Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwa sasa Hiki ndo kisa cha kuchekesha kuliko vyote humu[emoji23][emoji23]


Mkuu nimecheka sanaaa!!


"utamu wa uji ni kutingisha bakuli"
 
Mkuu pole Sana....badae ikawaje sasa ulivyorudi bongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
kabla ya hayo mabalaa tulikuwa na maisha mazuri ya wastani kiasi kwamba watanzania wengi hasa kutoka Rungwe vijiji walivyokuwa wanatokea wazazi na vya jiran wengi wao walikuwa wanakuja kuanza maisha Lusaka walikuwa wanafikia kwetu.Nilikuwa na akina shsngazi wengi,akina mjomba ,ba mdogo au ba mkubwa na akina ma mdogo.

Sasa maisha yalipobadilika na majanga yalipozid hao hao walileta taarifa Tanzania,kwa hiyo ndugu zake baba wakaja kumuona ndugu yao.wazazi wangu walikuwa maarufu sana kwa Lusaka hasa mitaa ya wanyakyusa.alikuja shangazi na baba mkubwa.mdogo wangu wa pili kunifata aliondoka na baba mkubwa me nikaondoka na shangazi tena kwa kumlilia.kwani wakati anakuja alituletea matunda ndizi na me nilikuwa napenda sana ndizi kwa akili ya utoto nikadhani anakotokea ni kuzuri zaidi.

Tulikuja kwa Treni ya Tazara tukianzia Capri mposhi mpaka Mbeya,then tukalala Tukuyu mjini kwa babu yngu mzaa mama siku iliyoafuta tukaanza safari kuelekea masoko kijijini kwa Babu mzaa baba.

Nilikuta migomba mingi sana hivyo ndizi nyingi sana zingine zinaozea shambani na kuliwa na nyani maana miaka hiyo biashara ya ndizi haikuwa kubwa kama leo.nilifurahi sana.nilikula ndizi ,maziwa mpaka kuvimbiwa.baba mkubwa alikuwa na ng'ombe ,mbuzi wengi sana hivyo maziwa yalikuwepo ya kutosha.

Tulifika Tukuyu April 24 1991 nakumbuka ilikuwa jmatano siku ya pili watoto wote wakaenda shule me nikaenda kuchunga ng'ombe na baba mkubwa.nikafurahia hiyo hali kwa siku kadha za mwanzo lakini upweke ulipozidi ndani ya week ya kwanza ikaanza kuwa shida.kwanza nimetoka mjini ambako kuna kila kitu umeme n.k naangalia Tv na film kuna miundo mbinu yote ya kisasa kwa ajili ya watoto kucheza sasa nipo sehemu ambayo ni kijijin na tofauti kubwa na nilikotoka, hakuna hata umeme.hakuna watoto wenzangu wa kucheza nao wote wapo shule.

Hali hiyo ilipelekea nianze kutamani nirudishwe Zambia nikawa mtoto wa kulia muda mwingi.lakini hawakunirudisha, kidogo kidogo nikazoea mazingira mapya lakini kwa taabu sana.nilitoka zambia nikiwa naingia darasa la pili lakini uku Tanzania nikaanzishwa darasa la la kwanza na ilikuwa mwezi wa nane.

Lugha ya kiswahili kwangu ilikuwa changamoto kubwa kwenye mawasiliano lakini nilikuwa najua kuzungumza kinyakyusa vizuri tu kwani ndio ilikuwa lugha ya ndani kwa familia yetu.na pia Lusaka kuna wanyakyusa wengi sana hata kabla ya uhuru.mitaa ya Mandevu,Chaisa,kanyama ,chipata ,Goerge, Matelo ambako ndiko nilikokuria toka mchanga mpaka miaka 3 ni mitaa iliyojaa wanyakyusa (wao wanaita mwachusa)kiasi hata kwenye masoko yao wakati huo wafanya biashara wengi kuanzia ndogo mpaka kubwa wakiwa wanyakyusa wakiwa huru kuzun
gumza lugha yao.


Ilipofika December matokeo ya mtihani nikawa wa 32 kati ya wanafunzi 88.lugha nikaanza kuijua vizuri.
Lakini nilipozoea maisha ya uku Tanzania nikaja kugundua wale ndugu wengi wa kule Zambia hawakuwa ndugu na wazazi wangu, wengi wao walitoka kijiji kimoja au kijiji jirani ,kulikuwa na shangazi yangu mmoja kule Zambia nilikuwa nampenda sana na tulikuwa tunaishi nae pale nyumbani yeye na watoto wake wawili baada ya yeye kufiwa na mumewe na hali kwake ikawa ngumu baba akamchukua pamoja na wanae,nilpofika huku Tanzania,baada ya miaka kama mitatu na yeye alirudi Tanzania akawa anakuja kunitembelea ndipo nikagundua hakuwa ndugu wa baba wa damu ila walitoka vijiji jirani.
Nikajifunza upendo walionao Wanyakyusa ugenini.Hakika wanapendana.lakini pia kwa Asili Unyakyusa ni Nchi ya Upendo na Ukarimu.
 
STUNTER said:
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nimecheka saaaana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamaa alituchezeshea kichapo kikali mnoo alafu lipo uchi kabisa yaani..😂😂
 
2013 Dodoma hahahaa nicheke kwanza lol..nilikutana na vibaka wa4 sehemu mbaya sana aiseee siji kusahau mida ya kama saa 4-5 hivi usiku jinsi nilivyonasuka acheni tuu MUNGU aitwe MUNGU ule ni ushuhuda tosha kwangu maana wangeweza kunicheza karata zote na kuiuza roho yangu lakini niliona mkono wa Bwana wa majeshi,. ndipo ninapokumbuka neno la MUNGU lisemalo "adui zako wakikujia kukuangamiza watatawanyika kwa njia saba"...

Kumtumikia MUNGU kuna faida.
Walokole bhana hamwishi vituko,badala ya kutupa mkasa unaanza kutupa vifungu vya biblia..
 
Mwaka 2012
Joka ndio nilikuwa moto kwa watoto warembo nikiwa kidato cha sita huko Kilimanjaro.

Nilitoka na manzi mmoja mkali mtoto wa Kigogo wa Chuo cha Polisi pale Moshi. Rafiki zangu walinionya kuwa niachane na Shani lakini Joka nilikuwa nimeshakolea.

Dogo alikuwa Mawenzi kidato cha tano Boarding. Kila ijumaa alikuwa akija Ghetto Na kurudi Jumapili. Kama unavyojua ujana basi nikawa najiona bonge la mjanja nikiwaoshea Washikaji. Manzi alikuwa amesimama haswa.

Siku moja tuliamua kwenda Waterfall ya Marangu. Na hapo ndipo nilipoonja Joto ya jiwe. Tuliondoka pale mjini mimi Na Shani. Tukafika Marangu Mtoni. Tukashuka. Tukaenda kuchukua Room kwenye hotel ya Kill Hotel kama unaenda kupanda Mlima Kilimanjaro kule.

Hao tukatoka. Tukachukua boda boda mpaka Waterfall ya Marangu. Ilikuwa mida ya jioni watu walikuwa wachache kama kumi na tano hivi.

Tukasaura nguo watu ndani. Punde walikuja washikaji wanne vijeba haswa. wakawaweka chini ya Ulinzi Wale waliokuwa nje ya maji. Walitoa Bastola na kutoa amri ya sisi kutoka ndani ya maji.

Nilikuwa mbishi. wakapiga Risasi moja juu ndipo nikaona hapa hawatanii. Tukatoka Mimi na Shani. Nilipigwa mitama nikahisi kiuno kimevunjika. Shani alipiga makelele tuu. Walipoona Shani anazidisha Kelele walimzaba Kofi akapoteza fahamu hali iliyonifanya nidhani Amekufa. Niliwabwatukia nikitumia nguvu kumfuata aliyempiga Shani. Ghafla nilihisi kitu kizito kichwani na papo hapo nilipoteza fahamu.

Nilikuja kuzinduka Asubuhi nikiwa kando ya Mto Karanga. Nikiwa sina nguvu kabisa.

Sitokuja kisahau. Mapenzi yaacheni tuu
Bila shaka ulisoma Majengo sec. wewe jamaa.hahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah pole sanaa mwana Jf
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1990 uko katika mtaa wa Mandevu compound Lusaka nchini Zambia,tulikokuwa tukiishi baba na mama wote wakiwa wafanya biashara.
mwaka 1990 uko zambia kulikuwa na vuguvugu la mabadiliko kisiasa,wananchi walikuwa wamechoka na maisha magumu baada ya uchumi kuyumba na bidhaa kupanda bei.Zambia chini UNIP na Kaunda wananchi walikuwa wanategemea sana msaada wa serikali kuendesha maisha yao.sasa bei ya shaba ilipoporomoka serikali ilishindwa kumudu kugharamia sehem ya mahitaji ya wananchi.wananchi wakaingia mtaan machafuko yakawa makubwa kiasi cha serikali kushindwa kudhibiti.
ikatangazwa amri ya hatari mwisho saa kumi na mbili jioni kutembea mtaani.Askali kutoka Tanzania wakashika doria mitaa mingi ya Lusaka.
siku moja muda wa saa moja usiku tukiwa ndani zikasikika risasi nje ya nyumba yetu,baba akaenda kufunga vizuri zaidi mlango wa nje,wale majambazi wakagonga kioo cha dirisha kwa kitako cha bunduki wakaingiza bunduki dirisha na kuamrisha mlango ufunguliwe na taa zizimwe.wakatoa amri kama baba akalale.
walikuwa wamevalia mavazi ya kijeshi na ya jeshi la Zambia.walionekana wanamfahamu vizuri mama shughuri zake.na walikuwa wamempania mama kwani wakati huo baba hali yake kibiashara haikuwa nzuri ilikuwa miezi michache tu imepita tangu avamiwe na kupolwa kila kitu na majambazi,kwa hiyo hawakushughulika nae.
wakikuwa kama 7 walioingia ndani wakadai wengine chakula wengine mmojanakatoa amri wafanye kilichowaleta.wakataka pesa mama akawapa alizotoka nazo dukan wakamwambia sio hizo hazitoshi wakaingia chumbani ambako baba alikuwa amelala baada kuamrishwa hivyo wakachukua fedha zote zilizo kuwepo.
Asubuhi yake mama akaenda kituo kikuu cha polisi kureport baada ya maelezo ikabidi liitishwe gwalide la utambuzi bahati mbaya mama hakuwatambua wale wahalifu.ikawa mwanzo wa maisha kuyumba.
wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 9 tu.mwaka ulifuata nikaja Tanzania.SIWEZI KUSAHAU KAMWE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama unafahamu tofauti ya mwizi au wezi na jambazi aisee! Hao uliokutana nao katika matukio hayo ni wezi na sio majambazi, mziki wa (ma)jambazi sio wa kitoto aisee! Nikiwa na muda nitasimulia!
 
Back
Top Bottom