Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Sidhani kama unafahamu tofauti ya mwizi au wezi na jambazi aisee! Hao uliokutana nao katika matukio hayo ni wezi na sio majambazi, mziki wa (ma)jambazi sio wa kitoto aisee! Nikiwa na muda nitasimulia!
Tunasubiri mkuu upate muda, tupate ushuhuda wako. Tuzidi kujifunza na kuchukua tahadhari.
 
2017 .siku hiyo tulikua geto tumekaa tunapiga story.gafla tukasikia kishindo

Kuchungulia nje tukaona njemba mbili zinapita kwa kasi huku zimebeba mfuko wa salfet yani mmoja kabeba kushoto na mwingine kulia.

Kuona hivyo tukachukulia poa na kuendelea na story zetu.

Gafla baada ya dak15 baba wa jamaa ambae tupo nae akasikika anapiga kelele weziiii weziiii

Ikabidi fasta tusogee kufika pale mzee analalamika et walikuepo hapa hapa.kumbe mzee alibamizwa ukutani akazimia.

Tulishindwa kujizuia tukaanza kucheka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimegundua pombe ndio kisababishi kikubwa cha watu kukutana na majambazi hasa nyakati za usiku. Miaka kadhaa iliyopita majambazi walivamia bar ambapo bro wangu alikua akikata kilaji. Wakaamrisha watu wote walale chini. Bro alikua anatembea na mguu wa kuku nafikiri aligoma akataka kupambana nao. Masikini walimchapa shaba kisha wakasepa wala hawakuiba tena. Alikimbizwa hospitali lakini siku iliyofuata aliaga dunia.
 
Maskini bora angekubali kulala chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka fulani nimetoka mbeya na Mr saa saba za usiku, Kufika maeneo fulani karibu na morogoro kuna kona fulani hivi ya kishkaji, sijui Mr alikua na nini kichwani hakuangalia mita kadhaa mbele, mi nimelala zangu nakula usingizi kwa raha zangu, gafla nikahisi kama gari imepaki gafla, nikasikia ananiambia amka amka! Kufungua macho naona malori mawili yamepaki pembeni ya njia mbele ya malori kuna gari dogo nayo imepaki halafu kuna bongee la gogo katikati ya barabarani Mr akanambia kuna tukio la utekaji hapa either linaendelea ama kimeisha muda si mrefu,Salaleee usingizi ulinitoka wote, nikakwambia Mr turudi tulikotoka akanambia No, kwenye matukio kama Haya huwa haturudi nyuma. Nilipaniki nusu nimnase kibao nikamwambia sa tusirudi nyuma tubaki hapa watushike na sisi? Akasema anavoona yeye lile tukio limeshaisha na wenye magari haya either wamepaniki wamekimbilia vichakani ama watekaji wamewachukua wameondoka nao... nililoa jasho hadi pichu, mi kwa akili yangu nilikua nafikiri wamewakusanya wenye magari wako nao mahala wanatuangalia na watajitokeza sio muda kutuchua na sisi Ndio maana nilikua namsisitiza Mr turudi tulikotoka ye anamsisitiza hakuna kurudi . Akanambia ye anashuka ajaribu kutoa gogo tupate pakupenya, hivo mi nishike wheel ikitokea wakajitokeza wakamkamata mi nirudishe gari reverse vyovyote vile bora nipate ajali ila wasinikamate nikiwa mzima anasisitiza maana wanaweza kunibaka. Haya mabishano yote yalifanyika kwa dakika kadhaa... mwisho kishingo upande nikamkubalia ashuke. Akashuka nikakamata usukani, nikafunga belt nikajiandaa huku natetemeka hakuna mfano. Ile ameshuka tu akakamata gogo naona ni zitooo hata haliwezi akatokea kijana porini amepigwa vibaya sana kumbe alikua mmoja wa madereva waliotekwa, kidogo wengine wakajitokeza wakawa wanaelezana kilichotokea, mwisho wakakubaliana watembee kwa kuongozana hadi wakutane na Barrie ya mapolisi watoe taarifa. Wale madereva na makonda wao walikuwa wamepigwa sana wanavuja tu damu, nakumbuka mmoja sikio la kulia lilikua limelegea kama linataka kudondoka na kwa wakati huo niliona kama hasens chochote zaidi ya kuona tu midamu inamvuja. Basi ndo hivo tukaondoka kwa kuongozana tulifika Barrie ya polisi karibu kabisa na moro tukawaacha sie tukasepa zetu, tumbo liliniuma siku hiyo sitasahau sijui ni sababu ya uoga.
huyo jamaa anaroho ngumu aise michezo hio asirudie atakuja kupewa adhabu ya kutoa beria wale jamaa ni nyoko ujue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimegundua pombe ndio kisababishi kikubwa cha watu kukutana na majambazi hasa nyakati za usiku. Miaka kadhaa iliyopita majambazi walivamia bar ambapo bro wangu alikua akikata kilaji. Wakaamrisha watu wote walale chini. Bro alikua anatembea na mguu wa kuku nafikiri aligoma akataka kupambana nao. Masikini walimchapa shaba kisha wakasepa wala hawakuiba tena. Alikimbizwa hospitali lakini siku iliyofuata aliaga dunia.
hio mimi nilishuudia arusha jamaa alikua mbishi hivyo hivyo aise walimpa ya kichwa moja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa miaka ya tisini mwishoni maeneo ya mbezi beach,vibaka walisumbua sana kuanzia saa mbili usiku...wanaanza kurusha mawe kwenye paa za nyumba kwa fujo...na ikifika saa 6 wanavamia tunawakurupusha wanakimbia...jirani yangu alikuwa analindwa na mjeda lakini bado hawakuogopa walivizia yuko eneo lingine ndani ya fence wanaruka ukuta upande mwingine wanaingia wanadokoa..siku ya siku mjeda akagundua mchezo wao....akawalia timing hawakujua kajificha wapi...akatangulia mmoja akadumbukia ndani....kosaa...mjeda kaikoki SMG kamwambia tulia hapo hapo....kibaka kaanza kusema kausha basi mshikaji...mjeda kampa moja ya mkono,kibaka chini lakini bado akawaeza kukurupuka akapanda fensi kurukia nje... akala risasi nyingine ya mkono... akakimbilia kwenye uchochoro mjeda nyuma akampiga ya mguu kibaka akaaanguka...wakati hayo yanatokea sisi tupo tunasikilizia tumezima taa zote...baada ya mda mjeda akaja akanigongea akasema tayari....tukatoka nje mpaka kibaka alipolala...hajafa ila mikono yote miwili na mguu vimevunjika...na anaongea...sikio moja hana (tulimuuliza akasema alikatwa siku za nyuma kwenye tukio)...unatokea wapi ...Mwananyamala...mjeda(mwenyeji toka mkoa wa mara) alihakikisha anataja wenzake wote baada ya kumtonesha madonda yake kwaxkumchokonoa kwa mtutu!baadae walikuja polisi wakamchukua,kwa jinsi alivyokuwa na roho ngumu,huyo kibaka alikaa muhimbili miez 3 licha ya kuwa kipindi hicho kulikuwa na mgomo wa madaktari kutowatibia vibaka baada ya daktari mwenzao mmoja kuuawa na majambazi.....lakini baada ya tukio hilo hakuna kibaka yeyote alikanyaga maeneo hayo kwa miaka kadhaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nacheka kama mazuri,,
2017 .siku hiyo tulikua geto tumekaa tunapiga story.gafla tukasikia kishindo

Kuchungulia nje tukaona njemba mbili zinapita kwa kasi huku zimebeba mfuko wa salfet yani mmoja kabeba kushoto na mwingine kulia.

Kuona hivyo tukachukulia poa na kuendelea na story zetu.

Gafla baada ya dak15 baba wa jamaa ambae tupo nae akasikika anapiga kelele weziiii weziiii

Ikabidi fasta tusogee kufika pale mzee analalamika et walikuepo hapa hapa.kumbe mzee alibamizwa ukutani akazimia.

Tulishindwa kujizuia tukaanza kucheka

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
Daahh kama masihara ila umenichekesha sana unakimbia unazunguka
 
2017 .siku hiyo tulikua geto tumekaa tunapiga story.gafla tukasikia kishindo

Kuchungulia nje tukaona njemba mbili zinapita kwa kasi huku zimebeba mfuko wa salfet yani mmoja kabeba kushoto na mwingine kulia.

Kuona hivyo tukachukulia poa na kuendelea na story zetu.

Gafla baada ya dak15 baba wa jamaa ambae tupo nae akasikika anapiga kelele weziiii weziiii

Ikabidi fasta tusogee kufika pale mzee analalamika et walikuepo hapa hapa.kumbe mzee alibamizwa ukutani akazimia.

Tulishindwa kujizuia tukaanza kucheka

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nimecheka Kwa sauti[emoji12] [emoji12] [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 98 nikiwa kijijini nikaamua kwenda kusalimia kwa ndugu wa karibu mbali kidogo na nilipokuwa. Huko niliwahi kwenda na wazazi zamani hivyo sikuwa napakumbuka vizuri. Nikafika kwenye kamji mida ya usiku wa saa 4 hivi na enzi hizo hakuna bodaboda na usafiri tegemeo ni lift za watu wa misheni. Kwavile mwendo wa kufika kule kutoka kwenye hako kamji ni kama 1 hr nikaona nitembee tu nikalae huko. Wenyeji pale wakanishauri nichukue gesti nilale maana kuna ujambazi wa kutisha na hasa kuna kundi la majambazi wakiongozwa na mtu anayeitwa Mwamba ni hatari ukikutana nao. Huyo Mwamba unaambiwa akitaka hela anakuja anakutaarifu hadi sehemu ya kumuwekea aje achukue mwenyewe. Ile kibishi na umjini nikawaambia nitatembea bado mapema. Mdogo mdogo after kama 25 min kwenye kimteremko giza nene na misitu nikaona mtu anatembea kuja nilipo, sikuhofu wazo likaja nimuulizie wenyeji wangu ili nijekupitiliza. Alivyofika nikasalimia nikamuuliza bahati nzuri anawafahamu akasema umefika twende nikupeleke. Hatua kadhaa akaniambia lete mzigo nikusaidie nikashukuru na kuanza kujiongelesha nikamwambia nasikia huku kuna jamaa anaitwa mwamba anaogopwa kijiji kizima kuwa ni mtu hatari, na jinsi watu walivyoshauri nilale town niondoke asubuhi nijekukutana nae. Basi najiongelesha njemba inatembea tu sigara mdomoni. Baada ya mwendo kidogo tukafika kwa wenyeji wangu nikagonga mlango. Mtu wa kwanza kufungua mlango na kutuona alitoka nduki na kushtua wengine kwa kile kishindo ikabidi waje mlangoni kutuona wote wakawa wanatetemeka huku wanatukaribisha. Nikashangaa ile hali ya wenyeji wangu alafu ile njemba ikaaga ikaondoka zake. Ndugu zangu wakaanza kunihoji unajua umekuja na nani, huyo ni kiongozi wa majambazi maarufu kwa jina la Mwamba! Dah, nywele zilisimama hasa nikumbuka nilivyokuwa nikipiga nae stori. Dah kila nikumbuka nacheka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
We unajiongelesha mwamba anakusikiliza tu uzingue
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah nimekumbuka mbali sana teh teh teh teh teh,.. Kwa wale wa kazi wa mwanza kama mnakumbuka, kuna kipindi flani majambazi walikua wanavamia mida ya Jioni Jioni, tena walikua wanafunga center nzima wanaingia duka Kwa duka,

Siku Hiyo niko maeneo ya nyambiti Hapo napata uji Kwa Maza mmoja maarufu sana Hapo, ilipigwa chuma juu Daah Sikumbuki vizuri, hila nilijikuta home Na kikombe cha uji,..

Hila wanadai wale majambazi walikua wanalipa kisasi, maana walikua wanaingia dukani hawachukui Chochote hila wanachanganya mafuta ya kula na ya taa,...unga wa mihogo wanachanganya Na sembe..
 
Back
Top Bottom