Jamani jana nilikuwa naiona thread hii na kuipita lakini leo imenikumbusha mbali sana hongera Balantanda nimekuvulia kofia......
kuna wimbo mmoja sijui kama mmeutaja... Kosa la mesenja....sijui uliimbwa na nani.....
messenger alipotoka posta ofisi ikawa imefungwa akaipeleka barua nyumbani kwa bosi ila bosi hakuwepo akaipokea wife... alipoifungua maandishi yakawa yamelalia kushoto... ikawa kasheshe sijui mnaukumbuka, Balantanda, Sikonge nisaidie beti zake.
Wimbo huu uliimbwa na
Maxmillan Bushoke akiwa na
Bima Lee Orchestra wana Magnet Tingisha,ni wimbo mzuri sana maana ulikuwa kama jamaa anwahadithia watu stori flani hivi.....
Wee Mesenjaa,hallow Sekretari(naam bosi) Mesenja yuko wapi(sijui bosi)
Mara Mesenja anaitika naaam bosi nilikuwa uani tumbo linaniletea matatizo mimi
Nae bosi anasema nenda Post office kachuke barua za ofisini na za nyumbani,za ofisini leta ofisini na za nyumbani peleka nyumbani
Kama inavyoeleweka kazi ya Mesenja ni kutumwa Posta au ofisi za nje na shughuli nyingine zinazohusu kutumwana kiofisi(rudia tena)
Mesenja kaleta balaa nyumbni kwa Meneja bila kufahamu(Mesenja kaleta balaa nyumbani kwa Meneja bila kufahamu)
Wakati anakwenda Post office anawaza moyoni mzee mie darasa la 3 la mkoloni nyumbani mke wangu na watoto wangu wamelalia ugali wa muhogo na sunga la kuchemsha jana,kutoka Post office kapitia Kariakoo,kaingia mitaaani anaikimbiza mia wakati siku hizi mia imeota matairi Mesenja hajatahamaki ni saa 7 na nusu wakati osisi zinafungwa saa 6 na nusu mchana
Mesenja kaleta balaa nyumbni kwa Meneja bila kufahamu(Mesenja kaleta balaa nyumbani kwa Meneja bila kufahamu)
Kakimbilia ofisini kakuta ofisi imefungwa na mlangoni yupo mlinzi kajaribu kumbembeleza zile barua akakataa akaamua kuzipeleka nyumbani kwa bosi wake alimkuta mkewe bosi na kumpa zile barua za ofisini na za nyumbani,mkewe bosi kapokea zile barua akaamua azitazame zile za ofisini kwa kuwa si desturi barua za ofisini kufika nyumbani katazama kaweka kando,katazama barua nyingine anuani maandishi yamelalia kushoto,hati kama ya kike akaamua aifungue na akakumbana na neno Darling kama kichwa cha habari na baada ya kuisoma akazimia nusu saa maskini
Siri imefichuka siri imefichuka kosa la Mesenja kaleta balaa kosa la Mesenja kaleta aibu(Siri imefichuka siri imefichuka kosa la Mesenja kaleta balaa kosa la Mesenja kaleta aibu)
Alipozinduka akamkuta mwanae mdogo amamuegemea analia mama nasikia njaa,alimjibu subiri baba ako aje apike,mimi leo sipiki sipakui,analia akisema mimi Baba Kulwa nimemtendea nini mie jamani eee,haya kamjengea nyumba ya ghorofa na gari kamnunulia huyu Darling jamani
Siri imefichuka siri imefichuka kosa la Mesenja kaleta balaa kosa la Mesenja kaleta aibu(Siri imefichuka siri imefichuka kosa la Mesenja kaleta balaa kosa la Mesenja kaleta aibu)
Bosi siku hiyo karudi saa 6 na nusu za usiku kichwani ana moja moto moja baridi,kubisha hodi aanza kushambuliwa na maneno,kalale huko huko kwa hao unaowajengea majumba na kuwanunulia magari,ilibidi bosi abembeleze alipoingia ndani kataka tu kumgusa mkewe kidogo,alipigwa kibao na zogo kubwa likaanza,mara maneno,mara kavutwa koti,mara kachaniwa shati...Mesenja kaleta aibu jama
Siri imefichuka siri imefichuka(imefichukaaa) kosa la Mesenja kaleta balaa kosa la Mesenja kaleta aibu(Siri imefichuka siri imefichuka kosa la Mesenja kaleta balaa kosa la Mesenja kaleta aibu) kaleta aibuuuu