Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Mwaka fulani nakumbuka majambazi yalifunga mtaa wetu tulipokuwa tunaishi!.. Jamaa walivamia nyumba ya jirani kwanza walipiga risasi kama 2 angani na 1 wakaua mbwa then wakaingia ndani ya nyumba.
Walimchukua mzee mwenye nyumba na familia yake wakawafungia chumba kimoja then wakaanza hamisha samani za sebureni kama zao, nje wamepaki canter kabisa hapo mvua inapiga balaa.
Kuna mjeshi flani alitoka ulevini sasa njia ya kuelekea kwake lile canter likawa limeziba, akawa anapiga horn walitoe, akapiga moja angani alipoona wasumbufu. majamaa ndio kukimbia, yakaacha canter lao!.
Sasa yule mjeshi akaenda gonga kwa yule mzee anatukana kinoma inakuaje wanahama usiku, ndio wenye kujiweza tukaanza toka!.Kumbe mtaa mzima ulikuwa macho upo kimyaa unaangalia sinema!.
Kesho yake ikawa story ya mtaa ulevi wa mjeshi ulivyookoa mtu kugeuka masikini!. Sidhani kama ile familia watamsahau yule mzee mjeshi!.. Watu tukawa tunajiuliza wale jamaa wangeact kulitoa lori lao njiani yule mjeshi angekuwa mjinga wa mtaa.
 
Ilikuwa mwaka 2015 tuko na washkaji tunapiga mitungi ndani ya Pub moja ndogo hivi Jijini Dar es Salaam.Tungi ilikuwa imekolea haswa na watoto wakali pembeni bas ilikuwa hakuna mwenye muda.

Mida ya kama saa tano hivi kama mnavyojua mambo ya tungi nikawa nimetoka kushusha mafuta kidogo,ile narudi sasa nikakumbana na sauti ya ukali"oyaah kaa chini ms**nge" wajomba walikuwa wameshavamia.Raia wote walikuwa wako chini pale ndani huku anapita mmoja moja mbele anasaula kila alichonacho.

Kwa kuwa nilikuwa tungi sikuweza kung'amua kwa haraka kuwa lilikuwa ni tukio la Kijambazi,nikamjibu "mkalishe chini bibi yako ms**nge wewe"
Jamaa bila kusita alinivamia kwa speed ya supersonic na kunitandika na kitako cha bunduki kichwani paaah huku akiniacha nikianguka chini na kuvuja damu.Nimekuja kushtuka nipo hospital wanafanya harakati ili niweze kushwona.




Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mdogo wangu pamoja na rafiki yake wallikua anakaa kwenye nyumba ya bro ilikua nyumba mpya. Usiku wa manane jamaa wa mapanga shaa wakaanza kuvunja mlango. Basi madogo kushtuka usingizini wakaanza kupiga kelele kuita majirani wakidhani majamaa yatakimbia. Cha ajabu majamaa hayaongei chochote yanaendelea tu kuvunja kimya kimya tena bila story. Madogo kuona makelele hayasaidii wakabadili style wakaanza kuchimba biti na kutukana matusi ya nguoni...'waseng nyie ingieni tuwaonyeshe kazi, mnadhan sisi tunakaa kiboya humu..ingieni tuwafumue ubongo'. Wale majamaa wala wao hawaongei wanaendelea tu kuvunja bila story na mtu. Madogo mle ndani wakaona hawa jamaa mbona hawatishiki...ikabidi waanze kupiga maombi na kukemea pepo kwa sauti kuu na wakinena kwa lugha. Basi yale majamaa yakafanikiwa kuvunja yakaingia...yakawanasa vibao afu yakasepa na vitu kidogo na simu maana nyumba haikuwa na kitu na madogo walikua wanaenda tu kulala..
Duuuh[emoji848][emoji848]hizi nyumba mpya mpya hizi, wanatuogopeshan wengine tuliohamia majuzi[emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona hapa wengi wamekutana na vibaka tu Ila sio majambazi.Leo nimekutana na majambazi hapa Johannesburg South Africa kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.

Nimetoka Eastgate mall mida ya saa moja hivi nikaona ubahili kukodi Uber nikatembea kwenda home . Nimevuka mataa kuna gari (salon) imesimama baada ya taa nyekundu kuwaka ,mara kuna salon nyingine ikaja ikaizuia gari ya kwanza halafu watu watatu wakashuka na bunduki AK-47 kama sikosei.

Nilipigwa na butwaa halafu jamaa akaenda mlango wa nyuma wa upande wa abiria ,ile anafika tu kapigwa risasi akaanguka ,wale wawili waliobaki wakaanza kumimina risasi nyingi.Jamaa akajibu mwingine tena akaanguka chini.Muda huo nimekimbia kidogo halafu nimelala chini,najiburuza kama Rambo vile, jamaa wa tatu aliyekua amebaki akaenda kujificha nyuma ya gari huku wakiendelea kurushiana risasi na jamaa wa kwenye gari

Nimejiburuta umbali mrefu kweli nikainuka huku nikipiga mbio nyingi sana kwenda home.Risasi zisikie tu kwenye movie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikuwa peke yko au na Said Mpemba wa maskani MTN kwa sopu sopu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2012 kipindi icho ndo nachipukia usichana niliendaga coco wananchi
Tuliporwa sikuhiyo vibaya mno..pale katikati ya maisha cluba na coco nilivamiwa na vibaka machalii tu kama kumi na zaidi
Nilivyowaona wananijia nikatimua mbio nilikua nmebeba kihandbag cha nainai kina mnyororo mkubwa kilivutwa ule mnyororo ukanichana shingo
Nilijikuta kawe .
Nilipata mikasa sikuiyo mana nilikua sina mbuni nafikaje Om kwa mguu.
Tangu siku ile nmejifunza mambo mengi sana maishani
Sijawahi kwenda kwenye kusanyiko la watu wengi tukiachana na sherehe & kanisani
Beach sijawahi kukanyaga hadi leo ahilia mbali naishi Dsm yani nafanya tu kuyaona maji yale nikipita posta etc nikienda mahala natamani kubeba mabodyguard

Sent using Jamii Forums mobile app
Coco miyeyusho sana pale...Ni mojawapo ya beach ambao siipendi kutokana na vurugu zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2012 kipindi icho ndo nachipukia usichana niliendaga coco wananchi
Tuliporwa sikuhiyo vibaya mno..pale katikati ya maisha cluba na coco nilivamiwa na vibaka machalii tu kama kumi na zaidi
Nilivyowaona wananijia nikatimua mbio nilikua nmebeba kihandbag cha nainai kina mnyororo mkubwa kilivutwa ule mnyororo ukanichana shingo
Nilijikuta kawe .
Nilipata mikasa sikuiyo mana nilikua sina mbuni nafikaje Om kwa mguu.
Tangu siku ile nmejifunza mambo mengi sana maishani
Sijawahi kwenda kwenye kusanyiko la watu wengi tukiachana na sherehe & kanisani
Beach sijawahi kukanyaga hadi leo ahilia mbali naishi Dsm yani nafanya tu kuyaona maji yale nikipita posta etc nikienda mahala natamani kubeba mabodyguard

Sent using Jamii Forums mobile app
Vibaka hao jambaz hujakutana aisee
 
Nimechekaa mpk machozi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]formula2 ww ni mwehu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani nimecheka mpaka nalia... Daah huyo bibi ni shidah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Hili tukio sitakuja nilisahau maisha, lilisababisha nirudishwe nyumbani kwa kosa la kutoroka na kuhatarisha maisha yangu,


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi wakatimwingine nipo form 4 nilikua nakaba na kuchukua hell kunasiku nilimkaba babaake na rafikiyangu ananijua vizuri sababu nilitokea nyuma hakuniona nikaona Bora nimalize kabisa yani niuwe nilikaba mpaka akalegea nikajua tayari nimeua kumbe kazimia
Tuheshimiane basi Mkuu.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom