Tukutane hapa tuliowahi kutoa na kupewa talaka, tujadili maisha baada ya talaka

Talaka ni mbaya sana


Hivi majuzi nimeona mtu akifilisika kabisa baada ya talaka.

Sasa hivi anasambaza hizi bidhaa za GNLD.
 
Mkuu usipende kuandika majina ya ndgu zako kwenye mali zako iwe wamejua au hawajajua, kama una watoto waandike watoto sababu haohao ndgu wanaweza kukugeuka kabla hata hujafa au ukiondoka hapa dunian hakuna atakaejua hata kumlipia mwanao ada wala kumsaidia. Yunaona sahv watu wanalia sana ndgu wamewafanya ndivyo sivyo, utataman bora ungemwamdika mke au watoto kama humuamin mke wako

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
 
Duuh ya kweli haya?

Kwahiyo we umeoa na watoto, yy kakosa?
 
Huyo hawezi kuinuka tena...unless akuombe msamaha wa dhati
 
Ameshaolewa, ila alianza kwanza kuzalishwa nje ya ndoa then jamaa nd kamuoa, after two years akampa talaka lkn wakarejeana so wapo wte na watoto wa 2,na mm pia nmepata watoto wa 2.hatuna mawasliano japo wte tunatoka kijiji kimoja
Nashukuru kwa majibu mazuri, nakushauri kuwa karibu na watoto wako ili sumu za wamama zisikuhairibie.Jitahidi kuwaunganisha watoto wako.Tukionana tutaongea zaidi mkuu.
 
Nimejaribu nimeshindwa kabisa... Ingewezekana kama mke angekua tayari kujishusha kuliko kuharibu aharibu yeye na ubabe (kiburi) afanye yeye... Kifupi kama kwao watoto wakike kuanzia mama yao ndoa hazidumu mi ni nani niwaweze kudumu nae?
 
Bora kukaa mbali mbali kuliko talaka. Kukeep distance haithiri watoto, upepo ukipita mnaungana tena kwa faida ya watoto. Zipo ndoa zinadumu kwa wawili kuwa mbalimbali.
Madhara ni yale yale... Unadhani watoto hayatowaathiri hayo mazingira?
 
Ukweli ni kuwa hapo palipofikia ni bora na hekima zaidi kila mtu akatafute sehemu inayompa FURAHA na AMANI kwani hakuna na hakutakuwa na mwanaume ataishi na mwanamke mwenye KIBURI||JEURI||na ASIYEKUBALI KUSHINDWA__Na ni mwanamke ndiye awezaye KUITUNZA na KUILINDA NDOA YAKE[emoji848]...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona sheria ya ndoa iko wazi kabisa. Kila mwana ndoa anaweza kumiliki mali zake binafsi. Ni suala la kuwa muwazi tu. Na hakuna kitu kama 50/50 mahakamani. Mimi siwezi eti kuandika majina ya ndugu zangu kwenye mali zangu, kwani wamezitafuta wao. Tatizo binadamu tuna tamaa mtu unaingia kwenye ndoa umemkuta mtu na mali zake halafu unataka ziwe zako.

Kuna dada mmoja kahangaika mahakamani miaka anasubiria mgao, hadi anashindwa kufanya shughuli nyingine. Kosa alilolifanya ni kuwa na boyfriend waziwazi wakiwa wametengana vyumba huku kesi iko mahakamani. Mwisho wa siku hakupata kitu. Sasa hivi kutwa kuongozana na boy friend . Yaani mtu una watoto 3, badala kuwa buzy na wanao unahangaika mtaani.

Kuna mwingine walitengana, mwanamke akahama mkoa. Watoto mpala leo hawajui kinachoendelea, likizo wanaenda kwa mama yao. Mkiwa na watoto ni bora kuangalia maslah yao kwanza maana hata ukiolewa au kuoa kwingine watoto ndio watapata shida. Ni wachache ndio wanabahatika kupata watakao kubaliana kuishi na watoto wa mwenza bika ubaguzi
 
Mahakama inaweza kuvunja ndoa ya kikristo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…