Kingfisher
JF-Expert Member
- May 22, 2015
- 5,140
- 8,399
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ulivyo jiita mnyama nikajua unaunyama Kweli Kama Savimbi ama Idiamiani kumbe paka tu[emoji1]
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ulivyo jiita mnyama nikajua unaunyama Kweli Kama Savimbi ama Idiamiani kumbe paka tu[emoji1]
Kama ni bure haina haja ya kufatana PM.weka hapa mwenye kutaka atachukua asietaka atawacha.Asante
Nimechekaaaaaaa!2017 .siku hiyo tulikua geto tumekaa tunapiga story.gafla tukasikia kishindo
Kuchungulia nje tukaona njemba mbili zinapita kwa kasi huku zimebeba mfuko wa salfet yani mmoja kabeba kushoto na mwingine kulia.
Kuona hivyo tukachukulia poa na kuendelea na story zetu.
Gafla baada ya dak15 baba wa jamaa ambae tupo nae akasikika anapiga kelele weziiii weziiii
Ikabidi fasta tusogee kufika pale mzee analalamika et walikuepo hapa hapa.kumbe mzee alibamizwa ukutani akazimia.
Tulishindwa kujizuia tukaanza kucheka
Sent using Jamii Forums mobile app
Polisi wetu wakifyatua lazima mtu afe!Ilikuwa miaka ya tisini mwishoni maeneo ya mbezi beach,vibaka walisumbua sana kuanzia saa mbili usiku...wanaanza kurusha mawe kwenye paa za nyumba kwa fujo...na ikifika saa 6 wanavamia tunawakurupusha wanakimbia...jirani yangu alikuwa analindwa na mjeda lakini bado hawakuogopa walivizia yuko eneo lingine ndani ya fence wanaruka ukuta upande mwingine wanaingia wanadokoa..siku ya siku mjeda akagundua mchezo wao....akawalia timing hawakujua kajificha wapi...akatangulia mmoja akadumbukia ndani....kosaa...mjeda kaikoki SMG kamwambia tulia hapo hapo....kibaka kaanza kusema kausha basi mshikaji...mjeda kampa moja ya mkono,kibaka chini lakini bado akawaeza kukurupuka akapanda fensi kurukia nje... akala risasi nyingine ya mkono... akakimbilia kwenye uchochoro mjeda nyuma akampiga ya mguu kibaka akaaanguka...wakati hayo yanatokea sisi tupo tunasikilizia tumezima taa zote...baada ya mda mjeda akaja akanigongea akasema tayari....tukatoka nje mpaka kibaka alipolala...hajafa ila mikono yote miwili na mguu vimevunjika...na anaongea...sikio moja hana (tulimuuliza akasema alikatwa siku za nyuma kwenye tukio)...unatokea wapi ...Mwananyamala...mjeda(mwenyeji toka mkoa wa mara) alihakikisha anataja wenzake wote baada ya kumtonesha madonda yake kwaxkumchokonoa kwa mtutu!baadae walikuja polisi wakamchukua,kwa jinsi alivyokuwa na roho ngumu,huyo kibaka alikaa muhimbili miez 3 licha ya kuwa kipindi hicho kulikuwa na mgomo wa madaktari kutowatibia vibaka baada ya daktari mwenzao mmoja kuuawa na majambazi.....lakini baada ya tukio hilo hakuna kibaka yeyote alikanyaga maeneo hayo kwa miaka kadhaa!
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ninja!Nakumbuka mwaka 2011 Siku Ya Eid pili nilienda Wet 'n' Wild Beach with Family, ilivofika Jioni saa 12 rafki zangu wakaniforce Niende South Beach... Nyumbani nilikatazwa kutoka ila sikuskia na Nilikosa gari ya kunipeleka kila mtu analalamika lile nyomi la magari Kigamboni siku za Skukuu inakua ZOGO.... Basi nilitaka kukodi Taxi lakini mwenye Taxi alikataa kunipeleka kigamboni akidai kwamba kuna foleni sn labda aniache kivukoni halafu nikishuka Pantoni ntachkua Bajaji au Pkpk mpk South Beach. Nikafata ushauri wa mwenye Taxi Sikujua km kuna Mabalaaa huko Kigamboni siku za Skukuu maana siku za Skukuu sisi huwa tunaenda Beach za hukuhuku hatuvuki.
Nilivoshuka Pantoni ilikua mida ya saa 1 usiku mapema tu, watu kibao km mkutano wa siafu! Bajaji zilikua hamna kituoni zilibaki pkpk tu, ikabidi nipande pkpk nilikua nimevaa Jeans, Blauz refu na Handbag yangu kwapani magari yalikua yanatembea taratibu mno hakuna pa kukanyaja Watu wengi walikua wanatembea kwa miguu, kumbe wale wanaotembea wengi ni wezi wamejichanganya kwenye umati wa watu. Njiani nilikua naona wanaharass wanawake na kuwashika shika, mara gafla nikashtukia mwanaume mmoja anaivuta handbag yangu, sikumuachia na mm nikawa naivuta.. Vuta nikuvute hatimae nikamshinda. Ndio yule Bodaboda ananiambia ooh 'samahani Dada nilisahau kukutahadharisha km kuna wezi shika vzr mkoba wako,' nageuka nyuma yule mwizi anaikimbiza pkpk yetu tena yupo na wenzie km 3 hivi na mbaya zaidi foleni kubwa mno magari yanatembea very slowly, nilichanganyikiwa sikujua hatma yngu itakuaje, nikageuka upande wangu wa kulia kulikua kuna gari (pickup) ipo kwenye foleni pia lakini ya Kurudi mjini yaani inaelekea magogoni, (nyuma kwenye hio pickup kulikua kuna watoto wamekaa km 4 hivi wadogo) nilijishtukia tu nimesimama juu ya Bodaboda nikamwambia mwenye Pkpk asogeze karibu na ile gari nikairukia ile gari ya watu mwenye bodaboda ananidai hela yake nikamlipa kisha nikamwambia mtoto mmoja aikalie handbag yangu ili aifiche, wale wezi walivofika walizunguka ile gari wanatafuta Handbag yangu hawaioni Bahati nzuri Dereva wa hilo gari akashuka alikua mtu mzima na ana mwili kiasi akawauliza mnataka nn kwenye gari yngu? Wakakimbia, yule Mzee akaanza kunihoji maswali nikamuelezea mkasa mzima wakanionya yy na mkewe siku nyengine nisirudie tena kwenda kigamboni siku za skukuu bila gari ya Family ni hatari. Tena walinambia una bahati sn sisi tulikua tunatoka Dar es salam Zoo, tulikua hatutaki kupita hii njia, tulipanga tuzunguke njia ya Mbagala kukwepa foleni ila nashangaa sielewi kitu gn kimenipitisha huku kumbe Mungu alipanga tuje tukunusuru ww. Walinifikisha mpk nyumbani na wao wakaendelea na safari yao, Dah. Mwenyezi Mungu awazidishie kheri popote walipo.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Naomba nitupie PM kama huwezi weka hapa.
Kama nakuona vile unavyoruka, sometimes fear could make you do wonders!Hahahaa usinipe kichwa Mkuu[emoji23][emoji23]
Kama nakuona vile unavyoruka, sometimes fear could make you do wonders!
- KANA -
Le masai dada... Upo? Ulipotelea wapi best?mkuu ingekua kenya talks ningekwambia leta hiyo hekaya
i mean story yako yafaa uweke uzi wake
Mzee mlinzi akawa jambazi ghafura[emoji3][emoji3][emoji3]Wale vibaka wangu walikuwa wajinga sana..........2001 hiyo nimetoka zangu kupiga liquid narudi home kama saa 7 hivi ucku, nilipokuwa naishi kuna umbali kidogo kutoka barabarani, dereva taxi kanishusha nikaanza kukata vichochoro kuelekea nyumbani, ghafla nikamulikwa usoni na tochi yenye mwanga mkali sana halafu ikatoka amri kali eti:- simama hapo hapo na ujisachi mwenyewe utoe kila ulichonacho mfukoni........yani sikujiuliza mara mbili mbili, niligeuka kwa kasi na kufyatua mbio kali sana ambazo sijawahi kukimbia.
Kuona ivo na wao wakaniunganishia kuanza kunikimbiza halafu mbaya zaidi wakaanza kuniitia mwizi, mi kusikia ivo nikapunguza mwendo hatimae nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, kuona natembea na wao wakaanza kutembea na hawapigi tena kelele za mwizi, nilipoona wananikaribia nikachomoka tena mbio kali......zoezi likarudia lile lile la kupigiwa kelele za mwizi, bahati nzuri natokeza barabarani na gari ya police hii hapa, nikawaelezea tukarudi hadi walipoanza kunikimbiza lakini hakuna mtu, basi wakanisindikiza hadi nyumbani.
1993 Tabora hiyo jamaa yangu mmoja kaja mjini kupokea pesa yake ya mauzo ya tumbaku, akawa na mipango mingi balaa ikiwemo kununua baiskeli mpya, kununua radio kaseti ya Lasonic na kuongeza mke wa tatu..........hakuna hata mpango mmoja uliotimia, usiku wa hyo aliibiwa pesa yote sh 100,000/= na baamedi aliyelala nae gesti (nadhani ndo alikuwa anamfanyia intavyuu kama anafaa kuongezwa kuwa mke wake wa tatu, tangu siku hyo jamaa yangu huyo alishikwa na uchizi akatoweka nyumbani hadi tulipokuja kupata taarifa za kifo chake cha kugongwa na gari.
Juzi juzi tu hapa kuelekea kipindi cha sikukuu za krisimasi na mwaka mpya kundi la vibaka wapatao kama 17 hivi walivamia kwa jirani yangu aliyekuwa kauza kagari kake kamechakaa chakaa kwa sh milioni 6, wale wapuuzi wakataka kuja kuchukua zile pesa kama vile walimuwekeza........kwa mara ya kwanza ndo nilikatumia vizuri ka manati kangu ka kizungu, nilimkongoroa goti mmoja wao na wengine wakakimbia, yule tulimmalizia pale pale kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali.
2007 kuna majambazi yalivamia mtaa flani wenye maduka mengi, sasa ile tabia ya mlinzi mmoja analinda karibu maduka 40, wakamkamata mzee wa watu wakaenda nae hadi kwenye mojawapo ya maduka anayolinda wakamkazimisha aanze kuvunja, zoezi lilipokamilika wakamlazimisha aanze kusomba vitu anapakia kwenye gari la majambazi.......ile wanamalizia mara paaaaap na mwenye duka akatokeza akamuona yule mzee mlinzi wa duka lake yupo kwenye harakati kupakia vitu kwenye gari ya wale wezi, jamaa akafyatua risasi hewani, wale wezi wakawahi kwenye gari yao ili wakimbie, na yule mzee mlinzi na akaona hapo sio pa kukaa tena, akadandia kwenye gari ya wale wezi akaondoka nao...........!!!!!!!!!!!!!!!!
komando kinjekitile ngwale
kenya haha kwenye JamiiForums.com
kenyatakkenya haha kwenye *********
shukrani mkuu
Ule ulikuwaga mchongo braza na waliohusika sina hakika kama wapo uraiani