Tukutane hapa ambao hatuna mpango wa kuoa kwa Me au kuolewa kwa Ke

Tukutane hapa ambao hatuna mpango wa kuoa kwa Me au kuolewa kwa Ke

Hii sio sababu, ukiumwa kiasi cha kushindwa kujihudumia huna tofauti na mfu kwahiyo aibu haipo yeyote anaweza kukuhudumia.
Kuna Balozi mmoja anaitwa alipopata kiharusi alirudi kijijini akamuacha mke wake na watoto Dar. Sijui kama bado yupo huko ila Nzee Nkapa huwa anaenda kumjulia khali. Kuoa hakukufanyi upate ntu ya kukusaidia ukiwa na matatizo hasa kama alishakuona na mchepuko sahau.
 
Mi kinachosababisha nishindwe kuoa ni mahari tu ile, hivi kwanini watu tunapendana tumekubaliana kwa mapenzi yetu tuishi wote wewe mzazi unasema hadi nikupe milioni moja na laki tano?

Ama tutoroke kama hautaki baki kwa wazazi wako.
Sasa hivi mahari imepanda bei kidogo..ni milioni 2 mpaka 3.

Ukijumlisha gharama za harusi na za kuanzia maisha: unaishia kuumiza kichwa na huzuni.

NB: Wazee watupunguzie mahari ili vijana tuoe
 
No matter what ndoa ni muhimu nikimwangaliaga na mkubwa ambaye hakuoa ana maisha ya shida hana mbele wala nyuma licha ya kuwa kwenye nyazifa nzito, kuwa na familia muhimu utajijenga nakufanya ya maana
Kwelii hata uwe na kila kitu familia ina umuhimu wake
 
Sina mpango wa kuoa ..na wala silifikirii hilo "".. naona kabisa kuwa waliokuwepo nje ya ndoa ndio watu ambao wana enjoy mnooo maisha "" ....no stress "" hakuna kusumbuana"".... nafurahia kuwa hivi nilivyo ndoa zimekuwa kama kigenge cha wahuni " "kila siku tunasikia Fulani kamuua Fulani " ambaye alikuwa ni Mume au mkewe...""" sitaki kujiingiza kwenye huo Mkumbo "" kwa miaka hii ya sasa sifikirii hilo kabisa ...labda kuna ambacho kitakuja kunibadilisha hapo baadae ""... na siombei hilo litokee
Acha uoga wewe
 
Sasa hivi mahari imepanda bei kidogo..ni milioni 2 mpaka 3.

Ukijumlisha gharama za harusi na za kuanzia maisha: unaishia kuumiza kichwa na huzuni.

NB: Wazee watupunguzie mahari ili vijana tuoe
Kwanza karibu tena pili mi naona gharama za mahari zifutwe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Na watoto pia hutaki kwahiyo?
Hahahaa Watoto na hitaji " lakini wapatikane nje Ya ndoa " mkuu....wawili tu wanatosha"" sihitaji kuzaa watoto wengi kama adamu au nuhu "" sina mpango wa kuanzisha taifa langu ""...
 
Kwanza karibu tena pili mi naona gharama za mahari zifutwe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Shukran kwa ukaribisho.

Zikifutwa kabisa watu watakosa maumivu na upendo utapotea kabisa
 
Haya mambo ya kwenda kumtambulisha mchumba halafu unakuta wadogo, kaka au washikaji zako washawahi pita nae ni tabu sana, me sidhani kama ntakuja oa kwa kweli.
 
Mwanaume kuoa ni lazima

Mwanamke kuolewa hua ni majaliwa

Mwanaume kunaumri ukifika automatically unaanza kuitaji kuoa iwe kwenye shida au furaha

Watu wasioa au kuolewa hua na STRESS nyingi

Kwanza kuoa kunaleta heshima,kunakushape automatically unakua mtu mzima,mwanaume alieoa hawezi kuvaa mlegezo,kunyoa viduku,

Ni bola uoe muachane ndo uendelee kua bachela ila sio kukimbia kuoa huo ni uoga na kutojiamini

Japo bado nipo nipo ila b4 uchaguz ujao liwe jua iwe nvua lazima nianze kua na family

blessed
Dogo Janja, Blue, mbona wanafanya ubishoo kama kawa na wameoa
 
Kuoa wengi tumeshaoa japo mabachela, sema kuishi na mwanamke ndio hatutaki kwasababu za umasikini na uoga wetu wa kuyakabili maisha ya ufugaji wa mwanamke nyumbani!
 
Huku kwetu Kwamtogole kuna bibi mmoja aliitwa Bi Lilian, hakuwahi kuolewa wala kujaliwa mtoto. Aliishi kwenye chumba cha kupanga. Baadae sana watoto wa kaka zake walimnunulia nyumba mitaa hii hii.

Akiugua mwenyekiti wa mtaa anaitisha kikao na watu hupeana zamu ya kwenda kumuona, kumpeleka chakula na kumbadilishia nguo.

Alivyokua na mdomo mrefu akitoka hospitali alikuwa anasema “kumbe mama Ashura anapikia kuni? Chai yake ilinishinda inanuka moshi”.
Bi Lilian alikufa kipweke sana.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom