Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] hii kali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka fulani nakumbuka majambazi yalifunga mtaa wetu tulipokuwa tunaishi!.. Jamaa walivamia nyumba ya jirani kwanza walipiga risasi kama 2 angani na 1 wakaua mbwa then wakaingia ndani ya nyumba.
Walimchukua mzee mwenye nyumba na familia yake wakawafungia chumba kimoja then wakaanza hamisha samani za sebureni kama zao, nje wamepaki canter kabisa hapo mvua inapiga balaa.
Kuna mjeshi flani alitoka ulevini sasa njia ya kuelekea kwake lile canter likawa limeziba, akawa anapiga horn walitoe, akapiga moja angani alipoona wasumbufu. majamaa ndio kukimbia, yakaacha canter lao!.
Sasa yule mjeshi akaenda gonga kwa yule mzee anatukana kinoma inakuaje wanahama usiku, ndio wenye kujiweza tukaanza toka!.Kumbe mtaa mzima ulikuwa macho upo kimyaa unaangalia sinema!.
Kesho yake ikawa story ya mtaa ulevi wa mjeshi ulivyookoa mtu kugeuka masikini!. Sidhani kama ile familia watamsahau yule mzee mjeshi!.. Watu tukawa tunajiuliza wale jamaa wangeact kulitoa lori lao njiani yule mjeshi angekuwa mjinga wa mtaa.
Glory to God

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv ukiwa na bastola ndani na risasi za kutosha tu,,na hawa majamaa yanakuvamia nao wanabastola,,hiii bastola ya ndani inaweza kuwa msaada kweli ilihali hujui wao nje(majambazi)wanazo ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani walikuja kufanya Vita nyumbani kwako, Yani we kitendo Cha kumvunja mguu mmoja wao Basi wote ni lazima wakimbie
 
Sio kwamba wale walikuwa washafanya yao sasa wakawa wanarudi, na pengine maza nae labda aliibiwa humo humo na vibaka wengine.
Mtu mwenye chuma hawezi kuiba simu kirahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao walitoka kwenye matukio yao makubwa,kitendo cha kupeleka gari polisi maana yake ungefanyika msako wa mtu kwa mtu sasa kumbuka walikuwa na siraha ambazo kivyovyote vile sio legit so ilikuwa lazima wazuie huo mchakato lasivyo wizi wa simu ungepelekea kukamatwa kwa majambazi halisi.
 
Nilikuaga napendaga kusikiliza njia panda ya clouds kipindk kile yupo Sebastian Ndege, siku.moja wakawa wanamhoji jamaa ambae alikuaga jambaz akawa anaelezea alivyokuaga anaiba wanakata watu mapanga sasa akaulizwa ilikuaje ukaacha, akasema siku hiyo walivamia nyumba moja kama sikosei walikua watatu wakaruka ukuta wakavunja mlango wakaingia ndani kumbe ilikua nyumba ya wajeda wakakabiliana nao wakataitiwa kuna.mmoja aliuliwa kama sikosei na hao wawili waliinamishwa wajade wakavunja duka kwa kupokezana jamaa anasema toka kipindi hiko akaacha hiyo kazi
 
Kuna jambazi mmoja mstaafu mtu poa kinyama. Haendi msikitini wala kanisani ila ana roho safi zaidi ya mitume.

Ukimuuliza ilikuwaje ukawa unapiga zile mishe na kwanini umeamua kuachana nazo? Jibu atakalokupa utashika mdomo kwa mshangao!

Sent using Jamii Forums mobile app
Anajibuje

Sent using Uncesored Device
 
Kuna jambazi mmoja mstaafu mtu poa kinyama. Haendi msikitini wala kanisani ila ana roho safi zaidi ya mitume.

Ukimuuliza ilikuwaje ukawa unapiga zile mishe na kwanini umeamua kuachana nazo? Jibu atakalokupa utashika mdomo kwa mshangao!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ukiendelea kufanya hiv hata kwenye ndoa yako hakika utachapiwa sana kama wewe ni me ama utasababisha mme atafute mchepuko kama wewe ni ke......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma sana dodoma
Enzi hizo barabara ya kwenda aneti
(Sahv mnaita barabara ya kwenda arusha)barabara ilikuwa vumbi tupu Unapita izava wakati huo hakuna barrier ya police
Kuna sehemu katikati wanaita msitu mtungutu kulikuwa na uporaji sana.....Kabla ya kupita hyo njia nlishatonywa kuna majambazi huwa wanateka mabasi na kuwapukutisha
Nlichofanya tu wakati napita njia hiyo kiasi fulani cha fedha nlikuwa naweka chimbo kwenye basi nyingine ambayo najua ndiyo kodi yao nlikuwa nabaki nayo kuwazugia
Kuna siku wakati napita huko basi Lili kuwa linaitwa supersonic likapigwa tanchi jamaa walisema kila mtu atoe alichonacho mm wakanikuta Nna 80000/ wakakwala
Pole yao wale ambao walikuwa wanajifanya wagumu maana walikula kibaoo hadi wengine kutolewa meno
Matukio mengi hiyo 1 tu ...
Iko ya nyakanazi mzee
Ingine nlikutana wakati fulani kidodi nlikuwa natokea kilimbero

Ova

Hiyo ya Nyakanazi itakua bonge la tukio maana warundi sio watu wa mchezo mchezo

Hivi dodoma wapo fedex?

Sijakuelewa...kiasi kingine unakiweka kwenye basi lingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom