweki viboksi viboksi vya kuziba. Ila kuna mdada akaniambia ukiweka kitambaa cheusi usoni unaona kila kitu.
 
Zile tamthilia za mida ya kubeti, akina Barbarita, Tony, Marcidita, Theresita......daaah watoto wa Kilatino wakali saana. Mambo ya Copa Cabana.
.......Acapulco Bay ! Daah walatino wazuri jamanii !
zamani life was so good
 
Hiyo CTN tunaijua wahenga tu na kisha tuliokulia jiji la Makamba wa mkoani TV zilikuwa ndio zinanusa.Hata humu wa mkoa watakumbuka ITV tu na kidogo DTV.
CTN jengo la SUKITA kitambo kidogo,kwa akina Ephraim Kibonde?
Sio jengo LA SUKITA, jengo la USHIRIKA kule juu ROOF GARDEN, meneja mwanzilishi KARIM, Afisa Usalama marehemu MPAPAI rip
 
Kuna vipindi kama Egoli, Hiki kipindi kilikuwa kinarushwa ITV, Ni kama isidingo ya sasa. Pia kuna Channel ilikuwa inaitwa ITV2 kwasasa nadhani ndio Channel 5, hii channel ilikuwa ni miziki tu tena ya Mbelembele.

Vipindi vya Maigizo kilikuwa kinajina sana kilikuwa Mambo hayo, waigizaji wake walikuwa wakina Bishanga, Aisha, Waridi na Rich mtambalike.

Enzi hizo channel bomba ilikuwa ITV kwa maigizo, hakuna bongo movie kabisa. Na mastar wa Movie bongo nzima hawakuzidi 15.

Mtaa mzima Tv ziko mbili, Vipindi vya michezo watoto mnajazana kwa jirani hadi kero kwa mwenye nyumba.

Ilivyo ingia miaka ya 2000, Ndio wasanii wengine wakaanza kuibuka kama wakina Muhogo, Mchungu, Cheni, Nyamayao, kibakuli, Bi hindu etc.

Sijui kwann ITV hawairudii hii michezo ya zamadi katika tasnia ya uigizaji, Ingetuburudisha sana sisi wahenga.

Kuna jamaa alikuwa anaitwa Bijampora, alikuwa anapewa shavu na kina Bishanga siku moja moja.

Hivi Monalisa na Mama yake waliingaje kwenye ITV, hawakutokea Mambo hayo kweli?
 
Zile tamthilia za mida ya kubeti, akina Barbarita, Tony, Marcidita, Theresita......daaah watoto wa Kilatino wakali saana. Mambo ya Copa Cabana.
.......Acapulco Bay ! Daah walatino wazuri jamanii !
Ahaa kuwapata ni ishu sana mkuu
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
Duh kweli we mhenga
 
Back
Top Bottom