Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda


We jamaa umetisha
 
Mwaombataa mkombe
 
Wakuu habari ya mapumziko ya mwisho wa Juma,

Soko la nguo za mitumba la Ilala ni maarufu sana hapa jijini kwa kuuza nguo kwa mfumo wa mnada hasa majira ya alfajiri hadi saa 3 asubuhi.

Kutokana na upatikanaji wa nguo za mtumba kwa bei nafuu, watu wengi hujazana hapo hasa wauza nguo wakichanganyikana na vibaka hapohapo.

Nakumbuka ilikuwa karibu tunafungua shule (Boarding) huko mkoani sasa Siku hiyo alfajiri nimejihimu nkaenda kununua jeans za kwenda nazo shule.

Nilikuwa nimevaa shati lenye mifuko miwili hivyo nikasema kwa namna kulivyojazana watu wacha nitoe pesa zote niweke kwenye mifuko ya shati halafu wallet ikabakiwa na elfu 11 na vitambulisho.

Nikaona haitoshi nikaamua kutoa wallet mfuko wa nyuma nikahamishia mfuko wa mbele ymwa jeans niliyokuwa nimevaa. Asee huwezi amini jamaa walinipiga ile wallet nilichoka na sikuamini yani ile kufumba na kufumbua dah.

Nikasema pale ni noma!!
 
Leo maeneo ya manzese nimesikia milio ya risasii[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji2089][emoji2089]
 
haaah haaa Haaaa bora angepokea laki yake tu
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Hii comment imenichekesha sina mbavu.
Eti nyie nitawaletea noma hadi mkasimulie kwenu.
Mwingine anapigwa na bapa halaf anaulizwa kwa nini hauna hela mfukoni yeye anajibu"Mimi mgeni hapa mtaani"
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Hii comment imenichekesha sina mbavu.
Eti nyie nitawaletea noma hadi mkasimulie kwenu.
Mwingine anapigwa na bapa halaf anaulizwa kwa nini hauna hela mfukoni yeye anajibu"Mimi mgeni hapa mtaani"
Mlioteswa Na vibaka mmepotelea wap
 
Mwaka sitautaja. Saa tano usiku nimeshuka bus la kiwanda cha ALAF njia panda Mwananyamala naelekea Kinondoni B. Dereva kagoma kunipeleka hadi pale mitambo ya umeme Bagamoyo road, bus likaelekea Mwananyamala. Nilitembea kama dakika kumi mita ishirini mbele vibaka watatu wametanda barabarani. Sina kitu mkononi lakini muguuni nimevaa buti nzito za kiwandani. Nilipata mstuko, uchaguzi wa kurudi nyuma au kukimbia haukuwa sahihi, maana ingekuwa rahisi kwao kunifikia. Kwa haraka niligundua tunalingana vimo, na hapo ni miezi minne tangu nimalize mwaka mmoja wa JKT kwa mujibu wa sheria, nikajesemea moyoni ntakufanao. Nilichofanya ni kuongeza kasi ya kuwafikia na kukita buti kwa nguvu, mikono kama nacheza paredi.
Plan yangu ilikuwa atakaenisemesha ni kumpa pigo la kuzirai, atakae nishika ni kumtoa nyama kwa meno. Nilipo wakaribia niliwasikia wakisema he mtu mwenyewe kama askari walinipisha bila neno lolote. Hata hivyo, kasi ya mapigo ya moyo ilikuwa juu sana, sijui pangetokea nini kama wange anza vurugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…