Tukumbushane Wachagga waliowahi kusakata kabumbu kwa kiwango cha ligi kuu bara

Wachaga na mpira wapi na wapi hamna kitu wale sifa tu na mipesa ndo mana kaskazin hamna timu ya mpira inayoeleweka
 
Wahenga watamkumbuka LYIMO wa TPC miaka ya 1960's akichezea TPC na Kilimanjaro Sunlight /Taifa Cup na Nafikiri Tanzania.
Tena nilisahau kumtaja, John Lyimo. Alikuwa hatari sana huyu Mangi.Sikuwahi kumshuhudia ila niliwahi kumsoma wasimu wake kwenye gazeti la Dimba la miaka ya tisini. Kulikuwa na ukurasa unaoitwa "ALIYEBOBEA" hutoa wasifu wa wachezaji mbalimbali.Kipindi hicho liko chini ya jenerali Ulimwengu, Habari Corporation yenyewe ile. Kuna mtu kama Johnson Mbwambo n.k. Ilikuwa lazima nibane shingi mia ya kununulia Dimba kila wikiend.Sio hili la sasa linaloandika Ugoro tu kila siku.
AJABU MNAPIGA KELELE, HATA KIPA WENU MMEMSAHAU?!!!!!!!
Deogratius Boniventura Munisi"Dida"
Babu Ally "kama sijakosea"
 
tupa kule!@&* eti aliona nyomi akaenda kuuliza getini kuna shilingi ngapi!!! mbavu zangu mimi ahh h
 


teh teh teh teh teh teh teh teh 😀 😀 😀 😀
 
Kuna mchezaji alikuwa anaitwa elisha John huyu alikuwa hatari Sana. Alichezea costar union baadae yanga alikuwa ni hatari sana mtaalamu WA dimba la Kati. Masawe kwa elisha ni Mtoto kimpira
 
Thomas Lema wa huku duniani hakika wachagga tumesambaa kila kona na kila idara.
 
Bahatisha Ndulute alikuwa goalkeeper was Ushirika
 
Ingawa sina uhakika lakini ninavyojua Bobani ni Mnyamwezi

Ukoo wao wamekulia Tabora mzee wao marehemu kwa sasa alikuwa 'TT' Wa train ya kati lkn nafikiri asili yao kabisa ni Kigoma na kwa Tabora walikuwa wanaishi mtaa wa Bachu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…