Tukumbushane wahenga vitu tulivyonunua enzi hizo na bei zake

Tukumbushane wahenga vitu tulivyonunua enzi hizo na bei zake

Marahaba, hujambo? Nakupa na hii! Zamani ilikuwa raha sana, unakula nauli unakwenda kuvizia mabasi ya kampuni za Tanzania Bag (Magunia), Breweries, Kibo Match au Bonite, yalikuwa hayaachi mwanafunzi
Hahahaa sijambo babu. Kweli hii kitambo sana, sasa hivi mambo yamebadilika sana.
 
Lah kweli zamani raha
Huku ambako sasa kuna parking za magari kwenye uwanja mpya ndiko foleni ilikuwa ya hatari, ukikata tiketi yako kuingia kuna mageti 3.

Moja huku linatazama indoor stadium kuingia mzunguuko ambako mnakaa mashabiki wote mnachanganyika Simba/Yanga .

Hakuna kusumbuana, mambo ya utofauti ni jukwaa kuu na jukwaa la kijani ambalo nalo kwa kiasi kikubwa likikuwa linatawaliwa na Yanga.
 
Baba yangu aliniambia walkua wanauza ng'ombe sh 60.
Alinunua baiskeli sh 40. Alkua mtumishi wa jeshi la muingereza
 
Ada shule ya sekondari day 2,500 na boarding 4,000 ikapanda 5,000 kwa 8000 kabla ya kuwa 15,000 kwa boarding baadae. Hakuna kuchangia nini wala nini ila nilichokuwa nakumbuka gharama ya msosi unaokula kwa mwaka ni zaidi ya ada
 
Enzi hizo tunasoma madaftari tunapewa bure shuleni yana chapa ya sungura likiisha unapeleka kwa mwalim anakupa jingine ada sh 200
 
Back
Top Bottom